Tafuta/Search This Blog

Saturday, February 19, 2011

GONGO LA MMBOTO: Kombora lamkosa kichanga kitandani



Na Florence Majani



NIPO katika basi la abiria nikielekea Gongo la Mboto ambako maafa yametokea baada ya makombora katika ghala la kambi ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kulipuka.Ninapofika nawakuta wakazi wa hapa wengi wakiwa bado wana wasiwasi, wengine wengi wakiwa wanachechemea na baadhi wakiwa wanaokoteza mabaki ya mali zao baada ya nyumba zo kuungua au kubomolewa na makombora yaliyolipuka usiku wa kuamkia juzi.

Nazungumza nao na kwa nyakati tofauti wakazi hawa wanatoa usemi ambao unawiana, kuwa wameona miujiza.

Wanasema, pamoja na makombora hayo kuacha misiba katika nyumba na familia kadhaa, kusababisha uharibifu mkubwa wa makazi na hata baadhi ya ndugu hasa watoto wadogo kupotezana, lakini wao walikuwa wakikoswa koswa kwa karibu kabisa na makombora hayo na wengine wanakiri kwamba kifo kiliwakosa sentimita chache au ilikuwa chupuchupu.

Kichanga kilichokoswa na bomu kitandani
Wengi husema kuwa watoto ni malaika wa Mungu. Naam ipo miujiza kadha wa kadha ambayo wakazi wa Gongo la Mboto hawataisahau, achilia mbali madhara yaliyotokana na milipuko ya mabomu. Miongoni mwa miujiza ambayo Mungu ameionyesha katika maafa hayo, ni kupona kwa kichanga cha miezi sita.

Makobora matatu yanayokadiriwa kuwa na urefu wa mita tatu na nusu kila moja, yalitua ndani ya chumba kilimokuwa kimelezwa kichanga hicho na moja ya makombora hayo kujikita katika kitanda ambacho alilala kchanga huyo, malaika wa Mungu. Chumba na hata kitanda viliwaka moto kutokana na kulipuka kwa makombora hayo, lakini hii leo kichanga hikipacha, kinachojulikana kwa jina la Kulwa mbali na kupata majeraha madogo madogo kiko hai.

Nazungumza na mama mkubwa wa kichanga hicho, Adia Roki mkazi wa Gongo la Mboto, Mzambarauni, ambaye anasema, siku ya tukio wakiwa hawana hili wala lile, mdogo wake, Rose Roki, mwenye watoto pacha alikuwa nje na Doto wakati Kulwa alikuwa amelala ndani.

“Mdogo wangu ana watoto mapacha, Kulwa na Doto, Doto alikuwa nje amepakatwa na mama yake wakati Kulwa alikuwa ndani amelala, ghafla mlio mkubwa ulisikika lakini watu waliudharau na kudhani kuwa itakuwa radi, lakini ngurumo zilivyozidi ilibidi watu waanze kuchukua hadhari ili kujinusuru,” anasema Adia.

Anasema, baada ya kusikia ngurumo zinakithiri na nyingine zikisikika ndani kabisa ya chumba alimolala mtoto Nasri Kasim(Kulwa) mwenye umri wa miezi sita, mama wa mtoto huyo alinyanyuka na kukimbilia chumbani ambapo alikuta kombora likiwa limejikita katikati ya kitanda ambacho Nasri alilala.

“Alichofanya ni kumchukua mtoto na kutoka nje lakini kabla hajamalizikia kutoka, kombora jingine lilijikita ardhini karibu kabisa na mlango wa chumba hicho na kuzama kabisa sakafuni na kubaki kichwa pekee,” anasema Adia.

Anasema, licha ya majeraha kidogo ya kuungua aliyoyapata, jambo ambalo wanamshangaa Mungu, ni kitendo cha kombora lenye ukubwa ule kukita pembeni na kumuacha mtoto Nasri akiwa salama.

Baba mwenye nyumba wa Rose, Adam Kasaba, anasema, hakuna aliye tegemea usalama wa Nasri kwani kishindo kilichosikika ndani ya chumba kile kilikuwa cha kutisha lakini kwa muujiza wa Mungu, kombora lilimkwepa na kutoboa kitanda likimuacha yeye hai.

