Tafuta/Search This Blog

Thursday, April 25, 2013

One beautiful evening around lake Victoria...

MV Victoria Loading, ready for Bukoba voyage

Sunsetting


Was just chilling on the shores of Lake victoria, Mwanza.

Wednesday, April 17, 2013

Wednesday, April 10, 2013

Samaritan's Purse at Kigogo TAG last Sunday

 Watoto wakiangalia zawadi zao
 Wanachekelea kwa furaha
 Mabox yenyewe
 Solomon naye alikuepo
Zawadi hizi zinatoka Marekani kwa watoto wa huko kuja kwa watoto wa Tanzania....

Friday, April 5, 2013

RAINBOW IN MWANZA

View from Isamilo

Kiseke PPF.

Please acknowledge this blog when using the pictures in anyway!

Hii nzuri sana...


Leo asubuhi. Ni msimu wa mvua hapa Mwanza na leo asubuhi kulikuwa na mvua kidogo mawingu yalikuwa yametanda upande mmoja wa anga na kuacha nafasi kidogo ya miale ya jua kupenya na kumulika visiwa vilivyopo kwenye ziwa Victoria na kuleta rangi nzuri sana ya dhahabu kama inavyoonekana! Ilibidi tu nipige picha hii kwa kutumia simu yangu ya mkononi maana hii ni taswira adimu na adhimu sana. #Beautiful Mwanza.
Jamani picha yangu hii, itumie kwa ruhusa yangu basi.


Tuesday, March 26, 2013

Ni kweli huwa simba anazaa wakati huu??

Mvua kubwa ya jioni wakati jua bado linawaka sana.

Hapa ni KVCC Mwanza.

Tangu nikiwa mdogo, nimekuwa nikisikia kwamba ukiona mvua inanyesha na jua linawaka ujue Simba anazaa.Juzi nikakutana na hili tukio tena lakini hii ya juzi mvua ilikuwa kubwa sana wakati jua linawaka. Kuna mtu anajua ukweli wowote??
Ila cha msingi ni kwamba msimu wa mvua umeanza!

Wednesday, March 20, 2013

Salma Cone Mwanza hapa...

Kijiwe maarufu sana jijini Mwanza kwa mambo ya Ice Cream, Kuku wekundu, Mishkaki, chipsi na mazagazaga yote ya tumboni. Jioni huwa panakuwa busy sana. Makao makuu ya klabu ya mpira wa miguu ya Toto Africans yapo karibu sana na hapa.

Sunday, March 17, 2013

Please Vote for our very own doctor Naiz!


Dear Friends and colleagues,
Please vote for me, I applied for grants in grand challenge Canada with an Idea of setting up a local RHD control program in lake zone/Mwanza, kindly follow the link below which will direct you to vote.Thank you very much for your assistance on this.Please help me by telling others too.

Naiz
Pediatric Cardiology Fellow
Wolfson-Israel




Saturday, March 16, 2013

Mdogo wetu Maria Mtili ametunukiwa Diploma ya Teknolojia ya Mawasiliano (IT)

Mwaka umeanza na shangwe pia zimeshaanza. Mdogo wetu hatimaye amefanikiwa kumaliza masomo yake na kutunikiwa diploma katika taasisi ya IIT hapo Dar Es Salaam. Hizi ndio picha za tukio.


Pozi la kisomi.


Mdada.

Mama na binti yake.


Mfanano, kama mtu na dada yake.


Fullu tabasamu...



Hongera dada.



...Na hasa kama una akili...


Zaidi ya diploma binti huyu pia alipata tuzo kadhaa kwa kuwa mkali sana darasani.





Tunakupongeza sana mdogo wetu na tunakuombea heri ili uende mbele na mbali zaidi.
Hongera nyingi kutoka kwa kaka mkubwa Godlove.