Tafuta/Search This Blog

Thursday, October 28, 2010

Arusha leo.

Wakati joto la uchaguzi linazidi kupanda hapa kwetu Tanzania, leo nimepita maeneo ya Arusha na kupata hizi picha.

Nyumba moja na wanafanya kazi moja lakini mitazamo ya kisiasa ni tofauti. Ni kama hasi na chanya. Lakini utanzania wao ni wamuhimu zaidi ya mitazamo yao.

Nimekutana na hili gari, hata sijui linaitwaje ila ni lakizamani sana lakini liko maintained vizuri sana!! Nimelipenda. kwa wanaojua jina lake hebu nisaidieni basi!!

Monday, October 25, 2010

Dr. Slaa na Elias Msuya.

Dr Slaa akisalimiana na watu akiwa anaingia katika Mdahalo uliorushwa LIVE na ITV. Hapa anaeana mkono na Bro wetu Elias Msuya.

Saturday, October 16, 2010

Wagosi na hatari zao!!

Hii nimeipenda sana kutoka kwa wagosi wa ndima wa Mombo. Inaonekana hawa ndugu zangu ili suala la hatari ili lieleweke vyema ni lazima liandikwe kinyume! Hahahahahaaa.



Hii picha imepigwa katika kituo cha mafuta kilichopo kwenye njia panda ya kwenda Lushoto pale Mombo!!
Hii ni hatai kwei kwei!!

Wednesday, October 13, 2010

Kidato cha nne wamaliza shule akiwemo Yusuph

Yusuph Kijana aliyeonekana mpole na Mtanashati alipokea cheti cha kuhitimu Elimu ya Sekondari katika shule maarufu hapa mjini Dar es Salaam inayoitwa Kambangwa.

Hatuna Shaka Umati Ulimshangilia na kushuhudia jinsi alivyopokea Cheti chake

(School Leaving Certificate)

Kwa kutambua Uchapakazi wa Yusuph na wanafunzi wa Darasa lao Mwalimu wa Darasa alipiga nao picha ya pamoja.

Baba Mzazi alimuandalia Yusuph keki nzuri ya rangi ya yenye maandishi ya Pinki kuonesha ameshinda.


Walimu waliandaa michezo hata kuwaita Makirikiri wa Bongo wanaotesa mji kwa miondoko ya KIDUKU.

He! Mara Graduation ilipokwisha! Uwiiiii!! Yusuph kaanza mambo haya.



Sasa amezidisha na Alama za Freemason kila anakokwenda.
Nichukue nafasi hii kutoa RAI, wadogo zangu Mtaani Kuzuri ila msiingie kwa Pupa.


Sunday, October 10, 2010

Hatimaye Tangi J avalisha mtu pete!!

Baada ya kumngojea kwa muda wa kutosha, hatimaye kaka Tangi J amekuwa serious na suala la kuoa na leo katika kanisa la TAG kigogo amemvalisha pete ya uchumba Happy Sasali.



Zifuatazo ni baadhi ya picha katika tukio hilo ambazo tumezipata kwa hisani kubwa ya "kaka mtu" Samuel Sasali a.k.a Papaa Sebene.





Hii ni ishara kuwa hata watoto walifurahia tendo hili la kishujaa, Kwa karibu anaonekana Mtoto Mussa akifurahia na kumsindikiza TangiJ kupita mbele.




Hoi hoi na vifijo, sauti za wimbo maarufu "Wifi wifi huyoo wifi" zilitawala


Tangi J akiwa Standby kabla ya kumvisha Happy pete na Happy pia akiwa katika pozi la kusubiria.




Shemejiiiiiiii




Ndio hivyo tena.


Ukishikwa shikamana. Happy alimtoa TangiJ kwa zawadi. Hatukujua ninini kiliwekwa.


Ndio hivyo jamani "Namilikiwa mie"



Pongezi za papo kwa hapo. Mama Nyenyema akimpongeza TangiJ.

