Papaa On Tuesday......Kama Unajua Utahitaji Watu Kwenye Maisha Yako, Jifunze Kuishi na Watu
Wakati wa Zoezi la Kujiandikisha kwa ajili ya Vitambulisho Vya Taifa kwa Jiji la Dar, likikamilika tarehe 30 Julai, 2012 nina waomba Wale ambao hawajajiandikisha kwa ajili ya Vitambulisho Vya Taifa Wafanye Mchakato wa Kujiandikisha.
Nilipokua nimekwenda kwenye zoezi la Kujiandikisha weekend hii pale kwenye Ofisi ya Mtendaji Wa Kata, kwa sisi tunaofahamu kidogo Serikali za Mitaa kuna WEO's hawa ni Ward Executive Officers yaani Afisa Mtendaji Kata, halafu kuna MEO's yaani Mtaa Executive Officers, halafu kuna "Balozi" huyu ni Mjumbe wa Nyumba Kumi, Ngazi ya Juu tunaenda ni "Diwani" Kisha Mbunge, hawa wote ni wawakilishi wa Wananchi kuanzia ngazi ya Mtaa mpaka Taifa. Nilianza Mchakato nilianza kwa kuandikisha barua ya Mjumbe Kisha nikaenda Ofisi za Kata, huko ndiko nikakutana na Kituko Cha Mwaka.
Kuna watu wanaishi kama hawawahitaji binadamu wenzao katika maisha yao, Nyumba wanazokaa hakuna mtu anamjua anaingia asubuhi, anarudi Usiku, hana Story na Mtu, Ofisini anakofanya hana story na Mtu, hana uhusiano na hata Mtaa anaokaa, dukani kwa Mangi hawamjui yeye vitu ananunua Supermarket ana maisha ya "Kizungu". Kuna Mdada juzi wakati Wa Zoezi ndipo alipata somo, yeye kila akipita Mtaani gari kafunga Tinted hana story namtu, imefika saa ya kutaka kwenda kujiandikisha anajiuliza aende wapi?nani amuulize, hajui Ofisi za Mtendaji ziko wapi, Balozi anakaa Wapi, yaani hakuna anachojua na hakuna anayemjua alijua hakuna siku atakayohitaji kujua kutoka kwa watu wanaomzunguka yeye anajitosheleza.
Kuna watu duniani wanaishi maisha ya Kivyao Vyao, anaishi na watu wenye Status yake, Ukiwa chini ya Status yake hawezi japo kukupa Salamu, Kuna watu wanadharau wenzao sababu wao wamesoma, labda wana vyeo maofisini kwao, au kwa kuwa yeye ana gari haongei na Wapanda daladala ukimuuliza kwanini husalimii hao watu atasema, hakuna ninachopoteza akiwapotezea, hawezi ongea na watu ambao sio type yake. Nakumbuka nimewahi kuandika Hujafya Hujaumbika ndugu yangu.
Hivi inakupotezea nini Kuwasalimia watu ambao wewe unadai sio Status yako, Inakupunguzia nini kukaa na watu ambao umewazidi kila Kitu, Kuna Watu wana amini kwenye Maisha yao hawawezi pata msaada kwa watu wanaowazidi. Mungu yupo aliyekupa wewe ndio kawanyima wao, kuna siku utajikuta unahitaji msaada wa hao watu unao wadharau leo.
Kuna watu wanaamini fedha ni jawabu la Mambo yote, Kuliko Utu, Umewahi Waza siku Ukizidiwa na Malaria hapo kwenye shughuli zako kama fedha itakupeleka Hospitali??Umewahi Waza siku gari yako ikapata Ajali na wewe ukiwa umeumia kama fedha yako yako itakusaidia??Umewahi kuwaza kuwa Kila Unalopanda utakuja kuvuna??Huwezi kuishi duniani kama unaishi dunia ya peke yako, yaani unataka mambo yako watu wayachangamkie ya wenzio unayapuuzia thubutu yako utavuna unachopanda.
Mama yangu aliwahi ni hadithia hapo zamani, Kulikuwa kuna familia ambayo kama kuna sherehe au msiba wao waliamini fedha ni jawabu wakawa wanaenda wanatoa tu fedha wanaondoka, kwenye Msiba wanakwenda wanatoa rambi rambi kisha Wanaondoka hawawezi Kulala kwenye Matanga Sababu kuna Mbu. Siku Moja Baba Wa Familia ile akafariki, Watu Walichofanya wakaenda Wakatoa rambirambi Wanaondoka, Wanatoa rambirambi Wanaondoka, ile familia wakawa wanajiuliza mbona watu hawakai kama kwenye familia zingine, na Wao wamenunua mavyakula walidhani watu watakuja wawasaidie kupika Wale kumbe wapi, Wakashindwa wafanye nini mwisho wasiku wakakaa ndugu wakaamua kuzika ndugu wachache Vyakula vikadodoa, Vyakula vikaharibika, Siku Moja Nyumba ya Jirani Kukawa Kuna Msiba, Mama tajiri aliyefiwa Mumewe akaenda kwenye Msiba akakuta Wananchi wako busy na kazi, wengine wanapika wengine wanafunga turubai, wengine wanatengeneza mazingira, ndipo yule mama akamtafuta mama Mmoja aliyekuwa wa makamu akamuuliza, "Mbona juzi juzi nimefiwa na Mume wangu watu hamkuja, Mlitoa tu fedha Mkaondoka'???Yule mama wa Makamu akamjibu kwa hekima "Kama Kuna Siku Mnajua Mtawahitaji Watu, Basi Mjifunze Kuishi na Watu"
Biblia inasema Unavyotaka Watu Wakufanyie Wafanyie wewe Kwanza, maana formula ya Apandacho Mtu ndicho anachovuna, Ukipenda Ugomvi basi utavuna manundu. Ukitaka Mambo yako Watu wayafurahie yafurahie ya wenzio kwanza, Ukitaka kujifunza kupokea basi jifunze kutoa kwanza. Sisi tunahitajiana kila iitwapo leo.
Kuna watu huwa wanajiona wao ndo wao wapo maofisini, pengine sijui huyo mdada anatembea na Boss au ni kimada wa Mwenyekiti wa Bodi ya hiyo Ofisi, basi full dharau yeye kila mtu anamtishia, kila mtu kwake ni taka taka, unasahau huyo mwanaume hana mkataba na Mungu kuna siku atakufa hayo magari unayo leo yasikufanye ukdharau walimwengu, unakaa mtaa hakuna hata unae peana nae Salamu, Una Mkataba na Tanesco???siku nyumba itapata la kutokea na kutokea moto ukatokea nani atakusaidia hao unaowaona taka taka?siku gari ikinasa kwenye mtaro nani atakutolea, kuna mambo ukifanya hayakupunguzii chochote ila yakutengenezea future yako.
Kuna watu wanasema kuishi na binadamu ni Kazi, Kama unaona kazi Jaribu uishi na Wanyama ndo utagundua kwanini hukuumbwa Nguruwe ukaumbwa mtu. Kuwa mwema haimaanishi kuwa Mjinga, kutokuwa na Misimamo, Ila Kama unajua kwenye Maisha yako utawahitaji watu basi jifunze Kuishi na Watu, haishi kwneye Kisiwa Unaishi kwenye dunia ya wazi.
Kama unaona wewe ni bora sana, potezea ila Ushupazae shinga Itavunjika ghafla na wala hatapata dawa.
Think differently and make a difference.
Papaa
0713494110
No comments:
Post a Comment