We are delighted to introduce HOPE FUNERAL SERVICES in Mwanza.
Company is coming to offer the residents of Mwanza Funeral services and support the families during the grieving time of loosing their beloved one.
To start, Hope Funeral Services is bringing you the state of art Funeral vehicle to help you give your beloved family members the well deserved send off.
This funeral vehicle will be available in Mwanza from the second week of April this year.
For any inquiry kindly call the numbers 0764 055413 or 0756 026428.
Hope Funeral Service wishes you a long and Happy life!
Shalom Broz Productions
This is a production house where you will meet talented young men producing Video and graphic designing! SBP ina wataalamu wafuatao: Enson Msuya - Video and imagery specialist, marketing. Godlove Lwendo - Graphic Designer. You can contact us by these numbers, +255 784 494906, +255 756 025428 We will be more than ready to serve you for any of the service you will need from us as we have described them thereup.
Tafuta/Search This Blog
Thursday, April 2, 2020
Thursday, June 20, 2019
SHALOM!
Hellows wapendwa wetu!
It has been so long! So many things have happened to us and we know so many things has happened to you too.
But all in all we are grateful for everything.
Katika mengi ambayo yalitutokea moja kubwa ni kwamba we lost our dear father who was sick for more than ten years.
Mchungaji Gordon Daudi Lwendo, alifariki tarehe 08 Mwezi Novemba mwaka jana wa 2018.
We thank God aliimaliza safari yake vyema na amepumzika.
Lets share some few shots of the send off ceremony we gave him on Dar. He was buried on the 10th of November.
Tunamshukuru Mungu kwa yote na company ya marafiki na ndugu tuliyoipata kipindi hicho and lets ROLL!
It has been so long! So many things have happened to us and we know so many things has happened to you too.
But all in all we are grateful for everything.
Katika mengi ambayo yalitutokea moja kubwa ni kwamba we lost our dear father who was sick for more than ten years.
Mchungaji Gordon Daudi Lwendo, alifariki tarehe 08 Mwezi Novemba mwaka jana wa 2018.
We thank God aliimaliza safari yake vyema na amepumzika.
Lets share some few shots of the send off ceremony we gave him on Dar. He was buried on the 10th of November.
Tunamshukuru Mungu kwa yote na company ya marafiki na ndugu tuliyoipata kipindi hicho and lets ROLL!
Thursday, April 6, 2017
Another new friend!
I just found this cat on the side of the road and it followed me home. I really dont understand...is tis s blessing? Should i call City council for these friends shifting to my house??
Bu this new friend is very cute!!! He is actually matching my carpet.
Im speechless!
Dar Es Salaam kwa ufupi.
Julias Nyerere International Airport.
Julias Nyerere International Airport. |
Samaki wa baharini! |
Samaki watamu sana |
Ujumbe maridhawa kutoka kwenye daladala la Tandika |
Daraja la Kigamboni. Hap Kama unaendesha gari jitahidi uendeshe speed chini ya 30Kph. Wamejibanza jamaa humu wanakupiga picha |
Dar Es Salaam CBD |
Dar Es Salaam CBD |
Dar Es Salaam CBD |
Thursday, March 16, 2017
FC BARCELONA NA GLENN CUNNINGHAM WANATHIBITISHA KUWA TANZANIA YA VIWANDA INAWEZAKANA
Nilipenda kukimbia
tokea nikiwa mvulana. Ilikuwa ni kukimbia maili moja (sawa na kilomita 1.8). Glen
alikuwa mvulana na hadithi yake ni ya kweli na kusisimua yenye mkasa unaotupa
funzo la kuwa ukiwa na nguvu ya dhamira na kufanyia kazi kile unachoamini
hakuna lisilowezekana chini ya jua.
Kwa kifupi hii ni
hadithi ya Glenn Cunningham alezaliwa August 4, 1909 huko Kansas nchini
Marekani.