Bibi Kizee naye anusurika
Mama Samjela mwenye umri wa miaka 78, mkazi wa Pugu Kajiungeni, shuleni, anasema, ilikuwa saa mbili usiku wakisikiliza taarifa ya habari akiwa na mtoto wake ambaye ni Diwani wa kata ya Pugu, Imelda Samjela, ghafla wakasikia ngurumo za radi, wakazipuuzia lakini walipoona hali hiyo inazidi wakaamua kuzima luninga na kuanza kujisalimisha.

“Tulipoona ngurumo zinazidi mimi na wajukuu na wanangu tuliamua kukimbia lakini mimi presha ikanipanda nikapelekwa hospitali ya Kisarawe, pale tukakuta watu wamejaa na hakukuwa na huduma ndipo nilipopelekwa Tumbi,” anasema mama Samjela.

Anasema, kombora lilitoboa paa la chumba anacholala yeye na kubomoa ukuta hivyo kama siyo Mungu yeye naye angekuwa anaitwa marehemu hivi sasa. Anasema anawaza ingekuwaje kama wakati huo angekuwa amelala katika chumba hicho?

“Baada ya kukimbizana hospitali, huku nyuma kombora lilikuja na kutoboa ukuta wa chumba changu, kwa hiyo kama siyo Mungu, hata mimi ningekuwa nimekufa tayari,” anasema.

Muuguzi anusurika, nyumba yake yateketea kwa moto
Muuguzi wa hospitali ya Buyuni iliyopo Gongo la Mboto, Maserlina Maeda, anasema,licha kuunguliwa nyumba yake, lakini anamshukuru Mungu kwa kunusurika na kifo kwani kombora lilienda kutoboa ukuta wa chumba anacholala na kujichimbia kitandani tena palepale anapoweka kichwa wakati wa kulala.

“Usiku huo mimi na mwanangu tukiwa tumetulia hatuna hili wala lile, tulisikia vishindo tukadhani ni majambazi lakini hali hiyo ilipozidi, mwanangu alipata woga akaanza kukimbia, mimi nikarudi ndani kuchukua fedha lakini nikakuta mlango umefungwa na mimi nikaamua kujisalimisha,” anasema Maeda.

Anasema, yeye na mtoto wake walipotezana na baadaye wasamaria wema walimfuata na kumpa taarifa kuwa nyumba yake inateketea kwa moto.

“Niliposikia hivyo nilichanganyikiwa, nilidhani mwanangu atakuwa naye ameungua na kufariki lakini majirani walinitia moyo kuwa mtoto yu mzima isipokuwa nyumba na mali zilizopo ndani yake vimeungua,” anafafanua muuguzi huyo ambaye sasa anaishi maisha ya kusaidiwa kila kitu kuanzia malazi mpaka mavazi.

Maeda anasema, bomu lile liliangukia katika kitanda chake na kulipuka tofauti na mengine ambayo yalikuwa yanatoboa nyumba bila kulipuka, jambo lililosababisha mali zake zote kuteketea kabisa.

Makombora yavuka nyumba za watu na kuchimbua makaburi

Katika hali isiyo ya kawaida, wakazi wa Gongo la Mboto, Mzambarauni, wanasema , baadhi ya makombora yalikuwa yanavuka nyumba zao na kutua katika makaburi hatua chache yalipo makazi yao.

Mkazi wa eneo hilo, Jamila Mwainunu anasema, anashangazwa na hali ile kwani, nyumba yake haijaguswa hata kidogo na kombora wala haikupata ufa, sio kwamba makombora hayo hayakuwa yakifyatuka upande wake bali yalivuka na kutua katika makaburi yaliyo jirani na nyumba yake.

“Mungu kweli ni wa ajabu, kwangu huu ni muujiza kwani, bomu lile pale (ananyoosheaa kidole juu ya kaburi ambapo bomu limejikita) limevuka nyumba yangu na kwenda kuchimbua kaburi,” anasema Jamila.

Anasema, pamoja na kusikitishwa na maafa ambayo yamewakuta ndugu jama na marafiki zake lakini anamshukuru Mungu kwani makombora makubwa yalikuwa yakivuka nyumba yake na kuangukia katika makaburi jirani kabisa na nyumba yake.

