![]() |
| Foleni kubwa kutokana mvua hiyo... |
This is a production house where you will meet talented young men producing Video and graphic designing! SBP ina wataalamu wafuatao: Enson Msuya - Video and imagery specialist, marketing. Godlove Lwendo - Graphic Designer. You can contact us by these numbers, +255 784 494906, +255 756 025428 We will be more than ready to serve you for any of the service you will need from us as we have described them thereup.
Tafuta/Search This Blog
Thursday, September 27, 2012
Friday, September 14, 2012
Emmanuel Na Anna wameremeta
Nakupena Anna
Nakupenda Emmanuel
Pokea pete hii
Wapigaji kbaoooooooo!
Libeneke la kukata kwa chain saw
Wazamiaji hawakosagi
Loveness Costantine aongeza miaka duniani.
Cake taaaamu
Loveness na mpambe wake Shamma
Pozi la pinda shingo
Baba na mama wapongeza mtoto kukuwa. wameahidi kufuga mbwa pale home kwao
Friday, September 7, 2012
Kazi na dawa.
Hii nilikuwa sijawahi kuisikia...
Wednesday, September 5, 2012
SOMA NJE YA NCHI
Dasprom Tanzania pamoja na Dort
Africa Company LTD wanawaletea Utaratibu
Mzuri kwa WENYE NDOTO ZA KUSOMA NJE YA NCHI. Masomo kwa bei nafuu kumwezesha
Mtanzania wa kipato hadi cha chini kumudu gharama.. Ni katika nchi za USA,
Australia, UK nchi za Kiscandnavia na Ukraine, Wale waliofaulu elimu ya Sekondari
form 4 na form 6 na wanataka kujiunga na
digrii ya kwanza, au wale wa Vyuo kwa kujiunga na Master degree tafadhali tembelea mtandao wetu www.overseastudies.info
au piga simu lucas 0713538820 na
0754871147...Eneza 0784494906 .na 0718817706 au barua pepe.. dsm@europe.com lucasmathw@yahoo.com . Skype Wahi kupata nafasi hii.
Ofisi zetu
zipo Mnazi Mmoja Jengo la Ushirika Ghorofa ya 7 chumba namba
710 na 711
Tufikie kwa jinsi unayoona ni rahisi zaidi kwako.
Mamia wamzika mwandishi aliyeuawa
MWENYEKITI wa Klabu ya Waandishi wa Habari ya Mkoa wa Iringa (IPC), Daudi Mwangosi aliyeuawa kwa kupigwa kwa bomu la machozi, amezikwa jana saa 7.30 mchana kijijini kwake Busoka wilayani Rungwe, mkoani Mbeya.
Wakati maziko hayo yakifanyika, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi alisema ameunda tume huru kuchunguza mauaji ya Mwangosi, ambaye pia alikuwa mwandishi wa habari wa kituo cha televisheni cha Channel Ten.
Tume hiyo itakayoongozwa na Jaji mstaafu Stephen Ihema, ina wajumbe wengine wanne wakiwemo wanahabari Pili Mtambalike kutoka Baraza la Habari Tanzania (MCT) na Theophil Makunga kutoka Jukwaa la Wahariri (TEF).
Mbali na wanahabari hao, wengine ni Naibu Kamishna Isaya Mungulu kutoka makao makuu ya Polisi na Kanali Wema Wapo kutoka Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ).
Akieleza kuundwa kwa tume hiyo, Nchimbi alisema ameiagiza ije na taarifa ambayo itaaminiwa na wananchi ndio maana ameteua wajumbe kutoka TEF, MCT na wataalamu wa mabomu kutoka ndani ya JWTZ na iongozwe na Jaji.
Hadidu za rejea Dk Nchimbi alisema tume hiyo inatakiwa kujibu maswali sita ambayo hayajapata majibu.
Alitaja maswali hayo kuwa ni nini chanzo cha mauaji ya Mwangosi, na kama kuna ukweli kuwa kuna uhasama kati ya polisi wa Iringa na waandishi wa habari wa mkoani humo.
Swali la tatu ambalo Nchimbi alisema tume hiyo inatakiwa kuja na jibu ni kama kweli kuna waandishi watatu wa mkoani Iringa ambao wako kwenye orodha ya kuuawa na polisi hao na swali la tano ni kama nguvu iliyotumiwa na polisi Nyololo, alikouawa Mwangosi, ilikuwa sahihi.
Waziri huyo alisema swali lingine ni kama kuna utaratibu kwa vyama vya siasa kukata rufaa kama haviridhiki na uamuzi wa Polisi na kama kuna uhusiano mbaya kati ya polisi na baadhi ya vyama vya siasa hapa nchini.