Akiwa shule msingi
na umri wa miaka 8, siku moja Glenn aliungua moto kufuatia mlipuko mkubwa
darasani ulisababishwa na galoni la mafuta ya Petroli. Nyakati hizo kulikuwa
baridi kali na kila siku wanafunzi walikuwa na jukumu la kuwasha jiko kwa
kutumia mafuta ya taa ili kupasha chumba cha darasa joto. Siku moja, mtu
asiefahamika aliweka petroli kwenye galoni badala ya mafuta ya taa. Glenn bila
kujua aliwasha moto kama kawaida na kupatwa na mlipuko uliounguza mwili mzima
na miguu yake kupoteza hisia kabisa kufuatia kufa kwa mifumo ya ufahamu.
Ushauri wa madaktari
ni kuwa akatwe miguu kwani asingeweza kutembea kabisa maishani mwake. Mama wa
Glenn aliekuwa anaitwa Rosa alikataa ushauri huo wa kumkata mwanae miguu
ulitolewa na daktari. Glenn alikaa hospitali kwenye hali ya kutojitambua (in coma
situation) na baada ya siku nyingi fahamu zilirudi na taratibu hisia za ufahamu
zikaweza kuwa hai tena.
Baadae Glenn alipata
ruhusa ya kwenda nyumban. Akiwa nyumbani alikuwa anawekwa juani na wazazi
kwenye kiti cha magurudumu (wheel chair) kama mtu mwenye ulemavu. Kuifanya
hadithi hii kuwa fupi kuna siku Glenn aliweza kutembea. Alipofanikiwa kutembea
japo kwa kuanguka anguka, aliamini kuna siku anaweza kukimbia. Glenn alikuwa
anatafakari na kukiri kitabu cha Isaya 40:31 “Lakini wote wanaomtumainia Mwenyezi-Mungu,watapata nguvu mpya.Wataruka
juu kwa mabawa kama tai; watakimbia bila kuchoka;watatembea bila kuchoka."
Miaka kadhaa baadae Glenn aliweka rekodi
kadhaa za dunia katika mchezo wa riadha. Ntaziweka rekodi chache hapa chini kwa
ajili ya kumbukumbu.
Alimaliza mbio za riadha za Olimpiki ya majira ya joto
mwaka 1932 na 1936. Akiwa njiani kurejea kutoka kwenye Olimpiki ya nchini
Ujerumani, alipigiwa kura kama mtu maarufu kabisa huko Marekani na wana riadha wenzake
wa Olympiki.
Mwaka 1933 Glenn alishinda medali ya Sullivan kwa
mafanikio yake katika mbio za kati.
Mwaka 1932 kwenye Olimpiki alikuwa mtu wa 4 katika mbio za
mita1500
Mwaka 1936 katika Olimpiki zilizofanyika huko Berlin
Ujerumani, Glenn alishinda Medali ya fedha katika riadha, umbali wa mita 1500
Mwaka 1934, Glenn aliweka rekodi ya dunia kwa kukimbia
maili moja kwa muda wa 4:06.8. Rekodi hii ilichukua miaka 3 kuvunjwa.
Mwaka 1936, Glenn aliweka rekodi ya dunia yam bio za mita
800.
Kwa kifupi Glenn aliweka rekidi nyingi sana. Tukumbuke,
hakutarajiwa kutembea kwa vipimo vya kidaktari kutokana na hali aliyokuwa nayo
kufuatia kuunguzwa vibaya na moto. Glenn alistaafu riadha mwaka 1940 akiwa na
miaka 31.
Hadithi ya Glenn imenikumbusha mechi ya fainali ya mpira
wa miguu kati ya Liverpool na AC Milan ya wakali wa wakati huo kama Andrey
Shevchenko, Paolo Maldini, Kaka na Hernan Crespo na wengine wengi. Mpaka dakika
45 zinaisha vijana wa Anifield walikuwa nyuma kwa bao 3-0. Kipindi cha pili,
Liverpool chini ya nahodha Steve Gerald walirudisha magoli 3 na kuingia katika
changamoto za mikuwaju ya penati. Kwa wapenzi wa soka mnakumbuka, Liverpool
chini ya kocha Raphael Benitez, walichukua kombe la klabu bingwa Ulaya 2005
kufuatia kuwashinda AC Milan kwa mikwaju ya penati.
