Kuna kila dalili njema kwamba kaka yetu aliyeonekana kama anasuasua kwenye suala la kumtafuta mwenzi wake wa maisha sasa amempata na mwaka huu hautakwisha kabla hajatuletea mkwe! Jumamosi ilopita kaka yetu Elifadhili Solomon Msuya alikwenda rasmi kwa familia na kujieleza kwamba amekuwa na amepata mchumba na sasa anaomba baraka za wazee ili aendelee na process za kuoa. Kama kawaida kamera yetu ya SBP ilijimuvuzisha kwenye tukio hili muhimu kwa mdau huyu... Tukio hili kwa kigweno linaitwa kutoa MBUTA!
Kutoa maelezo kama haya ni kazi kidogo inayoweza kumtoa mtu mzima jasho. Kikao hiki kinahudhuriwa na watu wenye ndoa tuuu!! Waseja hawaruhusiwi hata kukaa karibu na nyumba inayofanyikia kikao!
Kaka Stanley Msami.
kaka mkubwa David Yonaeli Msuya.
Kabla ya uamuzi wa kuikubali Mbuta ni lazima mawasiliano yafanyike kwa ndugu walio mbali ili wapewe taarifa kwamba kijana amekuwa anataka kuoa.
1 comment:
Hongera sana mkubwa kwa kutangaza nia.
Nina mpango wa kukata rufaa maana sijagawiwa MBUTA.
All the best.
Post a Comment