Upendo na kusaidiana
Upendo ulionekana wazi, kwani licha ya purukushani zilizokuwepo wakati wa mlipuko wa mabomu, Watanzania walisaidiana kwani baadhi walichukua jukumu la kuwaokoa watoto wadogo walioonekana kupotezana na wazazi wao.

Nazungumza na Baraka Tumsifu, mkazi wa Gongo la Mboto, Mzambarauni, ambaye anasema, katika kukimbiza roho yake hapo juzi alijikuta akiwaonea huruma watoto wadogo sita ambao walikuwa wamepoteza wazazi wao.

“Imenilazimu kuwaokoa kwani roho yangu haikuiruhusu kuwaacha wapate shida katika kipindi kile, wengine ni wadogo wana miaka mitatu na wanalilia maziwa lakini sina budi kuwalea hadi wazazi wao watakapopatikana,” anasema Tumsifu.

Kwa ujumla, wakazi hao walisema, pamoja na maafa hayo waliyoyapata lakini wanamshukuru Mungu kwa kuwanusuru na makombora hayo hatari ambayo yaliwakatakata baadhi ya watu na kuwatenganisha viungo vya miili yao.

-Mwananchi.
Pichani chini ni ndege ya KLM ikiwa imetulia kwenye uwanja wa kimataifa wa Kilimanjaro baada ya kuahirisha safari yake ya Amsterdam kupitia Dar Es salaam kutokana na milipuko iliyotokea Dar es salaam siku ya Jumatano.

Shalom Broz mpya!!

Wapendwa wadau wetu tunapenda kuwafahamisha kwamba tumefanikiwa kumpata mwandishi wa makala maarufu sana hapa nchini. Huyu si mwingine bali ni kaka Elias Msuya. Kuanzia mwanzoni mwa mwezi huu wa pili tumekubaliana kufanya kazi pamoja na hivyo makala zake motomoto za siasa na mambo mengine yanayohusiana na ishu za nchi yetu zitakuwa zikichapishwa katika blog hii.

Endelea kuenjoy kututembela na usiache kutoa maoni yako!!

Barikiwa sana!!

-SBP.

Friday, February 18, 2011

BAADA YA MABOMU GONGO LA MBOTO

Huu ndiyo uafiri baada ya milipuko ya mabomu katika kambi ya jeshi Gongo la Mboto jijini Dar es Salaam.

Monday, February 14, 2011

Kwanini CCM ilazimishe muungano wa wapinzani Bungeni?

Elias Msuya

MCHAKA mchaka umeendelea katika medani ya siasa wiki hii ambapo Bunge lilizizima pale wabunge wa Chadema walipotoka tena nje ya ukumbi wa Bunge kupinga azimio la kubadilisha kanuni za Bunge ili kuvishirikisha vyama vyote vya upinzani kuingia katika kambi rasmi ya upinzani.
Kikubwa kilichokuwa kikipiganiwa ni neno “kambi rasmi ya upinzani Bungeni” na ajabu ni kwamba wabunge wa CCM wakiongozwa na Spika Anna Makinda walikuwa mstari wa mbele kutaka wapinzani wote washirikishwe kwenye kambi hiyo.
Mabadiliko hayo yalitokana na barua iliyoandikwa na Mbunge wa Wawi Hamad Rashid (CUF) na Mbunge wa Kigoma kusini David Kafulila (NCCR Mageuzi) kwa Spika wa Bunge wakitaka kanuni zibadilishwe ili kambi rasmi ya upinzani Bungeni ivishirikishwe vyama hivyo badala ya kuiachia Chadema pekee kushikilia kambi hiyo.
Hamad Rashid ndiye aliyeshiriki kuingizwa kwa neno ‘kambi rasmi kwenye kanuni za Bunge kwenye mkutano wa tisa alipokuwa kiongozi wa kambi ya upinzani, leo baada ya kukosa uongozi wa kambi hiyo, amegeuka anataka kanuni hiyo ibadilishwe.
Kwa mujibu wa kanuni hizo, chama cha upinzani chenye asilimia 12.5 ya wabunge ndiyo chenye sifa ya kuunda kambo rasmi ya upinzani Bungeni. Chadema ndiyo chama pekee chee sifa hiyo ndiyo maana kiliunda kambi hiyo.
Hadi sasa Chadema kina wabunge wa kuchaguzliwa 25 na wa viti maalum 23. Hali hiyo imeonyesha kuitikisa CCM si majimboni tu bali hata Bungeni ambako kimebaini huenda maamuzi yake mengi yakapingwa hasa kama Chadema itashikilia kamati muhimu kama vile kamati ya Hesabu za mashirika ya umma, Kamati ya hesabu za serikali za mitaa na kamati ya Hesabu za serikali kuu.
Ndiyo maana mkakati ukasukwa na CCM ukivihusisha vyama ambavyo viliachwa na Chadema yaani CUF na NCCR Mageuzi ili kisipate nguvu zaidi.

