Tafuta/Search This Blog

Tuesday, June 23, 2015

Muhimbili yazichachafya taasisi za Serikali 84 Wiki ya Utumishi wa Umma

Muhimbili yazichachafya taasisi za Serikali 84 Wiki ya Utumishi wa Umma
·        Yaongoza kwa tuzo ya Ubunifu (Kangaroo) na Banda Bora
Na. Aminiel Aligaesha (MNH)
Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) imezichachafya taasisi 84 zilizoshiriki maonyesho ya wiki ya Utumishi wa Umma kwa kutwaa tuzo mbili kati ya tano maalum zikiashiria kuwa mshindi wa kwanza kwa kila tuzo. Tuzo ya kwanza ni ya ubunifu katika kutoa huduma iliyokuwa ikitaka taasisi kuwa na ubunifu ama wa kuiga (adoption) au asili (origin) na ambao haujawahi kufanyika hapa nchini na ubunifu huo uwe umeleta tija katika utoaji huduma eneo la kazi.
 
Katika tuzo hii MNH imeshinda kwa kubuni njia mbadala ya kulea watoto waliozaliwa kabla ya wakati (njiti) kupitia njia ya KANGAROO.  Ubunifu huu uliigwa kutoka nchi za  Afrika Magharibi na Afrika ya Kusini ambao walifanya utafiti kwa kumsoma KANGAROO anavyolea watoto wake akiwa amewakumbatia na kuonyesha mafanikio makubwa. Kwa misingi hiyo walionekana kufaulu ambapo vifo vya watoto waliozaliwa  kabla ya wakati vilipungua ukilinganisha na wale wanaolelewa kwenye incubators. MNH ilianza mpango huu mwaka 2002 na tayari umeonyesha mafanikio makubwa sana ambapo tayari Hospitali ya Lutheran Hydom iliyoko Arusha nayo imefundishwa na watalaam wetu kutumia njia hii nayo ikafanikiwa.
 
Tuzo ya pili iliyonyakuliwa na MNH ni tuzo ya banda bora kuliko yote wakati wa maonyesho ambayo vigezo vyake pamoja na mambo vigezo vingine ni uwezo wa washiriki husika kujua taaluma yao, uwezo wa kuelezea huduma zinazotolewa na taasisi wanayofanyia kazi, unadhifu katika banda na huduma bora kwa wateja.
 
Maonyesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yalijumuisha taasisi 84  zilishiriki kushindania tuzo nne ambazo ni (Tuzo ya Ubunifu, Tuzo ya Taasisi/Wizara Inayosimamamiwa kwa Mjibu wa Utawala Bora, Tuzo ya Uwezeshaji Akina Mama, Tuzo ya Mpango wa Wafanyakazi Wanaoishi na VVU Mahali pa kazi.  Aidha kati ya taasisi hizo ni taasisi 42 ambazo zilishindanishwa kwenye Tuzo ya Tano ya Banda Bora.
 
Kwa misingi hiyo, MNH imezigaraza taasisi 42 zilizojitokeza kugombea nafasi hiyo ikiziongoza ambapo tuzo hutolewa kwa washindi wa kwanza hadi wa tatu. Aidha MNH imeziongoza pia 84 kwenye nafasi ya kwanza kwenye tuzo ya ubunifu. Hii inadhihirisha MNH ipo juu taasisi hizi haziiwezi, haikamatiki. Katika tuzo ya  Taasisi/Wizara Inayosimamamiwa kwa Mjibu wa Utawala Bora, MNH imepata nafasi ya 8 kwani kila tuzo imetoa fursa angalu ya kutambua taasisi 10.  
Fuatilia habari katika picha:  
Dkt. Bashir Nyangasa, Daktari Bingwa wa Upasuaji Moyo akifurahi baada ya kukabidhiwa tuzo ya Ubunifu
Baada ya kupata tuzo mbili. Kutoka kushoto ni muuguzi kutoka chumba maalum cha kujifungulia Anna Danfold ambaye alikuwa akielezea dakika ya dhahabu ya kuokoa maisha ya mtoto mara tu anapozaliwa. Anayefuatia ni Muuguzi Rose Silaa ambaye ni Mkuu wa Kitengo cha Utunzaji wa Watoto kwa Njia ya Kangaroo akionyesha mtoto anavyotunzwa kwa njia hiyo.
Wakashindwa kuzuia furaha zao hapa Washiriki wa MNH wakasakata dansi baada ya kupokea tuzo mbili
Wakapata picha ya pamoja kabla ya kuelekea Muhimbili kukabidhi kikombe kwa Mkurugenzi Mtendaji wao aliyewatuma
Wakawasili Muhimbili kwa mbwembwe
Juu na chini ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili akipokea vikombe kutoka washiriki wa maonyesho. Juu ni Muuguzi Nemganga Kizegha na chini Dkt. Bashir Nyangasa
Msitari wa mbele ni baadhi ya Wakurugenzi wa MNH kwa pamoja wakiwa na nyuso za furaha katika picha ya pamoja na baadhi ya washiriki
Mkurugenzi wa Teknohama Bw. Modou Gaye akipokea tuzo hizo na kuyaweka Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili

