Tafuta/Search This Blog

Monday, May 24, 2010

Be careful!...you are in ARUSHA

Nitaonekana kama ninapenda sana kuwasakama viongozi wa jiji letu la Arusha kwa kuandika haya ninayoandika, lakini huu ndio ukweli kwamba hawa wenzetu wamejisahau sana kwamba wanatakiwa kutimiza wajibu wao! Nilipokuwa natembea mjini jana nilipiga picha hizi ili ndugu zangu muone na wao kama watapata nafasi ya kuangalia waone. Natamani sana kama siku moja kiongozi yeyote wa hili jiji letu atanitafuta ili nimwambie vile ninahasira. Jamani kama mnawafahamu hebu waambieni kwamba mimi ninawasakama huku!!

Hapa ni katika barabara ya sokoine karibu na Metropole. Hili lipo tangu alhamisi... Ila nimependa huu ubunifu wa kuweka miti!!







Sasa haya mashimoyaliyowazi ni mengi sana hapa Geneva yetu. Sijui ni kwa sababu wenzetu wanapita huku barabarani na magari kwa hiyo haya hayawahusu?? Haya yako wazi kwa enzi!! Kuna siku mzee moja alitumbukiza mguu humu ndani ya shimo kuteguka! Jamani sina la kusema ila kama unakuja Arusha uje umejiopanga la sivyo ziara yako itaishia kwenye mashimo ya jiji!!

Thursday, May 20, 2010

Angalia kwa makini alafu sema kitu.

Pumzi.... Naamini ni Mazoezi kupata punzi na kuwa na HDD kubwa ya storage na ubunifu wa kuficha ukweli. It is possible...

Monday, May 17, 2010

Best Mom

Unaujua upendo wa Mama?
Ni kama huu..

Hata wakali wanaupendo..



Na zaidi ya Upendo



Hata kuwalinda kwa kiasi hiki...

Friday, May 14, 2010

Maisha BORA kwa kila Mtanzania

Makazi haya ni ya Mtanzania wa kawaida ambaye ukimuona huku town kamwe huwezi kubaini kama wazee ndio wanaishi hapa. Mtanzania wa kawaida ni yule anayepata milo miwili hadi mitatu kwa siku.
Ugali wa ndizi tulioandaliwa wageni WAHESHIMA tulipotembelea makazi ya watanzania hawa wa kawaida.


Kwa mbaaaaali ile ni sitting room

Tuesday, May 11, 2010

Saturday, May 8, 2010

Ukitaka kuishi Dar Es Salaam lazima ugangamale!!

Haya ni mambo muhimu ya kuzingatia....

Uwe tayari kutembea kwa miguu wakati daladala zipo... mambo ya foleni! (Misuli iwe ya ukweli)


Hata kama una gari hakikisha umelifanyia matengenezo ya kuliwekea engine ya boat...maana katikati ya barabara kuna mabwawa ya kufugia samaki wa serikali!!



Uwe tayari kuvunja sheria. wakati mwingine itakupasa kupanda daladala kwa kupitia mlango wa dereva!!
Upo tayari kuhamia Dar es salaam?? Kama bado anza mazoezi au vipi achana kabisa na wazo hilo!

Jamani Moshi pasafi!!

Sina haja ya kuongea sana, lakini kwa kweli mjii huu nahisi una watendaji wanaofanya kazi. Pokeeni pongezi nyingi sana kutoka kwetu.
Lakini ajabu yake, kilometa 80 tu kutoka moshi kuna mji wa kitalii unaoitwa Arusha, kwa masikitiko kabisa mji huo ni mchafu. Hivi watu hawawezi hata kuiga tu au wanafikiria usafi ni mtihani kwamba wakiiga watafutiwa matokeo!! Inanikera sana!!

Hongera sana mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro, na hongera sana viongozi wooote wa manispaa ya Moshi, pongezi nyingi pia kwa migambo woooote wa manispaa hii na tunawakaribisha sana Arusha!!

Wednesday, May 5, 2010

Thursday, April 29, 2010

Banda la Mambo ya Tume ya Nguvu za ATOMIC Tanzania Atomic Energy Commission

Nilivutiwa sana na maonesho katika Banda hili, hata nikaomba mwelimishaji anipige picha.
Wanashughulika sana na mionzi kama ilivyo ya Urani.

Athari za muda mfupi kwa atakyegusa mionzi kama ya Uraniam



Mwelimishaji aliniambia kuwa mpaka kuweza kutengeneza umeme hapa tanzania, inaweza kuchukua hata miaka kumi au zaidi. Hivyo tuna safari ndefu.