Usiku wa jana kuamkia leo kati ya saa 4.45 usiku na
kuendelea FC Barcelona ikiwa chini ya Luis Enrique imeleta historia ya kupindua
goli 4-0 za mechi ya kwanza kwa kuibamiza PSG kutoka Ufarasa kwa bao 6-1.
Kufuatia ushindi huo, naomba kunukuu maneno machache kutoka kwa wanakabumbu
kutoka Calanonia.
Gerard
Piqué alisama haya baada ya mchezo… “Tumeona matokeo mengi yakibadlishwa katika soka, ila si kama
ushindi huu” akimaanisha kupidua magoli 4-0. Na kufunga mabao 6-1 ndani ya
dakika 90. Pique aliendelea kusema….”Yeyote asie-amini,
anatakiwa aende na aje tena”
Mtu
mwingine ni nahodha wa FC Barcelona kiungo mchezeshaji, Andrés Iniesta, ambae
alisema hivi…“Tumeshuhudia
kitendo cha kihistoria” Iniesta alihitimisha kwa kusema “Hatukukoma kuamini – kiuhalisia
ilikuwa haiwezekani isipokuwa imetendeka” (We never stopped believing — it was
virtually impossible but it happened.)
Mpira wa jana kati ya FC Barcelona na PSG una mafundisho
makubwa kwetu wanadamu, hususan sisi Watanzania. Tunawajibika kuamini na
kutoacha kuamini kwa jambo jema tunalolipigania haijalishi uhalisia wa matokeo
ya kushindwa huko nyuma ukoje.
Kwa akili tulizo nazo na tukiamua kuweka juhudi kubwa
kuleta msukumo kwenye ujenzi wa Tanzania ya Viwanda hususani lenye nia njema
kwa kutengeneza bidhaa zenye uhitaji katika soko. Tunaweza kubadili maisha yetu kiuchumi na kuwa sehemu ya kujenga daraja la
kada la uchumi wa kati Tanzania
Rasilimali zipo, fursa zipo. Cha msingi tunatakiwa kuweka
msukumo na jitihada kubwa ili kupata matokeo tunayotarajia.
Mkusanyiko wa jitihada (concentrated efforts) na imani ya
kufanya kile unachokusudia bila kukata tamaa, kunaweza kubadili matokeo na
historia ya maisha. Ni kweli Rais Magufuli ana muda wa miezi karibu 17 kati ya
miezi 60 ya utawala wa awamu yake ya kwanza. Na matokeo yataonekana kwa wale
watakao amua kuwa sehemu ya mchezo kubali matokeo na si kulalamika au kuwa
watazamaji.
FC Barcelona wamevuka kwenda robo fainali ndani ya dakika
90. Tumbuke, goli 3 zimefungwa kuanzia dakika ya 87 ukijumlisha na muda wa
ziada (extra time).
Watanzania, tuna nafasi ya kuwa sehemu ya kujenga uchumi
wa viwanda ikiwemo kulima kilimo endelevu kwa kuangalia mahitaji ya soko ndani
nan je ya nchi. . Kenya wametangaza, njaa kutokana na changamoto za mabadiliko
ya tabia nchi. Somalia wametangaza njaa. Djibout na Sudan hali kadhalika. Wingi
wa watu hawa wanahitaji chakula. Tanzania tuna fursa ya kufanya kilimo endelevu
cha umwagiliaji. Tuna fursa ya kuvuna na kusindika mazao ya chakula na mazao
malighafi kwa viwanda ili kukidhi mahitaji ya soko la ndani na nje.