Alisema tume hiyo inatakiwa impe majibu ndani ya siku 30 na iwapo watahitaji msaada wa kitaalamu kutoka nje ya nchi, Serikali iko tayari kuagiza wataalamu hao, ili waisaidie ili mradi tu wapate majibu yenye kuridhisha.
Alipoulizwa kama yuko tayari kumsimamisha Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Iringa, Michael Kamuhanda ili kupisha uchunguzi huo, Dk Nchimbi alisema ndani ya tume hiyo kuna Naibu Kamishna wa Polisi; hivyo kamanda huyo ambaye cheo chake ni Kamishna Msaidizi hana ubavu wa kuharibu uchunguzi huo.
Kuhusu askari aliyempiga bomu Mwangosi kama anashikiliwa na polisi au bado yuko nje, Dk Nchimbi alisema atachukua hatua mara baada ya tume hiyo au ile ya Polisi, iliyoundwa na Mkuu wa Polisi, IGP Said Mwema kukamilisha uchunguzi wake.
Tume ya Mwema inaongozwa na Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), Robert Manumba. Aidha, Dk Nchimbi alisema hakuna kitu cha kusherehekea wala kushabikia wakati aliyeuawa ni binadamu.
“Ripoti mojawapo ikitoka kati ya tume hizo mbili, hatua zitaanza kutekelezwa kwani zitakuwa na baadhi ya majibu ya maswali haya,” alisema Nchimbi. Dk Nchimbi kujiuzulu?
Kuhusu kama atajiuzulu iwapo ripoti itabaini kuwa polisi ndio waliofanya mauaji hayo, Dk Nchimbi alisema “Nikijiuzulu mtampata wapi waziri kama mimi? (kicheko) Shauri yenu…lakini nawahakikishieni kuwa ukweli utaanikwa wazi.”
Akijibu swali kwamba polisi wanatumiwa kukikandamiza Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) na kwa manufaa ya CCM, Dk Nchimbi alisema hataruhusu hali ya namna hiyo na akasisitiza kuwa polisi wamekuwa wanatekeleza agizo la Msajili wa Vyama vya Siasa la kupiga marufuku mikutano ya kisiasa katika kipindi hiki cha Sensa ya Watu na Makazi.
Alipotolewa mifano ya namna ambavyo wanachama wa CCM wamekuwa wakifanya mikutano yake bila kuingiliwa na Polisi, Dk Nchimbi alisema alipata taarifa hizo na akamjulisha Katibu Mkuu wa CCM, Wilson Mukama ambaye alimhakikishia kuwa hakuna mkutano wa hadhara unaofanywa na chama chake badala yake wanafanya vikao vya ndani.
“Mikutano ya ndani haikupigwa marufuku, kilichokatazwa ni mikutano ya hadhara na ninaomba wenzetu wawe wastahimilivu kwani zimebaki siku nne tu za sensa,” alisema Dk Nchimbi.
Vitisho vya mauaji Katika mazungumzo yake pia, Dk Nchimbi alimlaumu Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa kuwa ni mmoja wa watu waliosababisha mauaji hayo kwani Septemba mosi, siku moja kabla ya mauaji hayo, alimwandikia IGP ujumbe unaoonesha kuwa walidhamiria kufanya vurugu.
Alinukuu ujumbe huo unaodaiwa kuandikwa na Dk Slaa; “IGP nasubiri simu yako, wajulishe polisi wako waandae risasi za kutosha na mabomu ya kutosha. Mtakuwa na karamu ya mauaji na kisha mtasherehekea, mjiandae kwenda Mahakama ya The Hague. Ni afadhali tufe kuliko manyanyaso haya, Dk Slaa.”
Waziri huyo alisema anamshangaa IGP Mwema kwa nini polisi hawajamkamata Dk Slaa na kumhoji kwani ujumbe wake aliotuma unaashiria kutaka kuanzisha vurugu kama ilivyotokea huko Nyololo.
Maziko ya Mwangosi Mamia ya wakazi wa kijiji hicho, wanasiasa wa CCM na Chadema na waandishi wa habari kutoka mikoa ya Iringa na Mbeya walishiriki katika maziko hayo yaliyoratibiwa na waandishi wa habari.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais asiye na Wizara Maalumu, Profesa Mark Mwandosya na Dk Slaa walishiriki maziko hayo ambayo nusura yatawaliwe na hisia za kisiasa kabla IPC kwa kushirikiana na waandishi wengine kuidhibiti hali hiyo.
Katibu Msaidizi wa IPC, Francis Godwin aliwatahadharisha wanasiasa wa vyama hivyo kwamba Mwangosi atazikwa kama mwandishi wa habari japokuwa aliuawa katika tukio lililohusisha shughuli za kisiasa.
