Tafuta/Search This Blog

Wednesday, February 15, 2017

I have found a new friend...





This young one was left to live in our compound by her mother some few days after she was born. We decided to take care of her and it is some few months down the line and she is becoming a part of our family. She is very charming and playful, she recognizes the sound of our car and run very fast to say welcome home every evening.

My boys have decided to call her Tomtom. She is a good firend

Friday, February 10, 2017

Nice rain shots




Nimekutana na mama Elizabeth Bhoke!

 Katika maisha kuna wakati huwa unaweza ukapata changamoto sana na ikakufanya ujiulize na ujichunguze Imani yako kwa Mungu. Kuna watu wanampenda Mungu sana na maisha yao wamejitoa kwa Mungu kwa asilimia zote. Sasa hii changamoto ndio niliyokutana nayo.

Nimekutana na huyu mama anaitwa Elizabeth Bhoke. Mama huyu ana umri wa miaka 79 na hana mume wala mtoto lakini yeye ni mwinjilisti ambaye huzunguka akikusanya Pesa ili ajenge makanisa katika wilaya ya Serengeti. Mama huyu wa kanisa la Sabato, tayari amejenga makanisa matano huko Serengeti na anaendelea kukusanya pesa ili kujenga mengine.

Huu ni moyo wa ajabu sana sana na kwa kweli umenipa changamoto sana ya kumpenda Mungu zaidi na kujali kile ambacho Mungu amekiweka ndani yangu na kukifanya kwa bidii sana kama huyu mama.

Kama mama huyu atakufikia tafadhali nyosha mkono wako na umbariki. Yeye pia hutoa maneno ya kubariki sana na pia ni mchangamfu mwenye maneno mengi ya kutia moyo....



Im so challenged!. God Bless you mama!

Thursday, February 9, 2017

PAULO MAKONDA NAOMBA UJIFUNZE KWA SIR NICHOLAS WINTON


Nicholas Winton
Ilikuwa mwaka 1938 wakati kijana mdogo wa miaka 29 aliejulikana kama Nicholas Winton ambae aliekuwa ni dalali wa hisa (stockbroker) jijini London aliamua kuacha shughuli zake na kwenda nchini Czechoslovakia. Lengo la safari yake ilikuwa ni kuwaokoa watoto wa Kiyahudi 669 waliokuwa katika kambi ya wakimbizi.

Nicholas alitengeneza mpango wa kuwavusha kutoka Czechsolovakia na kuwapeleka watoto hao England; alipofika England alifanya kazi ya kutafuta familia za Waingereza na kuzishawishi ziwachukue watoto hao kwa lengo la kuwalea.

Katika mpango huo kabambe, Nicholaus alichukua magari 8 na kwa umakini na usiri mkubwa alifanikisha zoezi hilo la kuwaokoa watoto hao. Nicholaus alifanya siri ambayo hata mkewe hakuweza kujua. Miaka 50 baadae, mkewe wakati anapekua pekua vitu, aliweza kuona kitabu kikiwa kimefichwa kwenye dari. Kitabu hicho cha similizi kinachojulikana kama (scrapbook) kilikuwa na majina na picha za watoto wote waliokolewa na Nicholas kwa takribani miongo 5 iliyopita. Mkewe, Greta aliamua kuichukua simulizi hiyo na kumpelekea Elisabeth Maxwell ambae alikuwa mtafiti wa mauji ya kimbari ya Wayahudi (Holocaust) na barua za hao watu waliokuwa watoto nyakati hizo. Kulikuwa na mwitikio kutoka kwa watu zaidi ya 200 kati ya wale 669 katika ile orodha ya watoto kwa miongo 5 iliyopita kwa wakati huo.