Kwa muda mrefu, uhusiano kati ya Chadema, CUF, TLP na NCCR Mageuzi siyo wa kuridhisha. Vyama hivyo vimekuwa vikihitilafiana mara kwa mara hata kushindwa kuungana licha ya juhudi mbalimbali zilizofanyika ili kuunganisha nguvu ya vyama vya upinzani.
Mambo yalizidi kuwa mabaya zaidi kwa kadiri uchaguzi mkuu wa mwaka jana ulipokaribia, ambapo mpasuko kati ya vyama hivyo ulivyopendelea kupanuka.
Vyama hivyo vilifikia hata kushindania sehemu ambazo kama vingeungana vingekishinda CCM, lakini bado vikaendelea kuvutana.
Hata baada ya uchaguzi mkuu, kumekuwa na makovu mengi kati ya vyama hivyo. kwamfano NCCR Mageuzi kimekishitaki Chadema mahakamani kwa madai ya kuchezewa rafu katika uchaguzi wa ubunge katika jimbo la Kawe ambalo limechukuliwa Halima Mdee kwa kumbwaga mwenyekiti wa NCCR Mageuzi James Mbatia.
Chama hicho pia kimekuwa kikitoa maneno ya kejeli kwa Chadema na kuona afadhali kushirikiana na CCM kuliko Chadema.
Kama hiyo haitoshi, Mbunge wa Kigoma Kusini David Kafulila ni majeruhi wa siasa ndani ya Chadema, kwani alifukuzwa kazi baada ya kutokea kutokuelewana na uongozi wa chama hicho. kwa vyovyote vile hana uhusiano mzuri na Chadema.
Kwa upande mwingine maridhiano yaliyofikiwa Zanzibar kati ya CCM na CUF yamezidi kuichanganya kambi ya upinzani. CUF imejiweka njia panda kwani huko Zanzibar siyo chama cha upinzani tena kwakuwa kimeunda serikali ile ile ya CCM. Lakini kikija bara kinapingana na serikali. Hapo ndipo Chadema kinapata utata wa kukishirikisha kwenye kambi ya upinzani.
Hali zote hizi hazitoi fursa nzuri kuwa na kambi ya pamoja ya upinzani Bungeni. Lakini kwakuwa kina Hamad Rashid na Kafulila wamedai kushirikishwa kwenye kambi hiyo, CCM nayo ndiyo imepata pa kushikia na hapo ndipo kinatafuta kukibomoa Chadema kinachoonekana kuwa na nguvu.
Hoja ya kuwa na kambi ya pamoja ya upinzani ilishadidiwa na wabunge wa CCM wakitaka kubadilishwa kwa kanuni za Bunge ili kambi ya upizani ishirikishe vyama vyote na siyo Chadema pekee. Walitumia kila aina ya msamiati kubariki mabadiliko hayo, hali iliyokataliwa katakata na Chadema na hivyo wabunge wake kuamua kutoka nje ya ukumbi wa Bunge kama ishara ya kutokukubali.


