Tafuta/Search This Blog

Monday, October 28, 2013

KONGAMANO KUBWA LA UAMSHO NA MAOMBEZI



Kanisa la T.A.G Kigogo Mburahati Limekuandalia Kongamano kubwa la UAMSHO NA MAOMBEZI.

Tarehe: 28 Oct. hadi 3 Nov 2013

Muda: Saa 10:00 – 12:00 Jioni

Wahudumu: Askofu Laurence Kameta, Mch. Sir Gilbert, Mwinjilisti Crispin Madembwe pamoja na
Mch. Sabinus Mbogo.

Kwaya zitakazo hudumu ni Kinondoni Revival, Peace Maker Ilala na Wenyeji T.A.G Kigogo kwaya waimbaji binafsi watakao hudumu ni Lyanga George na Sara Shira.

Wenye shida mbalimbali kama Matatizo ya ndoa, Magonjwa, waliofungwa na Mapepo na matatizo mengine yote YESU MTENDA MIUJIZA ATAYASHUGHULIKIA! NJOO UKUTANE NA MUNGU!

Kanisa liko karibu na Kituo cha Mburahati msikitini mita chache sana kuelekea barabara ya barafu.

Kwa mawasiliano 0754 995 590 au 0712 554 528

Hatimaye Papaa Samuel Sasali a.k.a the Blogger ameoa!

Jana, tarehe 26 Oktobe ilikuwa siku ya kihistoria sana katika ngome ya mabachela nchini Tanzania baada ya bachela Nguli kujiondoa rasmi kwenye hilo kundi na kujiunga kwenye klabu ya waliooa! Sisi SBP tunawapongeza sana Sam na Mirembe kwa hatua hii na tunawatakia maisha mema ya ndoa

Smiles all over! Samuel na mke wake Mirembe.
Mambo haya yasingekosekana asilani!!


Ukweliii1



Hii picha muhimu sana! Nahisi Papaa alikuwa anamkabidhi rafiki yake Prosper Kijiti na kuweka msisitizo!

Mr&Mrs Sasali wakisindikizwa na Mr&Mrs Mndeme.

Picha zote zimetolewa Facebook page ya MC LUVANDA

Sunday, October 27, 2013

Sikiliza kuhusu daktari aliyejitolea maisha kuokoa wahanga wa ubakaji!

Denis Mukwege, daktari bingwa wa magonjwa ya wanawake kwa zaidi ya takribani miaka 15 amejitolea maisha yake kuokoa wahanga wa ubakaji huko mashariki mwa Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo, DRC. Akihudumia kwenye hospitali ya Panzi huko Bukavu, hospitali aliyoianzisha mwaka 1993, Dkt. Mukwege na wenzake wametoa usaidizi wa kitabibu kwa maelfu ya wanawake waliokumbwa na wanaoendelea kukumbwa na madhila ya ubakaji. Katika makala hii, Joseph Msami alipata fursa kuzungumza na Dokta Mukwege ambaye alifika makao makuu ya Umoja wa Mataifa kwa mazungumzo na Katibu Mkuu Ban Ki-Moon. Katika mazunguzo na Msami, Dokta Mukwege walijadili mengi ikiwemo alivyonusurika kuuawa mwaka mmoja uliopita. 


Monday, October 21, 2013

MILIKI KIWANJA CHAKO POPOTE TANZANIA. KWA WAKAZI WA DAR ES SALAAM VIWANJA MAENEO YA KIGAMBONI, CHANIKA NK

WALE WENYE MAWAZO YA KUJENGA HAPA TANZANIA NA HASA DAR ES SALAAM MSITIE SHAKA TENA, SASA UNAWEZA KUPATA ENEO ZURI LA KUJENGA KWA BEI NAFUU NA KWA UHAKIKA. BEI NZURI YA UNAYOWEZA KUIMUDU HATA MTU WA KAWAIDA. TAFADHALI WASILIANA NA Eneza KWA SIMU HII AKUPE JINSI YA KUMILIKU KIWANJA KWA NAMBA HII.... 0718817706. PIA TAASISI NA MAKAMPUNI WANAOTAKA VIWANJA KWAAJILI YA WAFANYAKAZI. TUWASILIANE TU. 