Dunia iliyobakia nikiwemo mimi nawe msomaji wangu ilikuja kuifahamu simulizi hii kupitia filamu-simulizi (documentary) iliyotengenezwa na kituo cha habari cha BBC yenye jina That’s life (yaani haya ndiyo maisha). Nicholaus alialikwa kama mmoja wa wahudhuriaji wa katika onesho hilo. Kile kitabu chake cha kumbukumbu kikafunuliwa na maelezo kutolewa, na aliekuwa mwenyeji wa hafla hiyo akauliza umma uliokuwa umehudhuria ambao walikuwa wameokolewa kutoka na uamuzi wa Nicholas kuokoa maisha yao. Zaidi ya watu 20 walisimama wakiwa wamemzunguka Nicholas na kupigia makofi ya kumpongeza na kumshangilia Nicholas.

Waweza kuiona video hiii kupitia tovuti ya www.youtube.com/watch?v=6_nFuJAF5F0 na kumwona mtu mkuu alieamua kugusa maisha ya watu na vizazi vingine baadae maishani. Kwa uchache kati ya watu aliowaokoa ambao ni maarufu katika jamii ni pamoja na Alf Dubs, Baron Dubs (iliezaliwa mwaka 1932) na alikuwa Mbunge wa bunge la Ungereza kwa kupitia chama cha Labour. Heini Halberstam (aliezaliwa mwaka 1926) na alikuwa bingwa wa hisabati. Renata Laxova (aliezaliwa 1931), alikuwa daktari bingwa wa masuala ya vinasaba vya watoto (peadiatric geneticist). Wengine ni Joe Schlesinger (aliezaliwa 1928) alikuwa mtangazaji wa vipindi vya televisheni huko Canada na muandishi wa vitabu. Na wa mwisho kumtaja katika makala hii katika orodha ndefu ni Yitzchok Tuvia Weiss (aliezaliwa 1926), alikuwa Rabi Mkuu Jerusalem. Rabi ni mwalimu wa dini ya kiyahudi.

Mpaka mwaka 2015 shirika la habari Uingereza BBC liliweza kuwasiliana na zaidi ya watu 200 kati ya waliokuwa watoto 669 walioweza kuoka na zahma la mauji ya kimbari.

Kutokana na maamuzi aliyoyafanya Nicholas, amefanikuwa kukusanya tuzo za heshima chungu nzima ikiwemo kupewa cheo cha heshima na ushujaa kutoka kwa malkia Elizabeth II wa na kuwa SIR NICHOLAS WENTON. Jamhuri ya Czech ilimpa Sir Nicholas Wenton tuzo ya heshima ya Simba Shujaa; Kwa upende wake Rais wa awamu ya 7 nchi Israel Ezer Weizman aliwahi kumpa tuzo ya heshima kwa niaba ya Taifa lake. 

Nimeguswa sana na watu wengie pia wameguswa na maamuzi ya Nicholas aliemua kuhatarisha maisha yake na kutumia gharama zake kwenda katika kambi kwa lengo la kuokoa watoto ili mkono wa mauaji ya kimbari wa Adolf Hitler usiwafikie. Miaka 50 baadae simulizi hiyo iliwekwa wazi na watu wengi kujua juhudi na “innitiatives” za Sir Wenton alizofanya akiwa kijana mdogo.

Napiga picha ya initiative ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Ndugu Paulo Makonda ya kunzisha vita dhidi ya uuzwaji wa dawa za kulevya jijini Dar es Salaam. Kimsingi watu wengi wamepokea taarifa hii kwa mshangao kuna kwamba “atafika wapi!”

Aidha kuna wengine wanamkejeli kama mtu anaejaribu kufunika aibu ya wanafunzi wa kidato cha nne kufeli hususan mkoani Dar es Salaam. Wengina wakidhani anatafuta umaarufu. Kila mmoja kwa hisia zake.

Binafsi nampongeza Paulo Makonda kwa nafasi yake na uzalendo wake kwa nchi uamuzi wa kuchukua hatua ya kufanya uchunguzi kwa kushirikiana na vyombo vilivyo chini ya ofisi yake na kutoa amri ya watuhumiwa wanaohusika kukamatwa ili wahojiwe na wengine kusimamishwa kazi ili uchunguzi uendelee pasipo wao kuathiri uchunguzi kama watakuwa kazini.