Barcelona waliamini na kutumia jitihada zote ili kuweka
historia. Nasi tuna nafasi ya kuamini na kufanya mambo ya maana. Glenn
hakutarajiwa hata kutembea. Ushauri wa daktari ilikuwa ni kukatwa miguu. Miguu
ya Glenn, maishani mwake iliweka rekodi kadhaa si za kukimbia kama mimi na wewe
ambao tunaweza kukimbia si kwa mashindano, bali Glenn alivishwa medali katika
mashindani makubwa kama Olimpiki ndani na nje ya nchi yake.
Watanzania tunawajibika kuamua. Tunaweza kuwa-prove wrong
wale wasio amini na watazamaji. Nchi za Asia ya mbali miaka ya 60 zilikuwa kama
sisi katika hali ya kiuchumi. Asia waliamua kwa juhudi zote na leo baadhi ya
nchi hizo wanatusaidia kiutaalamu, kutuunzia vitu na mambo chungu mzima.
Ni wakati wa kuamini na kutenda kwa kupigana mpaka mambo
yatokee. Barcelona hawakuwa na muda wa kumlaumu kocha Luiz Enrique. Wachezaji
walicheza mpira ili kuleta matokeo. Watanzania tunawajibika kucheza mpira wa
kuwa sehemu ya maendeleo ya Viwanda. Tukiweza kukuza kundi la wazalishaji bila
shaka kundi la walipa kodi litakuwa na kuongeza makusanyo ya hazina.
Kwa pamoja tunaweza kujienga Tanzania.
Fred Matuja
fmatuja@hotmail.com
Tuesday, March 7, 2017
RAIS MAGUFULI ANATUTAKA TUSOME KITABU CHA DONALD TRUMP
The beginning of every government starts with the education of
our youth.
(Mwanzo wa kila serikali unaanza na kuwapatia elimu vijana wetu)
—Pythagoras
Katika kitabu chake cha “Think Like a Champion” yaani fikiria
kama mshindi, mwandishi Donald J. Trump ambae kwa sasa ni Rais na Amri Jeshi
mkuu wa taifa tajiri na nguvu za kijeshi la Marekani, amenukuu falsafa ya
Pythagoras.
Muandishi Donald Trump, amehimiza umuhimu kwa kujifunza na
kuoanisha aina ya kujifunza kama mwanzo mpya kwenye kila zama ambayo mtu
unaingia. Katika kitabu hicho Donald Trump ameonesha jinsi Pythagoras aliekuwa
nguli wa falsafa hususani katika somo la hisabati, mara nyingi alitafsiri mambo
mengi kwa kuoanisha au kuwakilisha na tarakimu au nambari.
Donald Trump yeye kama mfanya biashara nyakati ameandika na
kupiga chapa kitabu kicho yaani mwaka 2009 ameonesha kuwa kuna muunganiko wa
moja kwa moja kati ya elimu inayompa mtu mmoja mmoja maarifa hali kadhalika
jamii nzima kupata maarifa kupitia mifumo mbalimbali ya elimu.
Mie ninaendika makala hii kwa uzoefu na ujuzi niliopata wakati
nasoma chuo cha ualimu na baadae kupata mafunzo ya taaluma nyingine, naweza
kurejea jambo ambao nimewahi kuandika huko nyuma kuwa sisi wanadamu, tuna namna
ya kujifunza shule au vyuoni (formal education), kuna namna ya tunajifunza kwa
malengo maalum ili kupata ujuzi tunaoutaka (non-formal education). Vilevile
tunaweza kujifunza kwa kupitia vitabu, majarida, mitandao ya kijamii, program
za radio, televiseni n.k na hii inaitwa (informal education). Vyovyote vile,
maarifa tunayoyapata yanatakiwa kutubadilisha namna ya kufikiri na kuzalisha
mabadiliko ya kitabia.
Trump, alijikita katika kusisitiza kila mtu anapoanza jambo
jipya, kuna umuhimu wa kujifunza au kujiongezea maarifa mapya kuhusiana na
mambo mapya anayotaka kuyafanya. Mwandishi ambae ni Rais wa awamu ya 45 kwa
sasa ya Marekani amejielezea kwa uzuri namna ambavyo amekuwa katika kujifunza
ujenzi wa nyumba na hoteli ili anapokuwa na wahandisi-wajenzi walau asiachwe
nyuma na lugha za kimsingi za kiufundi hasa katika ujenzi.