UTAPATA ENEO LILILOPIMWA USIBUGHUDHIWE NA MTU YEYOTE. MAENEO NI MAKUBWA NA MSAADA WA KUPATA RIGHT OF OCCUPANCY UTATOLEWA KWA WATEJA WETU.

TUNA HAKIKISHA VIPIMO

Friday, October 18, 2013

JIWE KUU - Mwanza.

What a wonderful scene!! I have never seen a rock as big as this! 
Huu mjiwe ni balaa


Eneo la Mihama linaonekana kwa chini.


JIwe kuu!



Mr &Mrs Lwendo above the JIwe kuu.

Umeshawahi kusikia kuhusu Jiwe kuu?? Jiwe kuu ni mwamba mkubwa sana uliopo maeneo ya Bwiru Mwanza. Hili jiwe ni kubwa sana limetapakaa katika eneo kubwa lipo juu sana. Leo nilipata nafasi ya kutembelea huko na kuliona jiwe hili maarufu. Nadhani hii ni sababu nyingine ya hili jiji kuitwa Jiji la miamba. Kama serikali kupitia wizara ya utalii wangetumia fursa, hii nieneo jingine la ukweli sana. Shukrani Kwa GLTI.

Tuesday, October 15, 2013

PROGRAM MAALUM YA REDI YA UM LEO - 15 OCTOBER 2013



Nawatakia kila la kheri kumbukeni mnaweza kupata habari nyingine kupitia  Radio.un.org/sw 

Mwalimu Nyerere miaka 14 baada ya kifo chake, fikra zake zazidi kuchanua

Julius Nyerere, Jabali wa Afrika- Mitizamo toka Arusha hadi Obama, kitabu kilichoandikwa kwa pamoja na Profesa Ali Mazrui na Profesa Linda Mhando. Je nini hasa lengo la kuandika kitabu hiki? Flora Nducha na Assumpta Massoi wa Radio ya Umoja wa Mataifa walipata fursa ya kuzungumza na Profesa Mazrui ambaye alikuwepo katika siku maalum ya kumuenzi Mwalimu Nyerere,mjini New York. Kwanza Profesa Mazrui anazungumzia kilichomtia hamasa 


Saturday, October 12, 2013

Taarifa ya habari ya radio UM - 11 October 2013



Habari zaidi nenda,   Radio.un.org/sw 

Shindano la kimataifa la uchoraji picha kuhusu uokoaji sayari ya dunia.

Shindano hilo mahsusi kwa watoto wenye umri wa kati ya miaka 6 hadi 14, litafikia kilele mwakani ambapo ukomo wa kuwasilisha picha zilizochorwa ni tarehe 15 mwezi Machi mwaka 2014. 



Wadau tunaomba muwahamasishe watoto kushiriki shindano hili na mshindi atapata zawadi ya $2000!!


Kupata maelezo zaidi tembelea Radio.un.org/sw 





NYERERE KUENZIWA KWA TUKIO MAALUM JUMATATU 14TH OCTOBER, NEW YORK

Kwa mara ya kwanza Siku ya ya Baba wa Taifa la Tanzania, Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere itaadhimishwa makao makuu ya Umoja wa Mataifa tarehe 14 mwezi huu. Shughuli hii imeandaliwa na ubalozi wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa ambapo mwandishi wa idhaa ya Kiswahili ya radio ya Umoja wa Mataifa Joseph Msami, amefanya mahojiano na Mwakilishi wa Tanzania wake wa  kudumu katika UM  Balozi Tuvako Manongi na ameanza kwa kumuuliza ninini umuhimu wa siku hiyo?


