Tafuta/Search This Blog

Tuesday, January 27, 2009

AMINI USIAMINI kumbe Tanesco wako juu.


Eti Tanesco wameshindwa kuhudumia nguzo ktk mitaa yetu. Hebu angalia huku kwa wenzetu ndo utajua kweli Tanesco yao inafanya kazi au haifanyi!!!

HOW DO THE IRAQIS HIDE FROM THE AMERICANS?

Tuna mambo mengi ya kumshukuru Mungu, moja wapo ni hili, Sisi hata ukutaka Kumwabudu Mungu wako chini ya Mti, hakuna atakaye kusumbua, ila hata kufika katika makanisa na misikiti ni ngumu. Ona wenzetu wanavyotafuta njia za kumwabudu Mungu wao. Najua wewe ungeshukuru na kusema ''AFADHALI TUMEZUIWA KUABUDU!!!!''

Saturday, January 24, 2009

Tumshukuru Mungu...

Tuna kila sababu ya kwenda mbele za Mungu kwa shukrani kila siku maana yeye anajishughulisha sana na mambo yetu.

Ninasema maneno haya maana kila siku mimi ninapita katika daraja la Nduruma ambalo karibu kila mwaka kunatokea ajali mbaya zinazochukua maisha ya waTanzania wengi.

Siku ya Jumanne tarehe 21 Jan 2009 nilipita kwenye daraja hilo asubuhi na mchana ikatokea ajali mbaya sana iliyochukua maisha ya watu zaidi ya 18. Nilipopita mahali hapo jioni baada ya ajali nilihisi machozi yakinilenngalenga na nikasema Mungu ninakushukuru kwa sababu umenipa nafasi nyingine zaidi ya kuishi.

Picha hizi nimepiga asubuhi hii wakati napita tena.


Picha kutoka ndani ya basi wakati tupo juu ya daraja.
Mbele kidogo ya daraja.
Hebu jaribu kujipa nafasi hata ya dakika moja na utafakari jinsi Mungu alivyokupitisha katika hatari mbali mbali na kukupa nafasi ya kuwa hai sio kwa sababu unastahili.
Tunawapenda!!

Friday, January 23, 2009

Je alikosea au alikua anaiba?

Alipokutwa na wapiga picha akiingiza fridge la Cocacola ktk gari la Pepsi. Hii ni kutaka ufurahi tu. Picha kwa hisani ya fun & fun only

Wednesday, January 21, 2009

Ladies and Gentlemen...the president of the USA!!


Barack akila kiapo kwa ajili ya majukumu yaliyo mbele yake!!


First Lady na Prezzoo wakipunga kwa wananchi.

Askari wa marekani akilia wakati akitazama uapishwaji wa Rais Barack H. Obama. Kijana huyu yuko Iraqi.

Kama na sisi waTanzania tungeipenda nchi yetu na kuwa wazalendo kama wamarekani, nadhani tungekuwa mbali kidogo. hili ni jambo la kujifunza kwa kweli.

Picha zote kwa hisani ya http://www.msnbc.msn.com

Tuesday, January 20, 2009

Picha zaidi za mazishi ya Fanuel Sedekia

Tumepata maombi ya wadau wengi ambao walipenda tuweke picha zaidi za matukio kutoka katika mazishi ya mtu wa Mungu Sedekia. Nami nawaletea hizi;






Baadhi ya wadau wa Muziki wa Injili wakimsindikiza kaka na rafiki yao.




Jeneza lililobeba Mwili wa ndugu yetu Sadekia.




Ni kama amelala.



Familia ya Marehemu.

Upendo Nkone alishindwa kabisa kujizuia...




Sura za majonzi na kutoamini!! Christine Shusho, Beatrice Muhone

Maua

Neno la Mungu!







Mwalimu Mwakasege pia alikuwepo!!







Mavumbini ulitoka na Mavumbini utarudi!





Mwakilishi wa Shalom Broz Arusha pia alikuwepo makaburini...macho!!

Wadau wa muziki wa Injili: Robert Ngowi, Mtumishi Tolla G na mwalimu Boniface Funyame wa Calvary temple.

Baada ya mazishi, chakula nyumbani kwa marehemu. Dada Asumpta na rafiki yake kutoka DPC.

Picha zoote ni kwa hisani ya mtumishi wa Mungu Tolla G wa Mfalme Music.