Nia ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam ni njema. Amenuia kupiga vita vizuri dhidi ya biashara ambayo inaua hatima ya vijana wa Kitanzania. Tukumbuke matokeo ya vijana kutumia “unga” ni kuwaharibia kesho yao na mchango wao ambao wangeweza kuutoa katika ujenzi wa taifa hili.

Ilitakiwa Watanzania kwa nafasi zozote tulizonazo tusimame na Paulo Makonda kwa kuwa anachokipinga ni kitu kibaya. Michelle Obama wakati mmoja aliwahi kusema kuwa “kumpiga vita mmoja wetu ni kutupiga vita sote” Kwa mantiki hiyo kumpiga Paulo Makonda nia yake njema ni kupinga sheria za nchi zenye lengo la kuzuia matumizi, uuzwaji na usambazaji wa madawa ya kulevya.

Ni ukweli ulio wazi kuwa, mtu yeyote mwenye mguso maishani alijengewa mazingira mazuri ya kumsaidia kufika ndoto zake maishani. Mihidarati ni kitu ambacho kinaweza kuharibu tabia njema na mwenendo wa vijana na watoto kuifikia kesho yao. Hivyo basi tunawajibika kuipingwa kwa ngivu zote.

Yawezekana si kila mtu ana nafasi ya kuwa kwenye vyombo vya dola ili kutumia misuli kuzuia utumiaji wa mihadarati au usambazaji; kutokuwa na nafasi kama ya Paulo Makonda au IGP Ernest Mangu, bado tuna jukumu la kupigana kwa kupitia kuwatia moyo wapiganaji walio-mstari wa mbele kwa njia ya kuwaombea kwa Mungu au hata kupaza sauti kupitia vyombo vya habari. Na tukiachukulia mfano wa wapenzi wa soka anafahamu nguvu ya kumshangilia mchezaji au wachezaji wanapofanya vizuri.

Nicholas alifanya maamuzi ya kuokoa watoto 669, miaka 50 baadae, watu wale walikuwa watu wenye mguso akiwemo muandishi wa habari, daktrari bingwa wa watoto, mwalimu mkuu wa dini na wengine wengi. Juhudi za Makonda zikifanikiwa Dar es Salaam na kila mmoja akacheza nafasi yake kutimiza wajibu wake kukaba ili wasambazaji wasiendelee kuuzaa katikati yetu, ni watu wangapi tutawaokoa?
Kama Mtanzania mzalendo, sioni kama mihadarati ina nafasi ya kuongeza thamani katika maisha ya watoto na vijana kama wahanga wakubwa wa mihadarati.

Rai yangu ni kuwa sisi kama wanajamii tunawajibika kwa pamoja kuijenga nchi hii. Jirani akiharibikiwa au mtoto wa jirani akiharibikiwa madhara yake yana uwezekano kwa upande mmoja au mwingine kugusa maisha yangu au watoto wangu. Njia rahisi ni kuamua kupigana kuzuia madhara yasisambae kuliko kuachilia yasambae.

Rais John Magufuli kampongeza IGP Mangu kwa kuchukua hatua ya haraka za kinidhamu kwa watuhumiwa ndani ya Jeshi la Polisi ili kupisha uchunguzi ufanyike.

Tukipanda mbegu njema kwa kugusa maisha ya wengine, ipo siku tutavuna taji ya heshima kwa mrejesho wa watoto wetu na vijana wetu kuwa na mguso chanya kwenye jamii. Ili jamii yetu iwe na uzalishiaji wenye tija (effective production) mihadarati lazima ipigwe vita ndani ya mipaka yetu. Paulo Makonda kaonesha mfano, kwa pamoja tumuunge mkono.

Fredrick Matuja
fmatuja@hotmail.com

Note: Tunamshukuru sana Fred Matuja ambaye amekuwa akitutumia makala ili tushirikiane na wadau mnaopitia kwenye blog yetu.