Katika rambirambi zao, IPC walitoa kwa familia ya marehemu Sh 750,550 huku Klabu ya Waandishi mkoani Mbeya (MPC) ikitoa kiasi kama hicho ambacho sehemu yake kubwa ilitumika kufanikisha shughuli ya maziko hayo.
Dk Slaa alisema watabeba jukumu la kumsomesha mtoto wa kwanza wa Mwangosi. Mtoto huyo ambaye hata hivyo jina lake halikupatikana mara moja yupo kidato cha nne katika Shule ya Sekondari ya Malangali, wilayani Mufindi mkoani Iringa.
Naye Profesa Mwandosya alisema atabeba jukumu la kuwasomesha watoto wengine wa marehemu huku akiahidi kufuatilia ahadi za watu wengine katika kuisaidia familia ya Mwangosi kwa kuwa marehemu huyo ni ndugu yake wa jirani.
Wengine waliochangia familia ya Mwangosi ni Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Iringa (Chadema), Chiku Abwao aliyetoa Sh 100,000
Stori kwa misani ya Singida Connection Blog
Tuesday, August 28, 2012
Papaa On Tuesday......Maisha Ya Pembe Tatu Ni Kwazo la Maendeleo Kwa Mkristo-2
Niwasalimu Kupitia jina la Bwana
wetu Yesu Kristo.
Wakati Zoezi La Sensa Limeanza nilibahatika kuhesabiwa siku ya Jumapili na kwa dakika zisizozidi 10 nilishaongea mengi na aliyekuwa Karani Wa Sensa Kwenye Nyumba yetu. Kati Ya Mambo tuliyoongea kidogo ni Mfumo wa Maisha tuliyoamua kuishi Watanzania am Wakristo Kwa Ujumla Wao. Na Katika Mazungumzo nilikuja baini kumbe Jamaa ananifahamu na ni Msomaji Mzuri wa Blog Hii akanikumbusha Papaa On Tuesday ambayo ilimbadilisha namna ya Kuwaza ambayo ilibidi niisome tena siku ya Jumapili Usiku kuona kile ambacho kiliandikwa mwaka Juzi kilikuwa ni nini hasa.
Niwashukuru Wasomaji wa Blog na Marafiki wa Facebook waliokuja kwenye Presentation Ya Papaa On Tuesday niliyofanya Live Pale VCC Jumamosi hii ya 'Think Differently and Make a Difference". It was Awesome sana Mungu awabariki.
Kati ya Mambo unapaswa to think Differently and Make a Difference ni mfumo wa maisha ya pembe tatu tunayoishi nikiwa na maana, 1. Unapolala (Nyumbani) 2. Unapofanya shughuli zako (Kazini ama shuleni) 3. Unaposali (Kanisani ama Fellowship).Kuna watu wakiamka asubuhi wanajiandaa kwenda kazini ama darasani, wakitoka wanaenda labda kanisani ama fellowship kisha wanarudi nyumbani kulala, kesho yake wanaamka wanarudia mzunguko huo huo.

Nichangamoto kubwa sana ya kizazi hiki ambacho kila mtu anataka kuwa "mjasiriamali" wa namna moja ama nyingine ama mtu unakusudia kuongeza kipato chako cha fedha then una maisha ya pembe tatu. Mtu yeyote unayemuona either amefanikiwa kwa namna moja ama nyingine lazima huyu mtu anamizunguko zaidi ya hiyo uliyonayo. Usitafute mchawi mchawi ni wewe mwenyewe.
Siku Moja Swahiba Prosper Mwakitalima aliniambia niambia "Hakuna tusi baya kama kusema haiwezekani, then ukakuta kuna mtu amefanya". Kati ya vitu ambavyo tunavyo na hatupendi kuvitumia ni ubongo, mfumo wa makuzi na malezi tuliyokulia umetusababishia mtu mwingine awaze kwa niaba yetu sisi tuchukue mawazo yake, huwezi kuwa msomi mwenye akili za kutosha na ubunifu wa hali ya juu kwa kutegemea "madesa", notes za handout na past papers, ndio maana waliokuwa wazuri "kukariri" darasani kwenye maofisi huku ni wengine ni vituko. Mimi ni mwandishi lakini nina taaluma yangu,ninapoandika na kusababisha hii Blog iwe na mambo ya maana iwe current sio sababu ya maombi, sababu kubwa am working hard for this, nachelewa kulala sababu ya kuwaza, inanipasa kusoma sababu ya hii, inanigharimu muda ili wewe usome, inanigharimu fedha ili mtu mmoja apone, we will never be the same my dear. Chukia mizunguko mitatu kwenye maisha yako.