Monday, January 19, 2009

SIKIA HI TULIPOKUA TUNATOKA TANGA KTK HAFLA YA Arusi ya BWN Thomas

Mkwakwani hapa maeneo ya Tanga Kunani. katika pitapita pita zangu niliona nikuchukulie kaeneo haka
Haya tena safari ya kuja Dar ilianza na Basi hili mali ya Tashrif Coach, namba za usajili za gari hilo ni hizi T286 AAF Mara ya kwanza maeneo ya Lisanga gari ikaharibika. Kufika Wami likaharibika tena. na hapo kagiza kalikua kanaanza kwa mbaliiiiii. Unajua nini? System ya Upepo ndio ilikua inasumbua. Mara likategeshwa tegeshwa tukaondoka.


Kumaliza wami tu likaharibika tena. safari hii giza lilikua totoro, hakuna uhakika wa kuondoka pale. Gari hili ndo yale yanayoongoza kwa ajali hapa Tanzania na hasa Tanga line.




Safari iliishia hapa Chalinze kama unavyoweza kuona katika picha ya hapo chini. Hawa jamaa walikua wakiitwa YARABISALAMA. (kama kumbukumbu zangu hazijapotea), wakapata ajali mbaya za mfululizo, wakabadili na kujiita No Challange na baadae Real No Challange. wakapata maajali ya kupitiliza, na kumalizia ile ya pale Muheza ktk Mto msangazi, makabadili jina na kujiita TAASHIRIF hata leo. Sasa inawezekana kabisa wakabadilisha tena. Mbona magari mengine hayapati ajali kama hizo?




Asubuhi yake hapa ndo tukaondoka hapa.


Wednesday, January 14, 2009

Mtumikie Mungu, UTAHESHIMIKA!!

Jeneza lililobeba mwili wa Sedekia likiwa limebebwa na wanamuziki wengine wa nyimbo za injili likisogezwa jukwaani kwa ajili ya ibada ya Mazishi.


Umati katika umwanja wa Sheikh Amri Abeid Karume.

watu kila mahali!!


Mtumishi wa Mungu Fanueli Sedekia ambaye alifariki dunia wiki 2 zilizopita huko Israel na kuzikwa hapa Arusha wiki iliyopita amenifundisha kitu kikubwa sana katika kumtumikia Mungu.

Katika Neno la Mungu tunaambiwa kwamba ukimtumikia Mungu utaheshimika. hili limekuwa dhahiri katika mazishi ya huyu ndugu. Watu kutoka maeneo yote ya Arusha, mikoa mbali mbali ya Tanzania pamoja na baadhi ya nchi walihudhuria.

Sedekia alimtumikia Mungu bila ya kuchagua jina la kanisa wala ukubwa au udogo wake. alikuwa tayari kumtumikia Mungu popote alipokuwa tena kwa moyo mkunjufu kabisa. Namshukuru Mungu kwamba niliwahi kupiga muziki pamoja naye katika siku za mwisho za uhai wake hapa Arusha na haya ninayoandika nimeyahahakikisha!

Ninamwomba Mungu anipe Roho ya utumishi usiokuwa na mipaka wala ubaguzi ili nitakapoondoka niwe nimeacha alama katika maisha ya watu.

Arusi ya Thomas na Genesis iliyofanyika Muheza/Michungwani TAG Tar 10 January 2009

Thomas & Wife ktk pozi


Nakupa pete hii uwe Mume wangu


Nakupa pete hii uwe mke wangu.

Pastor Martin Pyuza wa TAG Muheza na Pastor Peter Mgema wakiwakabidhi maarusi mikononi mwa Bwana.


Matukio haya pia yalijiri hiyo tar 10. Bwn Thomas alipobeba jiko lake

Thomas and wife pamoja na Wazazi wake
Kijana inaonesha Msuli anao


wamependeza sana sana.

Wadada waliopamba Arusi ya Mr & Mrs Thomas




Style za kileo za kulishana Keki. Dont try it at Home




Tuesday, January 6, 2009

Our Prayers for you!

Tunapoanza mwaka huu wa 2009...






Tunamwomba Mungu akufungulie milango ya baraka katika maisha yako lakini pia usiendelee kutafuta mlango ambao tayari umefungwa bali angalie pembeni ili uone mlango mwingine ambao Mungu ameufungua kwa ajili yako!






Tunamwomba Mungu pia akupe maisha ya utoshelevu na ushwari siku zote ili iwe rahisi kwako kumtumikia! Tafadhali usikae bure, Mungu amekupa nguvu sio kwa ajili yako peke yako tu, tumika pia kkwa ajili ya wengine. Tafuta japo siku moja katika mwaka huu ukawatembelee watu wenye matatizo na Mungu atakubariki.


Na pia acha kujisumbua sana kwa mambo ambayo hutaweza kuyasolve. Kimsingi huyawezi maisha haya peke yako...so dont bother to accomplish unaccomplished goals. Relax, acha mawazo!!




Mwisho kumbuka...



Dont complain for thorns between roses but be grateful for roses between thorns!!

Monday, January 5, 2009