Tafuta/Search This Blog

Sunday, August 15, 2010

To worship you i live


Kaka Leonard Swai akiwa amepozi na tshirt yake yenye maneno TO WORSHIP YOU I LIVE.

Tshirt hii ni moja kati ya products zetu. Unaweza ukaorder ya kwako na ukatengenezewa.

Saturday, August 14, 2010

Taswira za Arusha weekend

Maeneo ya karibu na Kisongo airport, panaitwa Shanga.

Kona mbauda.




Sijui ni baridi au kukata tamaa...



Sunday, August 8, 2010

Praise and Worship Month, Calvary temple

Kama kawaida na ratiba ya kanisa la Calvary temple Arusha, mwezi wa nane ni mwezi wa kusifu na kuabudu pamoja na shukrani. Mambo yameshaanza na sifa pamoja na ibada zinaendelea!!

Hii ni katika ibada ya jumapili ya leo tarehe 8 August 2010.

mass choir.


Ndg Pondo akiwa sambamba na mwimbaji Jobiso kutoka Moshi pamoja na wwatumishi wengine wakicheza kwa furaha.


Tolla G na ndugu Samuel nao hawakubaki nyuma.


Kama wewe ni mkaazi wa Arusha unakaribishwa sana kwenye ibada zetu kila jumapili na jumatano pamoja na ijumaa.

Wednesday, August 4, 2010

TAKUKURU!!

Napenda kuchukua fursa hii kuwapongeza sana kwa kusikika kuliko kipindi chochote tangu kuanzishwa kwenu!! Ninaamini kuna waTanzania wengi walikuwa hawawafahamu na walikuwa pia hawajawahi kuelewa vyema kazi zenu lakini sasa karibu kila mtu anawahamu including watoto wadogo! Tena najaribu kuhisi kwamba ina wezekana kuna watu watakuwa wanadhani labda "takukuru" ni kipengele flani cha mambo ya uchaguzi maana kipindi hiki TAKUKURU imesikika mara mia zaidi! Kwa kweli mimi na SBP tunawapongeza sana kwa kusikika!!

Sasa ninatamani mnijibu jambo moja tu ili niwe na moyo mweupe kabisa!! Kwani kazi yenu ni kuangalia rushwa za uchaguzi peke yake au kwa makini zaidi?? Mimi ninaona kama mmezidisha nguvu sasa ivi kuliko kipindi kikngine chochote. Mbona mabarabarani kuna rushwa za waziwazi tu, mahospitalini kibao achana na ofisi nyingine za kutolea huduma?? Mimi nadhani kama mmngekuwa na ksi hiyo mliyonayo kwenye uchaguzi mkaiapply kwenye mambo yute Tanzania ingekuwa ya kwanza Africa kwa kupambana na rushwa.

Nadhani kuna kitu cha kujifunza na kufanyia kazi! Maana sasa ivi mmezama kwenye uchaguzi kwingine mmesahau! Hebu prove yourselves right kwa kufanya vizuri au kama ikishindikana uchaguzi ukiisha mrudi kwa kasii, hatutawacheka!!

Habu libadilisheni hili taifa jamani.

Ninaamini sitachukiwa kwa kusema ukweli...

-Godlove.

Saturday, July 31, 2010

Hey, We are graphics designers

We are pleased to inform you that we can design graphics for all your needs. We can design web banners adverts and function cards at a very reasonable price. Discount will be given to all Shalom Broz followers. Here are the samples of some of our works.






















We can also design and print Tshirts!! Please call us or email us for more information.
One among the tshirts that we have already printed

Lets make it happen!!!!!!!!

Tuesday, July 27, 2010

Medani za Siasa

Pweza Paulo alipopewa kutabiria mahasimu wawili wa uchaguzi mkuu wa Tanzania Oct 2010.

Thursday, July 22, 2010

Fuso pori

Hapa fuso inasubiri kukamilisha kupakizwa mzigo na kuanza safari...

Kijenge chini- Arusha.

Monday, July 19, 2010

Ugweno, Wilaya ya Mwanga, mkoa wa Kilimanjaro!

SBP ilipata nafasi ya kutembelea maeneo ya Ugweno katika wilaya ya Mwanga mkoani Kilimanjaro. Hizi ni taswira za huko na kwa kweli Tanzania bado ni nchi nzuri ya kupendeza!!

Huko ni fullu maDish yaani ni mahabari na kila kitu cha lininga!!



Hili ni ghorofa lililojengwa kabla ya miaka ya 1945 na hadi leo lipo gado kama linavyoonekana. Ajabu!

Kinyozi siriazi!!

Usifanye mchezo na kazi za watu!!

video kwa hisani ya MarafikiHuru.

Sunday, July 18, 2010

Moshi tena...


Nilipata nafasi ya kuutembelea mji msafi wa Moshi weekend hii. Nilipokuwa kwenye kituo chao cha basi(bus terminal) ambayo kwa kweli ni ya kisasa, nilipiga hii picha. Nikagundua kitu kimoja kwamba maaskari wa usalama barabarani ndio wanaoshughulika pia na kuyapanga mabasi hapa kituoni na kuhakikisha hakuna matatizo yeyote yanayofanywa na madereva wa mabasi. Hii niliipenda. Lakini pia nikaona jambo jingine ambalo dada yangu Subi ataniunga mkono kwamba matangazo ya biashara (mabango) yamekuwa mengi sana. Kwa upande huu niliopiga picha tu nimeyahesabu yako 9!! Inawezekana kufanyika kitu cha kuyapunguza ili miji yetu ipendeze zaidi?? Nawakilisha!!