Mara zote waTanzania tumejisifia utulivu, amani umoja na upendo katika nchi yetu ya Demokrasia. Na tumekuwa na tabia ya kuficha baadhi ya maovu tunayoyatenda humu kwenye jamii yetu ili hii sifa njema isiharibike. Lakini kwa kweli kuna mambo ambayo yanakuwa too much na yanaudhi...na ajabu yake sasa ni kwamba mambo hayo yanaendelea kutendwa na viongozi wa jamii yetu wamekaa kimya kama vile kwa wao kuwajibika kutaharibu kitu flani! Hii inakera sana!!
Jana kulikuwa na habari kwamba wanafunzi "wakaidi" wa Kibasila Secondary School ya Dar es Salaam wamepambana na polisi baada ya kuamua kufunga barabara kwa kuwa mwenzao mmoja aligongwa na gari alipokuwa akitoka shule. Soma hapa. Sasa hapo ndipo hasira yangu inapoanzia. Watoto hawa hawa walilala barabarani mwaka jana kwa tatizo hili hili kwamba mwenzao mmoja aligongwa na gari hapo mbele ya shule na mkuu wa mkoa akaenda wakaongea na kukubaliana kwamba mahali pale patawekwa taa za kuongoza magari. Hadi linatokea tukio la jana hizo taa hazijawekwa na badala ya kusolve tatizo kwa kuweka taa mahali hapo ndio hao wanafunzi wakaitwa wakaidi na nguvu ya dola ikatumika dhidi yao. hata mtu asiye na akili atagundua kwamba hawa wanafunzi wanachodai ni haki yao na walipaswa kupigwa mabomu ya machozi ni mkuu wa mkoa na mkuu wa kikosi cha usalama barabarani.
Eneo lile limekuwa na ajali nyingi sana na ni karibu sana na kituo cha polisi, swali la kujiuliza ni kwa nini eneo lile haliwekwi taa za kuongoza magari?? Tatizo ni pesa au umeme?? au labda ni eneo maalum la kukamulia damu za waTanzania kwa ajili ya kafara ya Taifa???
Hivi mnategemea hawa wanafunzi mnaowapiga mabomu leo kwa sababu tu wanataka haki yao kesho mtawaambia waache ubinafsi wakiingia maofisini watawasikiliza?? Tunatengeneza Taifa la watu wenye uchungu na chuki kwa dola na uongozi kwa ujumla.
Ingekuwa ni taifa la watu makini nilitegemea kwamba mkuu wa mkoa wa Dar es salaam pamoja na viongozi wa kikosi cha usalama barabarani wakiongozwa na mkuu wao wangekwenda kuomba radhi kwa wanafunzi hawa majasiri na kuanza ujenzi wa taa za kuongozea magari eneo hili mara moja!!
Ninafahamu kwamba hawa wahusika hawasomi hii blog yetu lakini kama kuna mtu anawafahamu hebu uwafikishie ujumbe huu na uwaambie kwamba tumechoshwa na mambo yao ya ajabu wanayofanya. Na pia kuna siku hawa watanzania wanaowafanyia haya watachoka!!
Mungu ibariki na kuilinda Tanzania,
Poleni sana wanafunzi wa Kibasila Sec School na pia hongereni kwa kitendo cha ujasiri mlicho fanya!!
Picha ya Michuzi Blog.
-Kaka Gee.



















signing of the contract
pamoja na wasindikizaji.