Tafuta/Search This Blog

Thursday, November 13, 2008

Sisi kwa kumodifai!!

Yaani sisi wa TZ kutengeneza vitu vipya inaweza ikawa ngumu sana, lakini kwa kurekebisha walivyotengeneza wajapani.... sisi nooooma!! Hebu ona hii, nimeikuta kwenye blogu ya SUMO.

picture by http://mpoki.blogspot.com/

Msiba Kibosho

Mpendwa wetu na kaka yetu Erasmus Joseph Mmasi amefiwa na mama yake mzazi na mazishi yameanyika leo mchana huko Kibosho.

Kwa niaba ya wamiliki woote wa SBP tunapenda kutoa salamu zetu za pole kwa kaka Erasmus pamoja na familia yote ya Mmasi kwa msiba huu mkubwa uliowapata.

Mungu wa amani awakumbatie.

Tuesday, November 11, 2008

Nionvyo mimi.

Huyu hapa Obama, wengine wanasema Mtanzania, wengine eti mchaga kabisa (Obamaeli) ila mimi naona anafanana na Kikwete. Angalia vizuri wakicheka.

Huyu ni Kikwete, naona pia ukimtazama haraka haraka ni kama Obama vile. Hebu toa maoni hapo, wewe unawafananishaje?

Sunday, November 9, 2008

Weekend iliyopita

Naamini wadau woote kabisa mko fit na mnaendelea vyema na shughuli zenu za kila siku.
Weekend iliyopita nilikwenda kumsalimu babu yetu huko katika milima ya ugweno. Nilipiga picha kidogo ambazo naona itakuwa vyema na ninyi mkaziona.

Mlima Kilimanjaro unavoonekana ukiwa maeneo ya Bomang'ombe.


Huyo kijana wa katikati ndio mjanja wa kijijini, anaitwa Eliamani au Godlove G. Temba ni mtoto wa Uncle wetu anayeitwa Goodluck.


Nilipenda sana hili pozi la hawa marafiki wawili niliowakuta nyumbani kwa babu yangu. Yani huyo Mbwa hana noma kabisa akiwa na huyu Paka kiasi kwamba kuna wakati utakuta wanapiga stori zao na hakuna tatizo kabisa. Hapa walikuwa wameshiba na wanaanza kupata kausingizi ka mchana!!

Nice time wadau...


Friday, October 31, 2008

Abel na Josephine wanang'aa!!

Hatimaye yule senior Bachelor wa Tanzania Meteorological Agency intake ya 2002 ndugu Abel Nyamenda alichukua uamuzi wa kujisogezea kipenzi chake karibu naye kwa kufunga ndoa takatifu na dada Josephine Mwakang'ata huko Mbeya tarehe 4 mwezi wa 10 mwaka huu.


Mr&Mrs Nyamenda!!

Msafara katika mchuma wa ukweli!!

Mapozi ya Mrs Nyamenda haya!!

Mmmmhhhhhh!!! Sina nyongeza, jionee mwenyewe!!!!!





Mashahidi



Sisi Shalom Broz tunawatakia Mr&Mrs Nyamenda maisha mema na ya baraka. Kuna ukweli ambao bado hatujauthibitisha lakini tunauamini kwamba mtu akioa milango yake ya mafanikio hufunguka zaidi!! Kazi kwako kaka Abel!!
Tunasubiri ubwabwa wa kaka Sanga.