Unaweza pata wapi mawazo ya
biashara kwa maisha ya pembe tatu, unaweza pata wapi wateja ama network ya watu
kwa maisha ya pembe tatu, unaweza fanya jambo gani kwenye Jamii kwa maisha ya
pembe tatu??kila utakachokuwa unaongea ni Kazini kwetu, Kanisani kwetu, kwenye
TV kwenye nini sijui...Wake Up. Kwa taarifa yako kuna watu wa rika lako
wanafanya mambo makubwa wewe ukiwa bado unawaza nini cha kufanya. Kuna wanafunzi
kama wewe wameanza kujiongezea kipato chao, kuna wafanyakazi kama wa ngazi yako
hawategemei mishahara yao..tatizo kubwa sisi tukitoka kazini haooooooo,
kanisani, tukitoka kanisa haooooooo kulala, get me well kuna wengine hata
maofisini mwao ama shuleni ama vyuoni mwao ama kanisani kwao hawaoni kama hao ni
Opportunity kwenye maisha yao.
Kuna wengine mpaka sasa hawajaoa wala hawajaolewa si kwa sababu Bwana hajataka ila Mfumo wao wa maisha una walostisha, kuna wengine mpaka sasa hawajapata kazi si kwa sababu Bwana hajataka ila mfumo wapembe tatu unawalostisha, kuna wengine mpaka sasa biashara ni ngumu sababu ya mfumo wa pembe tatu. Ninaamini tumeumbwa tofauti, lakini through friends ndipo unaweza gundua kile ambacho Mungu ameweka kwenye Maisha yako pia. Aliyenipa wazo la kuwa na Blog is my friend Weda Ringo..she saws something in me akasema Papaa you Can do It, but wote hatukujua on "how to do" kwenye Nia pana njia, leo hii Blog imesimama, Blog imekuwa chanzo changu cha fedha, Blog imekuwa Msaada kwa Watanzania wenzangu na Ulimwengu kwa Ujumla. Blog imekuwa madhabahu ya wengine kufunguliwa. Nilipoanza Blog sikujua kama nitakuwa na "Papaa On Tuesday" lakini Mungu akawapa akaweke idea ya mimi kuwa na "Papaa On Tuesday", leo kuna wazo lingine ninalo ambalo pia litabadilisha mtazamo wa Blog hii, siangalii leo, wala mwaka huu ninatazama miaka mitano ijayo.Na kile Mungu anasema kuhusu Blog hii.This will be the most Popular Christian Blog hapa Tanzania si kwa sababu ya mapicha picha au sababu ya uandishi I came to realise this blog is not mine, last week nimepokea testmony za kutrosha mpaka nikaogopa kuwa kupitia Blog hii kuna watu wamepona kabisaaaaaa magonjwa yao, kuna watu wanainuliwa kupitia blog hii, kuna watu wanasubiri Jumanne Kusoma Papaa On Tuesday sababu anajua kuna Kitu kutoka Madhabahu hii. Nimejifunza kumsikiliza aliyeniajiri katika kazi hii na kuweka hizi idea na gifts ndani yangu anataka twende wapi kupitia blog. Is not only about writings lakini how many people wamekuwa transformed wamekuwa inspired kupitia hapa, we need to live a life with impact.
Lakini haya yote is not all about me kuna watu wananiombea kuna watu wananipa Ideas. Let me be Honesty Mwanzo ni mgumu sana, na kuna watu wanapenda wengine wafanye wao wanavyodhani ni vizuri, nimekutana na watu wengi sana wanatamani Blog yangu ile kivileeeeeeeee, wengine wanaongea rangi mbaya, wengine wanaongea lugha ninayotumia, wengine wanaongea kuna picha nyingiiiii, the simplest thing that I always do, ninasikiliza then ninachambua kina go ahead ya ndani ama lah kama sio napiga chini wazo kama unaona unaweza anzisha Blog yako iwe inavyotaka kuwa, usikate tamaa kwenye maisha huwezi jua nini kitakutoa kwenye maisha yako.
Ukiona mwezi mzima unamaisha ya pembetatu tafakari kisha chukua hatua. Kila siku ya Mungu lazima nikutane na watu kwa ajili ya kubadilishana mawazo na kila siku ninapata mawazo mapya kupitia watu kupitia vitabu mbalimbali.
Think
Differently and Make a Difference.
...//Papaa
0713 494110
samuel_sasali@yahoo.com
posted by 0718817706
...//Papaa
0713 494110
samuel_sasali@yahoo.com
posted by 0718817706
Thursday, August 23, 2012
Ustaarabu kwa tafsiri yetu...
Subscribe to:
Posts (Atom)