Friday, January 10, 2014

Friday, November 1, 2013

Kanisa la Mt. Cecilia BUJORA

Najua umewahi kuona makanisa mengi hapa africa ambayo mara zote yamekuwa yakijifananisha na tamaduni za ulaya kutokana na historia ya kanisa ilivyo. Makanisa yote yamekuwa yakijengwa kufananishwa na jinsi makanisa ya KIZUNGU yalivyo na kuitwa majina ya huko yalipoanzia na pia kuwaonesha Yesu na mitume wake kama wazungu n.k

Sasa, kuna kanisa lipo Bujora Mwanza. Hili ni la kipekee! Lilijengwa na mzungu lakini kini limejengwa kwa kufuata tamaduni za kisukuma. Kuanzia jengo na vitu vilivyomo ndani na hata sanamu ndani ni za sura za kiAfrica pamoja na Yesu mwafrica. Inapendeza sana jinsi ambavyo jamii hii ya wasukuma ilivyofikiwa na hawa wamishionari. Hebu jionee mwenyewe hizi picha za kanisa hilo.

Hili ndio jengo la kanisa, na hivi ndivyo wasukuma walivyojenga nyumba zao.

Yesu wa kisukuma!



Madhabahu ambayo imefananishwa na pembe ya ng'ombe. Pembe ilitumuka na wasukuma kuwaita kwenye vikao.


ndani.

Sanamu ya bikira Maria wa kisukuma.angalia hata nywele zimesukwa mtindo wa "twende kilioni"

Viti vya watumishi. Hivi ndio viti vya asili vya wasukuma. Pembeni ni mtungi wa maji kwa ajili ya kubatizia.

Viti vya viongozi. Angalia jinsi rangi zilivyopamba ukuta!


Kinanda cha kwaya.
Kaka Godlove ndani ya kanisa.

Unaweza ukatembelea kanisa hili ambalo lipo Bujora Sukuma Museum, Magu mkoani Mwanza.

Monday, October 28, 2013

KONGAMANO KUBWA LA UAMSHO NA MAOMBEZI



Kanisa la T.A.G Kigogo Mburahati Limekuandalia Kongamano kubwa la UAMSHO NA MAOMBEZI.

Tarehe: 28 Oct. hadi 3 Nov 2013

Muda: Saa 10:00 – 12:00 Jioni

Wahudumu: Askofu Laurence Kameta, Mch. Sir Gilbert, Mwinjilisti Crispin Madembwe pamoja na
Mch. Sabinus Mbogo.

Kwaya zitakazo hudumu ni Kinondoni Revival, Peace Maker Ilala na Wenyeji T.A.G Kigogo kwaya waimbaji binafsi watakao hudumu ni Lyanga George na Sara Shira.

Wenye shida mbalimbali kama Matatizo ya ndoa, Magonjwa, waliofungwa na Mapepo na matatizo mengine yote YESU MTENDA MIUJIZA ATAYASHUGHULIKIA! NJOO UKUTANE NA MUNGU!

Kanisa liko karibu na Kituo cha Mburahati msikitini mita chache sana kuelekea barabara ya barafu.

Kwa mawasiliano 0754 995 590 au 0712 554 528

Hatimaye Papaa Samuel Sasali a.k.a the Blogger ameoa!

Jana, tarehe 26 Oktobe ilikuwa siku ya kihistoria sana katika ngome ya mabachela nchini Tanzania baada ya bachela Nguli kujiondoa rasmi kwenye hilo kundi na kujiunga kwenye klabu ya waliooa! Sisi SBP tunawapongeza sana Sam na Mirembe kwa hatua hii na tunawatakia maisha mema ya ndoa

Smiles all over! Samuel na mke wake Mirembe.
Mambo haya yasingekosekana asilani!!


Ukweliii1



Hii picha muhimu sana! Nahisi Papaa alikuwa anamkabidhi rafiki yake Prosper Kijiti na kuweka msisitizo!

Mr&Mrs Sasali wakisindikizwa na Mr&Mrs Mndeme.

Picha zote zimetolewa Facebook page ya MC LUVANDA

Sunday, October 27, 2013

Sikiliza kuhusu daktari aliyejitolea maisha kuokoa wahanga wa ubakaji!

Denis Mukwege, daktari bingwa wa magonjwa ya wanawake kwa zaidi ya takribani miaka 15 amejitolea maisha yake kuokoa wahanga wa ubakaji huko mashariki mwa Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo, DRC. Akihudumia kwenye hospitali ya Panzi huko Bukavu, hospitali aliyoianzisha mwaka 1993, Dkt. Mukwege na wenzake wametoa usaidizi wa kitabibu kwa maelfu ya wanawake waliokumbwa na wanaoendelea kukumbwa na madhila ya ubakaji. Katika makala hii, Joseph Msami alipata fursa kuzungumza na Dokta Mukwege ambaye alifika makao makuu ya Umoja wa Mataifa kwa mazungumzo na Katibu Mkuu Ban Ki-Moon. Katika mazunguzo na Msami, Dokta Mukwege walijadili mengi ikiwemo alivyonusurika kuuawa mwaka mmoja uliopita.