Haya tunarudi Mwanza na hapa ni Mwanza International Fish Market Mwaloni.
Hayo ndio yaliyojiri huko kisiwani.
Haya ndio mambo ambayo unahitaji kuyafahamu kuhusu Ukerewe.
- Kisiwa cha ukerewe kina ukubwa wa kilomita za mraba 530.
- Ukerewe kama wilaya inaundwa pia na visiwa vidogo vidogo 38.
- Kutoka Mwanza hadi ukerewe ni umbali wa kama kilometa 45 ila vyombo vilivyopo vinatumia takribani masaa manne kusafiri umbali huo.
- Inasemekana kisiwa hiki kimezalisha wasomi wengi sana hapa Tanzania. Kwa taarifa ambazo nimepewa na mtu (sio lazima uamini na mimi sina jinsi ya kuzidhibitisha) kisiwa hiki kimetoa maprofesa 70.
- Hiki ndio kisiwa kikubwa zaidi kilichopo ndani ya bara Africa. (inland island)
- Kuna Matatizo mengi sana ya ardhi kwenye kisiwa hiki hadi inaonekana kama watu ni wengi kuliko ukubwa wa kisiwa.
- Kama kuna lingine unalifahamu unaweza ukalituma ili tulifahamu.
Plan to visit Ukerewe, you wont regret.
|
No comments:
Post a Comment