Kwa mara ya kwanza Siku ya ya Baba wa Taifa la Tanzania,
Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere itaadhimishwa makao makuu ya Umoja wa
Mataifa tarehe 14 mwezi huu. Shughuli hii imeandaliwa na ubalozi wa Tanzania
katika Umoja wa Mataifa ambapo mwandishi wa idhaa ya Kiswahili ya radio ya Umoja
wa Mataifa Joseph Msami, amefanya mahojiano na Mwakilishi wa Tanzania wake
wa kudumu katika UM Balozi Tuvako Manongi na ameanza kwa
kumuuliza ninini umuhimu wa siku hiyo?
Shughuli hiyo itaenda sambamba na uzinduzi wa kitabu
kiitwacho JULIUS
NYERERE: Jabali wa Afrika katika medani za kimataifa
kilichohaririwa kwa pamoja na Profesa Ali Mazrui na Dokta Linda Mhando. Hayati
Mwalimu Nyerere alifariki dunia tarehe 14 Oktoba mwaka 1999 nchini Uingereza
kutokana na ugonjwa wa saratani ya damu.
Msami akimhoji balozi Manongi |
No comments:
Post a Comment