Kwa
mara nyingine tunaendelea na mfululizo wa makala za kudadavua dhana ya
uzalendo na wajibu wetu kwa nchi na yetu Tanzania, ambae kupitia maziwa
tuliyonyonya na misingi aliyotujengea, leo hii tunaweza kujumuika na
wanadunia wengine kupitia teknolojia ya habari na mawasiliano.
Leo,
hii tuangalie dhana ya wajibu wetu kwa nchi yetu ni nini hususan,
katika wakati huu wa mpito wa mageuzi ya kiuchumi na kiutawala mara
baada ya kuingia madarakani mzawa wa chato na mbobezi wa kemia na
hisabai Rais John Magufuli.
Viktor
Frankl ni mtafiti wa wa tabia za wanadam kutafuta furaha (pursuit of
happiness) na kupitia majarida kadha wa kadha ame-eleza kwa ufasaha
ramani au michoro katika akili ya mwanadamu. Mtafiti huyu ameweka wazi
namna akili inaweza kuendelezwa na kumfanya mtu kuwa na kitabia ya aina
flani. Na tabia hiyo huwa ni mfumo wa maisha ya watu na hali kadhalika
katika jamii husika.
Mathalani,
jamii za Korea, Japan hata Malaysia mtu akishindwa kutimiza azma yake
ya kutoa mchango kwa maendeleo ya jamii, huishia kujua. Wengi hujiua kwa
kushindwa kukubaliana na uhalisia wa nje kama vile kufilisika,
kuachishwa kazi ghafla hasa kama ulikuwa ni wadhifa mkubwa serikalini au
kampuni za sekta binafsi. Tabia hii ilikuwa dhahiri sana nyakati za
anguko la kiuchumi duniani ambalo pia liliathiri uchumi wa nchi hizo na
makampuni yao kibiashara.
Kwa
upande mwingine, mtafiti Frankil alikusudia kutufunulia na kutujuza
matokeo ya kitabia ili kupata tija ya hali ya juu (highly effective)
kutoka kwa mtu katika mazingira yoyote yale. Tija katika muktadha huu ni
uwezo wa kuona na jicho la kutafuta jibu au suluhisho katika mazingira
magumu au wakati tete katika jamii.
Kwa
maana nyingine, “jicho la tatu” laweza kuitwa “proactivity”. Proactive
kwa tafsiri rahisi ni hali ya kuwa na fikra ya kuanzisha jambo lenye
kutatua tatizo linaloinzunguka jamii au nchi ya mhusika.
Dhana
inayojengwa na inayotazamwa ni hali ya kumtaka mwanadamu kunawajibika
na maisha yake kwa kuyakabili mazingira au changamoto za mazingira
yanayomzunguka. Tukumbuke, tabia ya kila mwanadamu ni mwitikio wa
maamuazi (behavior is a function of decision of an individual). Ni namga
gani mtu anayakabili mazingira au hali inayomzunguka.
Tanzania
inapitia katika changamoto ya kimtazamo na kifikra tokea Rais John
Magufuli achukue hatamu ya kutuongoza. Rais Magufuli amekuja na mfumo
wake wa kudhibiti matumizi ya serikali na kuziba mianya ya “kupiga dili”
ndani ya serikali na katika sekta binafsi; ambayo ilikuwepo kupitia
mambo kadha wa kadha kama wafanyakazi hewa, wanafunzi hewa ambao
walipelekea malipo hewa kupigwa na wezi wachache.
Kufuatia
kusudio lake la kusimika mfumo mpya, kuna namna baadhi ya shughuli za
kibiashara zimeathirika kutegemea na misingi ya wenye biashara
walivyokuwa wamejenga mifumo yao ya kuziendesha.
Tukichukua
wajibu wetu ili kujipanga upya namna ya kuendana na mfumo mpya wa awamu
ya tano, tunawajibika kuamua namna ya kufanya biashara kwa kuzingatia
misingi halali ya kulipa kodi na kufuata sheria na msingi ya kufanya
kibiashara ili kukidhi uhitaji wa soko au walaji.
Pengine,
tupate maana ya neno wajibu. Wajibu lilitokana na neno la kingereza
responsibility -- "response-ability" – nguvu ya mwitikio au uwezo na
maamuzi ya kuchagua kutenda ikisukumwa na nguvu iliyo ndani ya mtu. Huo
ndiyo wajibu au kuwajibika.
Hivyo
basi, wajibu ni mwitikio na uwezo na kufanya maamuzi kuyatawala au
kuyadhibiti mazingira, au kulia na kulalama dhidi ya hali iliyopo. Kama
tunakumbuka, Rais Obama wakati ameingia madarakani mwaka 2009, Marekani
na dunia ilikuwa na anguko kubwa la kiuchumi (global economic crisis).
Obama na wenzie hawakulia na kumlaumu Bush na kukumbuka miaka nane ya
Bill Clinton uchumi ulikuwa mzuri, walitimiza wajibu wao wa kujipanga na
kujenga mfumo mpya na leo hii uchumi wa Marekani umeimarika tofauti na
miaka 8 iliyopita.
Itaendelea…
No comments:
Post a Comment