Wamama wakimsindikiza Mama mzaa Chema kutoa Pongezi..


SBP tunampongeza sana kijana wetu na kumtakia maandalizi mema ya arusi. Tunatoa wito kwa huyu mmoja aliyebaki afanye Hima.

Saturday, October 9, 2010

UTAFITI WA REDET WAPINGWA KILA KONA

MATOKEO ya utafiti wa Redet yaliyoonyesha kuwa mgombea urais wa CCM, Jakaya Kikwete anaongoza kwenye kura za maoni, yamepingwa vikali na wasomi, wanasiasa na wananchi ambao baadhi wameeleza kuwa "yamepikwa ili kuwavuruga wapiga kura".Hata CCM ambayo mgombea wake amepata alama nyingi, imeeleza kuwa matokeo hayo hayakutoa picha halisi ya maoni ya watu kwsa Kikwete, ikidai kuwa alistahili kuongoza kwa kura nyingi zaidi za maoni.
Redet ilitangaza matokeo ya utafiti wake juzi ikieleza kuwa Kikwete alipata asilimia 71.2 ya kura za maoni katika utafiti uliofanyika mwezi Septemba na kufuatiwa na mgombea wa Chadema, Willibrod Slaa aliyepata asilimia 12.3 wakati Prof Ibrahim Lipumba, ambaye katika chaguzi mbili zilizopita alikuwa akishika nafasi ya pili, alipata asilimia 10.1.
Huku kampeni za uchaguzi zikizidi kuwa kali katika siku 22 za mwisho, matokeo hayo ya utafiti yamepingwa na wadau wa demokrasia waliohojiwa na Mwananchi wakisema utafiti huo unapaswa kulaaniwa kwa kuwa ni mkakati maalumu wa taasisi hiyo 'kuifagilia' CCM na kuijengea mazingira ya ushindi katika uchaguzi ujao, huku wasomi wakihoji vigezo vilivyotumika kupata watu waliohojiwa.

Wasomi na wanazuoni

Muhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Dk Ezavel Lwaitama alisema ripoti ya utafiti huo ina upungufu mwingi.
Alisema ripoti hiyo haijaeleza umri wa watu walioulizwa maswali na kwamba hata uchaguzi wa maeneo ambayo utafiti huo ulifanywa una walakini.
“Ukiangalia matokeo ya ju juu utapotea," alisema msomi huyo. "Kwanza inabidi ujiulize katika maeneo ambao utafiti ulifanyika kuna watu wangapi, uangalie jinsia, umri wa watu waliolizwa na pia hata swali lilikuwa linasemaje.
“Wangetuambia kama wamehoji watu wa miaka 40, 60 na kuendelea, hakuna mtu angeshitushwa na ripoti hii, lakini pia swali lilisema utamchagua mgombea wa chama gani, wangeuliza ni kiongozi wa aina gani utamchagua, tungekuwa tunazungumza mengine hapa.”
Lakini akaonya kuwa CCM inatakiwa ijifunze jambo kutokana na maeneo ambayo ripoti hiyo imebainisha kuwa chama hicho kimefanya vibaya na upinzani ukawa na nguvu.
“Kwa mfano angalia Dar es salaam, CCM inaongoza Temeke CCM, lakini Kinondoni ambako tunaamini kuwa kuna wasomi na watu walioerevuka Chadema ndio imeongoza. Kwa hiyo wakati mwingine mtafiti anaweza kukupa somo bila wewe kujua,” alieleza.
Naye Mhadhiri wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Tumaini, Dk Failres Ilomo aliuponda utafiti huo akieleza kuwa hana sababu ya kuuamini kwa kuwa taasisi yenyewe inawajibika serikalini.
“Sisi (Chuo cha Tumaini) tuliomba kufanya utafiti huo, lakini walitukatalia na badala yake kazi hiyo ikipewa taasisi ya Redet ambayo ni taasisi ya umma ambayo kimsingi imefanya kazi ya mkuu wao,” alisema Dk Ilomo.
"Hao waliofanya walichaguliwa kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ambacho kiko chini ya serikali, lakini hata kama chuo cha serikali kimepata kazi hiyo, kilitakiwa kiwashirikishe wadau wengine ambao hawako chini ya serikali.”