Kuna nyakati alijikita katika uendelezaji wa viwanja vya gofu,
ilimlamlazimu pia atafute kundi la wataalamu wa kucheza mchezo wa gofu na
wajenzi wa viwanja wa gofu. Lengo lake, ilikuwa ni kukaa na wataalamu kwa lengo
la kupata taarifa za msingi kutoka kwenye uzoefu wa sekta au biashara ambayo
alikusudia kuifanya.
Donald Trump aliamini na anaamini sana katika hisia mpya huwa
zinajengwa katika misingi ya mwanzo mpya na mwanzo mpya umeunganishwa na
maarifa mapya yanayopelekea namna mpya ya kufikiri na namna mpya ya kutenda ili
kupata matokeo mapya.
Haina tofauti na msemo wa kibiblia wa umuhimu wa divai mpya katika
chupa mpya ili kupata matokeo tarajiwa. Tofauti na divai mpya unaweka katika
chupa ya zamani. Inapelekea kupoteza divai na chupa hali kadhalika.
Natamani kununua au kuazima uzoefu wa falsafa ya Donald Trump
katika muktadha wa Tanzania ya Rais John Pombe Magufuli na Watanzania walio
wengi.
Kuna namna Mheshimiwa Rais ameingia darasani kama mwalimu na
anatoa mafunzo kwa chaki ubaoni. Wakati Mwl. Magufuli anafundisha kwa mujibu wa
mungozo mpya wa somo (new syllabus) kwa upande mwingine wanafunzi ambao ni
Watanzania wanakumbuka mafunzo na malezi ya Mwl. Jakaya Mrisho Kikwete ya awamu
ya 4. Na wengi wakitaka kuishi kama awamu ya 4.
Falsafa ya Mwl. Kikwete ilikuwa 1+ ( ) = 5. Wanafunzi ambao ni
Watanzania tulikuwa na jukumu la kufikiri ni namba ngapi ikijumlishwa na moja
tunapata 5. Kwa muongozo wa kujifunza haukuhitaji njia ya kuonesha jibu ambalo
ni 4 umelipataje. Na kwa muongozo wa mafunzo yale, ukiweka 4 mwalimu atakupa
vema kwa kuwa jibu ililoweka ni sahihi.
Mara hii ameingia Mwl. Magufuli ambae ana swali kama lile la
mwalimu wa awamu ya nne, isipokuwa badala ya parandesi, wakati swali lina
herufi X
1+X = 5.
Mwalimu Magufuli anataka utafute thamani ya X kwa njia za
kihisabati za jiometri.
Sote tunakubaliana kuwa thamani ya X ni 4, isipokuwa njia ya
kuifikia 4 ni tofauti na muongozo wa mafunzo ya Mwl. Kikwete.
Awamu ya 5 anatutaka ili kupata jibu, sisi Watanzania ambao ni
wanafunzi darasani, tuna wajibu wa kujua kwamba tunatakiwa kuonesha njia ya
kulifikia jibu ambalo ni 4.
Kwa lugha rahisi inatakiwa kuchukua swali 1+X = 5 na kutoa 1
kila upande
1+ (-1)+ X = 5 – 1
Jibu litakalopatikana litakuwa wazi kabisa kuwa
0 + X = 4
Hivyo basi kumbe thamani ya X = 4.
Huu ndiyo mfumo wa muongozo wa mafunzo anayotumia mwalimu wa
awamu ya 5. Kuna uwezekano kutokana na wepesi wa masomo awamu ya 4, kuna
nyakati mwalimu alihitaji tuimbe nyimbo kama sehemu ya kujifunza.
