


Mtumishi wa Mungu Fanueli Sedekia ambaye alifariki dunia wiki 2 zilizopita huko Israel na kuzikwa hapa Arusha wiki iliyopita amenifundisha kitu kikubwa sana katika kumtumikia Mungu.
Katika Neno la Mungu tunaambiwa kwamba ukimtumikia Mungu utaheshimika. hili limekuwa dhahiri katika mazishi ya huyu ndugu. Watu kutoka maeneo yote ya Arusha, mikoa mbali mbali ya Tanzania pamoja na baadhi ya nchi walihudhuria.
Sedekia alimtumikia Mungu bila ya kuchagua jina la kanisa wala ukubwa au udogo wake. alikuwa tayari kumtumikia Mungu popote alipokuwa tena kwa moyo mkunjufu kabisa. Namshukuru Mungu kwamba niliwahi kupiga muziki pamoja naye katika siku za mwisho za uhai wake hapa Arusha na haya ninayoandika nimeyahahakikisha!
Ninamwomba Mungu anipe Roho ya utumishi usiokuwa na mipaka wala ubaguzi ili nitakapoondoka niwe nimeacha alama katika maisha ya watu.
1 comment:
Godlove that was really powerful, really touching, nimependa sana comment yako kwamba kumtumikia Mungu bila kuchagua na kuweka alama kwa watu, that people will have something nice to tell abt u. That's very encouraging. Homgera sana kwa kutumika na mtumishi wa Mungu in his last minutes.
Kwani ni lazima niweke jina, si mnanijua shalom broz!
Ni mimi mdau wa ughaibuni.
Nawapenda.
Post a Comment