Msomi mwingine ambaye ni mwanafunzi wa Udaktari wa Falsafa (PHd) katika Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA), Gasper Mpehongwa alidai utafiti huo si sahihi kwa sababu Dk Bana ni mshauri wa masuala ya siasa wa Rais Kikwete.
“Ni mtu ambaye yuko jirani sana na Kikwete, hivyo hawezi kutoa matokeo ambayo ni tofauti na Kikwete,” alidai Mpehongwa.
Mhadhiri mwingine wa Tumaini, Ordination Mgongolwa alisema: “Mimi nilipopata ripoti hiyo jana nilifedheheka sana kwa sababu kwanza Redet ni taasisi ambayo haiko huru; lakini pia ripoti yake ina msukumo wa CCM.
"CCM inawasukuma watu katika kampeni zake kwa kutumia vitu wakati watu wanaojaa katika vyama pinzani wanavutiwa na sera, hivyo CCM imefanya mbinu ya kuwakatisha tamaa wapiga kura. It is something cooked(ni kitu kilichopikwa) kwa sababu wanalipwa na serikali."

Vyama vya siasa
Katika hali isiyotarajiwa, utafiti huo pia umekosolewa na CCM ambayo imesema kuwa inaamini kuwa matokeo yake si sahihi kwa asilimia zote.
Meneja wa kampeni wa CCM, Abdulrahman Kinana alisema jana alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari ofisi ndogo ya makao makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam kuwa utafiti huo una kasoro.
Hata hivyo, Kinana alikubaliana na utafiti huo katika kipengele kinachomwonyesha mgombea wa0 anaongoza, lakini akaeleza kuwa utafiti huo umeshindwa kueleza ukweli kwamba Kikwete atashinda zaidi ya asilimia 71.2.

“Hii ni tathmini ‘fair’ (nzuri), lakini si 100% correct (si sahihi kwa asilimia mia)," alisema Kinana.
Tutapata ushindi zaidi ya matokeo ya Redet. Kuna baadhi ya maeneo mimi sikubaliani nao. ‘I completely disagree’. Nyinyi mnaoripoti kila siku msubiri mtaona matokeo tutapata zaidi ya asilimia 90.”
Alitoa mfano wa maeneo ambayo alisema wazi kuwa hakubaliani na matokeo ya utafiti wa Redet ambayo aliyataja kuwa ni Kigoma Vijijini na Mvomero mkoani Morogoro ambako utafiti huo umeonyesha kuwa CCM imepata asilimia ndogo ya kura, lakini Kinana akasema chama hicho kitashinda kwa zaidi ya asilimia 90 katika maeneo hayo.

Alisema utafiti wa Redet ulifanywa kwa kuzingatia wilaya na si majimbo na kwamba upo uwezekano kwa waliohojiwa kutoka katika jimbo moja lenye mtazamo mmoja wa kisiasa na siyo majimbo yote katika wilaya.
Kuhusu kushuka kwa asilimia za ushindi wa mgombea wa CCM kulinganisha na utafiti wa taasisi hiyo wa mwezi Machi mwaka huu, Kinana alisema: “Nijibu hili la ‘kudrop, hii ni tathmini ‘fair’, lakini si ‘correct’ asilimia mia moja.”
Kwa kujiamini Kinana alisema mgombea wao wa urais atapata zaidi ya asilimia 80 ya kura na wabunge zaidi ya asilimia 76 na kuwaita wapinzani wasindikizaji, akieleza kuwa wagombea wake urais kwa ujumla wataambulia moja ya tatu ya kura za nafasi hiyo.