Isipokuwa muongozo wa kujifunza na kufundishia uliopo sasa
watutaka tujue namna tofauti ya kutafuta thamani ya X. Muongozo wa mwalimu
hautupi fursa ya kuimba kama namna ya kujifunza kama kule nyuma. Na hapa ndipo
tofauti inapoanza kuonekana kwani baadhi ya wanafunzi bado wanatamani uji kumbe
tupo katika zama za kula ugali na nyama ya mifupa. Tunawajibika kutumia meno
yetu kutafuna kuitoa nyama katika mifupa.
Wanafunzi darasani (yaani Watanzania wengi) bado wanataka mwl.
Magufuli afundishe kama mwl. Kikwete na kutumia njia za zamani kuja na jibu la
thamani ya X.
Nitoe rai kwa Watanzania wenzangu ambao ni wanafunzi katika
darasa la mwalimu wa awamu ya 5; chonde chonde, tuna jukumu moja kubwa la
kufanywa upya namna ya kufikiri. Namna pekee ya kufikiri na kukubaliana na
ukweli, mfumo mpya wa muongozo wa mafunzo ndivyo unavyotaka, na mwalimu tulie
nae, muongozo wa masomo na mbinu zake za kujifunzia si kuimba (nibebe
nibembeleze kama wimbo mmoja uliowahi kutamba katika nyimbo za injili).
Tukiji-position kwa kujua tupo awamu ya 5 na kuamua kujikita
katika mbinu mpya za kukokotoa ili kupata majibu; tukifanya hivyo bila shaka
lawama na manung’uniko yataisha. Na tutajikuta tunawajibika na kujituma kwa
kutumia mbinu halali na njia halali ya kufikia jibu.
Tukigoma kujifunza, tunajiweka katika hali ya kutokua kiufahamu
hususani kwenye kukabiliana na changamoto zinazotuzunguka.
Tunaweza kupata jibu la changamoto nyingi ikiwemo kutengeneza
hela kihalali bila kutumia njia za mkato pale tu tunapojua, awamu hii na muhula
huu, unahitaji mtanzamo mpya katika utatuzi wa matatizo yanayotuzunguka.
Na utatuzi unapofanyika, maana yake njia ya kufikia jibu
inatakiwa kuwa wazi ili mtu yeyote anaekagua namna mwanafunzi alivyopata jibu,
bila maswali ya ziada aone jibu lilivyopatikana.
Ili tufaulu hisabati za mwl. Magufuli hatuna budi kumpenda na
kumkubali kuwa ndiye mwalimu wetu na tunawajibika kukubaliana na mbinu zake za
kufundishia na kujifunza ili kupata matokeo tunayotarajia.
Wataalamu wa saikolojia wanaonesha kuwa, wanafunzi hufaulu vyema
pale wanapokuwa na uhusinaano mzuri na mwalimu huhusani kwa kumpenda na
kushirikiana nae hata nje ya saa za darasa kwa kwa nia njema ya kujifunza ili
kutatua mafumbo kwa lengo la kupata majibu.
Chuki kwa mwalimu hupelekea kuchukia somo vilevile, na hatimaye
kushindwa kukabili changamoto za masomo. Ufaulu wa masomo ni faida ya
mwanafunzi kupata daraja zuri au alama nzuri. Ufaulu wa kutatua changamoto
zinazotuzunguka, sisi wanafunzi (Watanzania) ni wafaidika wa kwanza.
Hii yanikumbusha siku chache zilizopita nilipata kuhudhuria
mafunzo yaliyokuwa yakifanywa na maafisa wa kijeshi. Moja ya kitu nilichopata
katika mafunzo yale, ni namna wapiganaji hao wanavyofikiri ili kupata majibu ya
utatuzi wa maswali magumu au changamoto mbele yao.
Afisa mmoja akatoa mfano, ukikutana na mto wenye mamba wakali na
unatakiwa kuvuka upande wa pili wa mto; Je utapita katikati ya maji ili mamba
wakutafune au utafanya nini. Afisa yule wa kijeshi akaweka wazi kuwa, kuna
namna ya kuishughulisha akili ili kupata suluhisho la kusonga mbele na
kuendelea na safari ili kufika kule unakotaraji.