Shughuli hiyo itaenda sambamba na uzinduzi wa kitabu kiitwacho JULIUS

NYERERE: Jabali wa Afrika katika medani za kimataifa kilichohaririwa kwa pamoja na Profesa Ali Mazrui na Dokta Linda Mhando. Hayati Mwalimu Nyerere alifariki dunia tarehe 14 Oktoba mwaka 1999 nchini Uingereza kutokana na ugonjwa wa saratani ya  damu.

Msami akimhoji balozi Manongi

Friday, October 11, 2013

Taarifa za habari Kutoka Radio ya Umoja wa Mataifa.


Wapendwa wetu na wadau wetu!

Tunapenda kuwataarifu kwamba sasa tumejiunga na radio ya umoja wa mataifa idhaa ya kiswahili na hivyo taarifa za habari za radio hiyo zitakuwa zinapatikana hapa kila siku. tumeweka katika format/mfumo rahisi wa wewe kusikiliza bila tatizo lolote.

Endelea kuburudika na kuelimika kupitia Shalom Broz Productions.

Taarifa ya habari kutoka Radio ya Umoja wa Mataifa - 10 October 2013



Habari zaidi nenda,   Radio.un.org/sw 

Thursday, October 10, 2013

Taarifa ya habari kutoka UN Radio - 09 October 2013



Kwa habari zaidi tembelea tovuti radio.un.org/sw 


Nichague ipi??






Kuna vingamuzi lukuki hapa Tanzania sasa baada ya kuamua kuingia kwenye mfumo wa dijitali tukiachana na ule wa analojia. Kampuni za kutoa huduma hii zimekuwa nyingi sana na wote wanasema wao ndio bora na wenye picha nzuri zaidi. Sasa  mimi nichukue ipi kati ya hizi au nisubirie AZAM TV maana nao nimesikia wako njiani wanakuja....Naombeni ushauri wenu wapendwa!

Thursday, October 3, 2013

JOYCE KIRIA / WANAWAKE LIVE WAFICHUA NDOA YA WATOTO!!




Najua kila mtu mwenye ufahamu wa kawaida kabisa atakuwa ameshtushwa sana na tukio hili. Yaani ni kama tuko nyuma sana na ninahisi tatizo kubwa ni umasikini na njaa za wazazi!

Tunampongeza sana Joyce Kiria pamoja na kipindi cha Wanawake Live kwa kufanikisha kufichua tukio hili. Dada Joy, Keep it up na Mungu akulinde maana maeneo mengine unayoingia ni hatari kama hili. Endelea kufichua haya majanga kwenye jamii zetu.

Video ni mali ya Wanawake Live/Joyce Kiria.

-SBP

Wednesday, October 2, 2013

TUMETIMIZA SEHEMU YA MALENGO YA MILENIA ,YALIYOSALIA TUNAPAMBANA - KIKWETE

Rais wa Tanzania Jakaya Kikwete amesema kwa sehemu kubwa utekelezaji wa
maendeleo ya milenia umefanikiwa nchini mwake licha ya kwamba yako malengo
ambayo bado hayajafanikiwa matahalani usafi wa mazingira na kuanisha
mipango iliyopo katika kuyatimiza.

Katika mahojiano maaluma na Joseph Msami wa Idhaa ya Kiswahili ya radio ya
Umoja wa Mataifa Rais Kikwete amesema nchi zilizoendelea zimekuwa zikisita
kutimiza lengo namba nane linalowataka watoe asilimia saba ya pato la taifa
ambapo akitoa mfano kwa nchi kama Marekani amesema ni kiasi kikubwa na
hivyo kutotomizwa jamabo ambalo kwa ujumla linachelewesha utekelezaji wa
malengo hayo.

Kaka Joseph Msami akimhoji rais Kikwete.

-Kutoka Idhaa ya Kiswahili ya Radio Umoja wa Mataifa.