Tafuta/Search This Blog

Monday, June 27, 2016

Friday, June 24, 2016

Kiingereza, Kidhungu hiki!!


Eti wengine wanasemaga hii lugha ni Janga la taifa, wengine wanasema hii lugha ni kipawa ambacho mtu inampasa atunikiwe na Muumba.

wewe Unasemaje??

Ila hii lugha imekuja na meli jamani, tuwe makini tusiharibu vya kwao! si tumie kiswahili chetu tu!!

Mbwa wa kwetu wanalala juu ya Ukuta.


Hii aina ya Mbwa sijui inaitwa nini jamani. mapumziko yao juu ya ukuta. Karibu kwetu.

Tuesday, June 21, 2016

In love with nature!

Whether you like it or not but for sure God is the greatest artist ever! Wondering how he planned and orchestrated everything it is so amazing/

Enjoy these shots from Mwanza Tanzania;








Psalm 8:1 
Lord, our Lord,
    how majestic is your name in all the earth!
You have set your glory
    in the heavens.
Through the praise of children and infants
    you have established a stronghold against your enemies,
    to silence the foe and the avenger.
When I consider your heavens,
    the work of your fingers,
the moon and the stars,
    which you have set in place,

Hey, we are back - Tumerudi!!!

Hello good people!!

It has been so long!! Tumekuwa na mambo mengi, tumekutanan na mengi na tumewakosa sana, we missed you alot! 

We have grown! tume kuwa wakubwa sana sasa, tuna familia na wote tunendelea vyema. Sasa tumeamua tena kurudi kwenye huu ulimwengu wa blogging! Na we are coming back so strong!

Where and how do we start that is the challenge but we are ready to face that. We will be coming from Dar es Salaam and Mwanza Tanzania but also from wherever we will be at that particular time.

So welcome back and stay here with us.

Please share your memories and we will post!

our addresses; godlovegordon@gmail.com and enson79@yahoo.co.uk are still on.

Whatsapp; +255756025428 and +255784494906

Lets roll!!!

Tuesday, June 23, 2015

Muhimbili yazichachafya taasisi za Serikali 84 Wiki ya Utumishi wa Umma

Muhimbili yazichachafya taasisi za Serikali 84 Wiki ya Utumishi wa Umma
·        Yaongoza kwa tuzo ya Ubunifu (Kangaroo) na Banda Bora
Na. Aminiel Aligaesha (MNH)
Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) imezichachafya taasisi 84 zilizoshiriki maonyesho ya wiki ya Utumishi wa Umma kwa kutwaa tuzo mbili kati ya tano maalum zikiashiria kuwa mshindi wa kwanza kwa kila tuzo. Tuzo ya kwanza ni ya ubunifu katika kutoa huduma iliyokuwa ikitaka taasisi kuwa na ubunifu ama wa kuiga (adoption) au asili (origin) na ambao haujawahi kufanyika hapa nchini na ubunifu huo uwe umeleta tija katika utoaji huduma eneo la kazi.
 
Katika tuzo hii MNH imeshinda kwa kubuni njia mbadala ya kulea watoto waliozaliwa kabla ya wakati (njiti) kupitia njia ya KANGAROO.  Ubunifu huu uliigwa kutoka nchi za  Afrika Magharibi na Afrika ya Kusini ambao walifanya utafiti kwa kumsoma KANGAROO anavyolea watoto wake akiwa amewakumbatia na kuonyesha mafanikio makubwa. Kwa misingi hiyo walionekana kufaulu ambapo vifo vya watoto waliozaliwa  kabla ya wakati vilipungua ukilinganisha na wale wanaolelewa kwenye incubators. MNH ilianza mpango huu mwaka 2002 na tayari umeonyesha mafanikio makubwa sana ambapo tayari Hospitali ya Lutheran Hydom iliyoko Arusha nayo imefundishwa na watalaam wetu kutumia njia hii nayo ikafanikiwa.
 
Tuzo ya pili iliyonyakuliwa na MNH ni tuzo ya banda bora kuliko yote wakati wa maonyesho ambayo vigezo vyake pamoja na mambo vigezo vingine ni uwezo wa washiriki husika kujua taaluma yao, uwezo wa kuelezea huduma zinazotolewa na taasisi wanayofanyia kazi, unadhifu katika banda na huduma bora kwa wateja.
 
Maonyesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yalijumuisha taasisi 84  zilishiriki kushindania tuzo nne ambazo ni (Tuzo ya Ubunifu, Tuzo ya Taasisi/Wizara Inayosimamamiwa kwa Mjibu wa Utawala Bora, Tuzo ya Uwezeshaji Akina Mama, Tuzo ya Mpango wa Wafanyakazi Wanaoishi na VVU Mahali pa kazi.  Aidha kati ya taasisi hizo ni taasisi 42 ambazo zilishindanishwa kwenye Tuzo ya Tano ya Banda Bora.
 
Kwa misingi hiyo, MNH imezigaraza taasisi 42 zilizojitokeza kugombea nafasi hiyo ikiziongoza ambapo tuzo hutolewa kwa washindi wa kwanza hadi wa tatu. Aidha MNH imeziongoza pia 84 kwenye nafasi ya kwanza kwenye tuzo ya ubunifu. Hii inadhihirisha MNH ipo juu taasisi hizi haziiwezi, haikamatiki. Katika tuzo ya  Taasisi/Wizara Inayosimamamiwa kwa Mjibu wa Utawala Bora, MNH imepata nafasi ya 8 kwani kila tuzo imetoa fursa angalu ya kutambua taasisi 10.  
Fuatilia habari katika picha:  
Dkt. Bashir Nyangasa, Daktari Bingwa wa Upasuaji Moyo akifurahi baada ya kukabidhiwa tuzo ya Ubunifu
Baada ya kupata tuzo mbili. Kutoka kushoto ni muuguzi kutoka chumba maalum cha kujifungulia Anna Danfold ambaye alikuwa akielezea dakika ya dhahabu ya kuokoa maisha ya mtoto mara tu anapozaliwa. Anayefuatia ni Muuguzi Rose Silaa ambaye ni Mkuu wa Kitengo cha Utunzaji wa Watoto kwa Njia ya Kangaroo akionyesha mtoto anavyotunzwa kwa njia hiyo.
Wakashindwa kuzuia furaha zao hapa Washiriki wa MNH wakasakata dansi baada ya kupokea tuzo mbili
Wakapata picha ya pamoja kabla ya kuelekea Muhimbili kukabidhi kikombe kwa Mkurugenzi Mtendaji wao aliyewatuma
Wakawasili Muhimbili kwa mbwembwe
Juu na chini ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili akipokea vikombe kutoka washiriki wa maonyesho. Juu ni Muuguzi Nemganga Kizegha na chini Dkt. Bashir Nyangasa
Msitari wa mbele ni baadhi ya Wakurugenzi wa MNH kwa pamoja wakiwa na nyuso za furaha katika picha ya pamoja na baadhi ya washiriki
Mkurugenzi wa Teknohama Bw. Modou Gaye akipokea tuzo hizo na kuyaweka Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili

Friday, January 10, 2014