Moja ya suluhisho lililotolewa na mpiganaji yule ni kurusha
kamba upande wa pili wa mto na kuifunga kamba nyingine kwenye kipago au mti
mubwa na kisha kuvuka kwa kutambaa kwa miguu na mikono kwenye kamba huku mamba
wakikukodolea macho unapopita juu yao.
Kwa mtu mwingine angeweza kurudi alikotoka, mwingine angeweza
kutupa lawama ooh… kuna mamba kwenye mto, na mie siwezi kuvuka. Tofauti ya
kufikiri kwenye tatizo lile lile ndilo linawafanya Wanajeshi kujiona washindi
na akili zao zimejiengwa kusonga mbele hata pale mambo yanapokuwa magumu. Hivyo
kurusha kamba upande wa pili na kisha, anavuka kwa kamba ni moja ya mbadala
katika mbinu mpya ya kutatua tatizo la mto wenye mamba.
Katika nyakati hizi, tuna wajibu wa kufikiri kwa kiwango sawia
na muongozo wa somo la awamu ya 5. Moja ya assignment (homework) aliyoitoa
mwalimu Magufuli wakati mmoja akiongea na wahariri, ni waandishi kufungua
kampuni ili kujenga viwanda au kuwa na shughuli ya uzalishaji mkubwa unaotoa
ajira kwa vijana na kuongeza thamani ya malighafi hasa za mazao ya kilimo na
mifugo. Nae Mheshimiwa Rais alitoa ahadi ya kusaidia mchakato ili kampuni hilo
lipate mkopo kutoka benki ya ukekezaji. Je kuna, mtu au waandishi wameshapeleka
andiko la mradi wa kampuni na mwalimu wetu wa darasa la awamu ya 5 akashidwa
kutoa msaada? Au ndiyo wengi wanatumia kalamu na keyboard za social media
kulalamika tu?
Kumbe tunaweza pia kungusha mti na kuulaza upande mmoja wa mto
kwenda upande mwingine na kuvuka kwa kutambaa juu ya gogo la mti na kuendelea
na safari ya maisha pasi kulalamika kwanini mwalimu anatuelekezea njia ngumu za
kupata matokeo.
Mungu ibariki Tanzania. Tuna jukumu la kumkubali mwalimu wetu
ili tufaulu mitihani katika zama za mafunzo mapya ili kupata alama nzuri na
kusonga mbele katika hatua ijayo.
Fred Matuja
fmatuja@hotmail.com
Tuesday, February 21, 2017
Wednesday, February 15, 2017
I have found a new friend...
This young one was left to live in our compound by her mother some few days after she was born. We decided to take care of her and it is some few months down the line and she is becoming a part of our family. She is very charming and playful, she recognizes the sound of our car and run very fast to say welcome home every evening.
My boys have decided to call her Tomtom. She is a good firend
Friday, February 10, 2017
Nimekutana na mama Elizabeth Bhoke!
Nimekutana na huyu mama anaitwa Elizabeth Bhoke. Mama huyu ana umri wa miaka 79 na hana mume wala mtoto lakini yeye ni mwinjilisti ambaye huzunguka akikusanya Pesa ili ajenge makanisa katika wilaya ya Serengeti. Mama huyu wa kanisa la Sabato, tayari amejenga makanisa matano huko Serengeti na anaendelea kukusanya pesa ili kujenga mengine.
Huu ni moyo wa ajabu sana sana na kwa kweli umenipa changamoto sana ya kumpenda Mungu zaidi na kujali kile ambacho Mungu amekiweka ndani yangu na kukifanya kwa bidii sana kama huyu mama.
Kama mama huyu atakufikia tafadhali nyosha mkono wako na umbariki. Yeye pia hutoa maneno ya kubariki sana na pia ni mchangamfu mwenye maneno mengi ya kutia moyo....
Im so challenged!. God Bless you mama!
Subscribe to:
Posts (Atom)