Ni kweli vyama vya upinzani vinapaswa kushirikiana, lakini Napata wasi wasi na na ushawishi huu wa CCM. Tangu lini CCM ikaunga mkono muungano wa vyama vya upinzani?
Ni CCM hiyo hiyo iliyopinga mabadiliko ya Katiba yanayoviwezesha vyama vya upianzani kuungana bila kupoteza hadhi zake. Kwa maana hiyo ili vyama hivyo viungane ni lazima vife ili kiwe chama kimoja jambo ambalo wapinzani hawalitaki.
Huo ndiyo umekuwa mkakati mkubwa wa CCM kuhakikisha kuwa vyama hivyo haviungani ili visije vikashika dola. Ndiyo maana imekuwa vigumu kwa vyama vya upianzani kuungana miaka 19 tangu mfumo wa vyama vingi urudishwe.
Baada ya kuona hivyo kila chama kimekuwa kikicheza kivyake ili kujijenga. Ndipo katika uchaguzi wa mwaka jana Chadema kimejitahidi kupata wabunge wengi na kufikia kiwango cha asilimia 12.5 ya kuweka kuunda kambi rasmi bungeni.
CCM ile ile isiyotaka muungano wa wapinzani inakuja na kuutaka muungano huo Bungeni. Huu ni unafiki, CCM kinalia machozi ya mamba, hakina jema lolote na umoja wa wapinzani. Lengo ni kuua upinzani.
Hivi leo kama Mbowe atakuwa kiongozi wa kambi ya upinzani inayovishirikisha CUF yenye ushirikiano na CCM Zanzibar, huku NCCR Mageuzi iliyoishitaki Chadema, TLP ambayo pia haina uhusiano mzuri na Chadema, hiyo itakuwa kambi gani ya upinzani? Hapo ndipo malumbano yatazuka kwa wapinzani, huku CCM wakishangilia.
Lengo la wabunge wa CCM ni kuhakikisha kuwa Chadema chenye wabunge wengi kinakosa utawala wa kamati nyeti za Bunge na hivyo kuwakosesha nguvu ya kuhoji Bungeni.
Kwakuwa vyama vya upinzani mbali na Chadema vimepewa nguvu na CCM katika kuingizwa na kwenye kambi ya upinzani, vitashindwa kufurukuta hata kwenye maamuzi.

Lengo la baadhi ya viongozi wa CCM ni kuzima hata upinzani ndani ya CCM yenyewe kwa kushika kamati nyeti. Wanataka walidhibiti Bunge ili zile kelele za ufisadi safari hii zipungue, wajisafishie njia ya uchaguzi wa mwaka 2015. Rejea mchakato wa kuwapata wenyeviti wa kamati 16 za Bunge.

Matokeo yake Bunge litarudi kuwa la chama tawala, bunge linalotetea maslahi ya wachache wanaotuhumiwa kwa ufisadi huku chama kikiwalinda.

Wednesday, February 2, 2011

Joseph Msami Atangaza nia. Aweka hadharani Mchumba wake.

Joseph wa Msami Akiuza sera mbele ya umati katika kanisa la Tanzania Fellowship of Churches Sinza Christian Centre Jumapili iliyopita tar30 Jan 2011
Anasema "Alikua kama dada yangu mwanzoni, nilipomwambia sikuamini kama angekubali, Lakini kama Muujiza demu akakubali"
(Nyosha kidoleeeee Adela! sinania mbaya kukurudisha .........)
Pokea pete hii iwe alama ya Kukuonesha wewe Adela ni mchumba wangu halali.


Vituko vilitawala. Chadema haikuachwa nyuma na Mtaalamu huyu.

Kama utani, Ila dogo alidiriki kuficha soda ili atleast anywe soda angalau 9 kama ilivyo kawaida yake. Aliogopa watu wanaweza kupewa kwani zilikwisha mapema.

Hapa Joseph akipokea mkono wa PONGEZI kwa mkono wa kulia wakati wa kushoto ukiwa umeficha soda 2 aina ya Kokakola.

Mchumba wa Msami Joseph akiwa deep katika Maombi, Kulia Joseph msami akifurahia Tendo hili la kukabidhiwa kwa Bwana. unaweza kushangaa wakati Askofu akiwaweka wakfu watu hawa alikua na FULL UPAKO lakini dogo anafurahia. Kizuri zaidi angalia picha ya chini

Joseph akimcheki Mchuchu wake kwa jicho la Upanga. Sijui haamini kuwa ni wake au vipi! Maombi yanaendelea na Shalom Broz wanaendelea na kazi, Kamera yetu ilimnasa Msami hajafumba Macho na anampiga CHABO mchuma wake. Hahahahahahahahahahah!