“Uchaguzi ni hesabu, ushindi ni hesabu, sisi tunajali hesabu... hii inatupa mwanga kuwa tutashinda," alijigamba.
Nayo CUF imesema haikubaliani na matokeo hayo ya Redet kwa kuwa inaamini kuwa ni mpango uliotumwa na CCM kufanya utafiti huo tena kwa maslahi binafsi.
Naibu katibu mkuu wa CUF- Bara, Joran Bashange alisema Redet inatumiwa na chama tawala tangu zamani hivyo kinachofanyika ni udanganyifu kwa wananchi.
“Huu mpango unatumiwa dhahiri na chama tawala kumfanyia mgombea wao kampeni ndio maana unaona wanampatia kura nyingi, lakini ikitokea kampuni nyingine inamuangusha," alisema.
Bashange alieleza baadhi ya mambo yanayofanya utafiti huo uonekana kuwa wa kupangwa ni pamoja na kutotoa mchanganuo wa idadi ya watu walioshiriki kutoa maoni zaidi ya kutaja asilimia zao tu.

"Maswali yanayoulizwa ni elekezi na hivyo majibu yake yalilingana na swali lilivyoulizwa," alisema.
Naye mgombea urais kwa tiketi ya APPT-Maendeleo, Peter Mziray aliuponda utafiti huo akisema haukufanywa kisayansi na umelenga kuibeba CCM.
“Kitaaluma, mimi ni mwanasayansi na utafiti uliofanywa na Redet naona kabisa haukufanywa kisayansi. Haiwezekani kura za Lipumba na Slaa zioane,” alisema.
“Mara kwa mara Redet wanapofanya utafiti wamekuwa wakiitaja CCM kuwa namba moja na sisi tunajua kwamba wanaibeba CCM,” alisema.
Alisema yeye amepita mikoa mingi kujinadi na kwamba anaelewa mwamko walionao wananchi kuhusu CCM na vyama vingine hivyo matokeo hayo kwa upande mwingine yanaweza kuwachanganya wananchi.
Alisema hata matokeo yanayoonyesha chama chake kupewa nafasi ndogo ya kushinda ni ya uongo kwa sababu yeye ametembea mikoa mingi na baadhi ya maeneo wananchi wana mwamko na chama chake.
Mwenyekiti huyo pia alitahadharisha kuwa kama taasisi hiyo itaendelea kuipendelea CCM, hawatavumilia watachukua hatua za kisheria.

“Sasa hivi niko busy mikoani kwenye kampeni lakini nina haki kabisa ya kuwashtaki, na kama wataendelea hivyo hatutavumilia,” alisema Mziray.
Mwenyekiti NCCR-Mageuzi, James Mbatia jana alishindwa kuzungumzia matokeo ya utafiti huo kwa madai kuwa hajausoma, zaidi ya kuona habari katika magazeti.
Mbatia, ambaye anawania ubunge jimbo la Kawe, alisema: “Siwezi kusema lolote... ningeweza kuzungumza kama ningekuwa nimeupitia na kujua nini kilichomo. Nikiupitia ninaweza kusema lolote kwa kuwa nitakuwa nimeulinganisha na tafiti nyingine zilizowahi kutolewa na Redet,” alisema Mbatia.
Kaimu katibu mkuu wa Chadema, John Mnyika hakuwa tayari kuzungumza jambo lolote juu ya utafiti wa Redet kwa maelezo kuwa chama kitatoa tamko lake leo.

