Tafuta/Search This Blog

Sunday, August 7, 2016

Ni HUMPREY na LEAH!!

 Msafara kuingia kanisani.

 Mkao wa matumaini!

 



Hatimaye Humphrey ni mume wa Leah. Ndoa imefungwa mchana huu hapa Mwanza na sherehe itakuwa leo jioni hapahapa Mwanza.

- Picha kwa Hisani ya Warren Charles.

Hivi ndivyo mambo yalivyokuwa na kumalizikia kwa amani kubwa sana.

Humphrey sasa ni mume wa Leah na Leah ni mke wa Humprey.

SBP inawatakiwa maisha mema sana ya kushesha kitrilionea!! 



--Picha zaidi kwa hisani ya Matilda.





Tuesday, August 2, 2016

Iringa


I think this is one of the best shot ever.

Photo courtesy of @tanzaniaphotos

IMF: Uchumi wa Tanzania waongoza Afrika Mashariki

Tanzania inatarajiwa kusajili kiwango cha juu zaidi cha ukuaji wa uchumi wake mwaka huu katika kanda ya Afrika Mashariki na kati.
Hii ni kwa mujibu wa ripoti ya shirika la fedha la kimataifa - IMF.
Katika ripoti yake iliyotolewa hii leo Tanzania inatarajiwa kusajili kiwango cha juu cha ukuaji wa uchumi wake wa asilimia 6.9% mwaka wa 2016.
Kasi hiyo ya ukuaji wa uchumi wa Tanzania ni ya pili tu nyuma ya Ivory Coast baina ya mataifa ya Kusini mwa jangwa la Sahara .
Ivory Coast inatarajiwa kukuwa kwa kasi ya asilimia 8.5%.
Katika kanda ya Afrika Mashariki ,uchumi wa Kenya ndio wa pili kwa kasi ya ukuaji kwa asilimia 6%.
IMF hata hivyo inasema kuwa kasi ya ukuaji wa uchumi kusini mwa jangwa la Sahara unatarajiwa kupungua kwa mwaka wa pili mfululizo kutokana na kudorora kwa viwango vya uzalishaji na hivyo uwekezaji.
Kwa mujibu wa shirika la fedha la kimataifa - IMF, eneo hilo linakadiria kushuka kwa ukuwaji wa uchumi kwa asilimia 3 mwaka huu.
Kiwango hicho ni cha chini kabisa kuwahi kushuhudiwa katika miaka 15.
Mataifa yanayotegemea mapato yanayotokana na mafuta ndiyo yalioathirika zaidi kama vile Nigeria na Angola.
Aidha Zambia pia imeathirika vibaya kutokana na ukosefu wa soko la kimataifa la shaba yake.
Ripoti hiyo inaitaja Afrika Kusini kama moja ya mataifa ambayo kiwango chake cha ukuaji kimedorora kwa kiasi kikubwa mno.
Katika orodha ya mataifa yanayotarajiwa kuwa na kiwango cha juu cha ukuaji Kusini mwa jangwa la sahara Ivory Coast ndio inayoongoza.
Orodha ya mataifa ya kanda ya Kusini mwa Jangwa la Sahara na viwango vya kasi ya ukuaji wa uchumi 2016.
  1. Ivory Coast 8.5%
  2. Tanzania 6.9%
  3. Senegal 6.6%
  4. Kenya 6%
  5. Zambia 3.4%
  6. Nigeria 2.3%
  7. Afrika Kusini 0.6%  


- BBC
THE BEST IS YET TO COME!!