Hata hivyo, meneja wa kampeni wa Chadema, Profesa Mwesiga Baregu alisema taarifa hiyo ina udhaifu kadhaa.
“Bado naisoma ili tutoe taarifa kesho (leo), lakini jambo la msingi la kuangalia pale ni 'je nani kaulizwa maswali, utafiti umefanyika maeneo gani, swali lilikuwa linasemaje,” alisema Profesa Baregu.
“Inaelekea watafiti walipelekwa kwa wajumbe wa nyumba kumi wa CCM”.
Habari kutoka Tanga zinasema mgombea ubunge wa Jimbo la Korogwe Mjini kwa tiketi ya Chadema, Kalistus Shekibaha ameichachamalia taarifa ya utafiti huo akidai kuwa imepikwa ili kuwavuruga wapigakura.
Alisema utafiti huo haukubaliki na kuzitaka taasisi zinazoendesha tafiti kuwaachia wananchi waamue wenyewe viongozi wanaowafaa na si kuendesha kura za maoni ambazo zina lengo la kuwakatisha tamaa wagombea.

“Unapotoa taarifa za kitafiti, unatakiwa kutoa uchambuzi ambao utasababisha uheshimiwe na wananchi... lakini unapoonekana kubabaisha unasababisha wananchi kukosa imani na wewe,” alisema Shekibaha.
Mgombea huyo alisema, hata hivyo, kuwa kutokana na kuzifahamu njama hizo, wagombea kutoka vyama vya upinzani hawawezi kukata tamaa badala yake wataendelea kupiga kampeni ili kuwaachia wananchi kujua nani wa kuwafaa.
Wakati mgombea huo akieleza hayo, mwananchi mmoja jijini Dar es Salaam aliyejitambulisha kwa jina la Kilimba Fulgence alipiga simu Mwananchi na kusema kuwa kuna kila dalili kwamba utafiti huo umefanywa katika maeneo ambayo CCM ina mashabiki wengi.
Matokeo hayo ya Redet yamekuja katika kipindi ambacho kuna mzozo mkubwa baina ya taasisi nyingine inayofanya utafiti wa masuala ya kijamii, kisiasa na kiuchumi ya Synovate na Chadema ambayo inadai kuwa mgombea wake wa urais, Dk Willibrod Slaa aliongoza kwenye kura ya maoni iliyofanywa na taasisi hiyo.

Synovate imekana kufanya utafiti wa aina hiyo na kwamba hadi sasa imefanya utafiti kuhusu mwenendo wa vyombo vya habari katika kuripoti habari za uchaguzi mkuu, lakini Chadema imesema inao ushahidi kuwa taasisi hiyo iliendesha utafiti ulioonyesha kuwa Dk Slaa alipata asilimia 45 dhidi ya 40 za Kikwete.
Katika matokeo ya utafiti wa Redet, CCM inaonekana itapoteza wabunge wengi baada ya matokeo kuonyesha kuwa chama hicho tawala kitapata asilimia 66.7 za kura, ikiwa ni kuanguka kwa asilimia 4.5.

Kwa mujibu wa Redet, matokeo yangekuwa hivyo iwapo uchaguzi mkuu ungefanyika kati ya Septemba 20 hadi 28 mwaka huu.
Akitoa matokeo ya utafiti huo wa 17 uliofanyika katika mikoa yote 26 ya Tanzania Bara na Visiwani katika kipindi hicho cha Septemba, Dk Bana alisema jana kuwa waliohojiwa walitakiwa kutoa maoni kuhusu uchaguzi mkuu wa rais, wabunge na madiwani.
Alisema katika utafiti huo wahojiwa waliulizwa: "Mwezi Oktoba mwaka huu utafanyika uchaguzi mkuu.
Kama uchaguzi huo ungefanyika leo, je wewe ungemchagua mgombea wa chama gani?"
Alifafanua kuwa kutokana na swali hilo vyama vitatu vya CCM, CUF, Chadema vilipata alama nyingi kwa wagombea wake wa urais, wabunge na madiwani.
Hata hivyo, Dk Bana alisema kiwango cha asilimia za kura kimepungua kwa mgombea wa CCM kulinganisha na utafiti uliofanywa na Redet mwezi Machi wakati matokeo yalipoonyesha kuwa asilimia 77.2 wangemchagua mgombea urais wa CCM na tofauti na asilimia 71.2 alizopata safari hii.
"Itakumbukwa kwamba matokeo ya utafiti wa Redet wa hapo Machi mwaka 2010 yalionyesha wengi wangemchagua mgombea urais wa CCM asilimia 77.2. Katika utafiti CCM bado inaongoza, hata hivyo kiwango cha asilimia kimepungua," alisema Dk Bana.
Dk Bana alisema utafiti huo wa Redet ulifanywa kwa kuwahoji watu 2,600 katika wilaya 52 na kwamba watu 1,849 ndio waliosema watamchagua mgombea wa CCM, 263 wa CUF na 319 mgombea wa Chadema.
Ikilinganisha na utafiti wake wa mwezi Machi mwaka huu, Redet ilisema kuwa katika kipindi cha miezi sita kilichopita, idadi ya watu ambao wangemchagua mgombea wa Chadema imeongezeka kwa asilimia nane (8) kutoka 4.2 za mwezi Machi hadi 12.3.
Redet ilitaja pia kuongezeka kwa asilimia 0.9 kwa kura za urais wa CUF, asilimia 02 kwa TLP na 0.1 kwa NCCR-Mageuzi huku ikitaja sababu kuwa ni kampeni za uchaguzi zinazoendelea.
Lakini, taasisi hiyo ilisema mgombea urais wa CCM anaongoza kwa kutajwa jina lake kama mtu ambaye wangependa awe rais wa Tanzania na asilimia 68.5 ya wahojiwa wote akifuatiwa na Dk Slaa wa Chadema aliye na asilimia 11.9 huku Profesa Lipumba wa CUF akiwa wa tatu kwa asilimia 9.3 ya wahojiwa.

Taasisi hiyo ya utafiti wa kitaalam ilisema kuwa katika kura za urais, CCM itapata kura kidogo zaidi katika Jimbo la Kigoma Vijijini ambako atapata asilimia 28 huku Jimbo la Nkasi akipata asilimia zote 100.
Kwa mujibu wa utafiti huo, kwa upande wa wabunge wa Jamhuri ya Muungano, pia asilimia ya watakaochagua mgombea wa CCM imepungua kwa asilimia 1.3, huku ikiongezeka kwa vyama vya upinzani, vikiongozwa na Chadema ambayo imeongezeka kwa asilimia 2.9, CUF 1.5, TLP na NCCR-Mageuzi asilimia 0.8 kila kimoja.

Habari hii imeandaliwa na Fidelis Butahe, Burhani Yakub, Tanga, Hussein Issa, Jackline Laizer, Nora Damian, Petro Tumaini, Fredy Azzah, Exuper Kachenje na Emmy Kihongole

-Mwananchi.

Saturday, October 2, 2010

Mbona hivi jamani??

Jamani hii picha nimeikuta kwa blogger SUMO ambaye yeye ameandika hivi; "Kifaa cha kisasa kikionyeshwa tayari kukabili watanganyika kipindi cha uchaguzi, tumejitahidi sana kuwekeza huko kama South miaka ya 70! Hilo mbele sijui lakuondolea Ice barabarani ama kukusanya waandamanaji?"



Mimi kama mTanzania nahisi hivi ni kama vitisho na havifai maana ni kama kutuonyesha kwamba serikali imejiandaa kwa fujo. Kwani kuna fujo yeyote iliyotangazwa??



Jana mnadhimu wa jeshi alipiga "biti" kuhusu fujo ambazo mimi sijaona umuhimu wa kutengeza hiyo tension kwa waTanzania. Nadhani kuna kamchezo kachafu kanataka kuchezwa...Mungu atulinde!!

Mungu ibariki Tanzania...naamini sitachukiwa kwa kusema ukweli!!