Popote katika Kona ya dunia hii unaposoma Makala hii ya leo ninakusalimu Kupitia Jina La Bwana Wangu Yesu Kristo. Nimatumaini yangu ya Kuwa u Mzima na Unaendelea vema na shughuli za ujenzi wa Taifa na Maisha yako kwa Ujumla.
Wakati nchi yetu bado masekeseke ya kila siku yakiendelea huku tukishuhudia Mabosi wa Tanesco Wamesimamishwa na Bodi ya Shirika hilo, Bodi nayo imeitwa na Kamati Ya Bunge Dodoma kuhojiwa Kulikoni Kuwasimamisha Mabosi Wote???Nadhani sakata hili linafanana na Kusimamishwa kwa Mabosi wa ATC, nchi hii rah asana ukiwa na nguvu tu unafanya unachoweza ili mradi tu huvunji sheria, si unakumbuka Boss wa TBS nae alimimamishwa, Wakasimamishwa Wale Mabosi wa Wanyamapori, unafanya mchezo si ajabu kesho ukasikia Waziri Mwenye Dhamana na Habari amepiga marufuku ya Papaa On Tuesday kutoka, si anaweza bana utasema nini sasa.
Jana nilikuwa namuangalia Waziri Membe kwenye kipindi cha 45 Minutes akiongea sana na akitishia kutaja majina ya watu wanaomuharibia hapa nchini, alisisitiza sana lkuwa kuna siku atawataja hadharani. Kuna watu kutwa kucha tumekuwa tukiongea sana yaani maneno yanaweza kujaa Pipa zima ila matendo ni kama Kijiko tu, nikakumbuka maneno ya wahenga Mtaka Unda Haneni ila hufanya kile anachotaka kukifanya. Unadhani makelele ya watu yanaweza mnyamazisha asitende anachotaka kukifanya ni kama kujilipua tu, hasikii
maneno ya watu.
Kuna hadithi moja nili hadithiwa zamani nadhani pia inaweza kutusaidia. Siku moja kilikuwa kuna mashindano ya kupanda mlima ambao juu ya ule mlima kulikuwa na Lulu ambayo watu walitakiwa kuupanda huo mlima na kuchukua hiyo Lulu. Kando ya njia hiyo kulikuwa na watu na wanyama wa kutisha walikuwa wamewekwa kwa ajili ya kutishia bila kudhuru mtu. Kila aliyejaribu kupanda mlima alikutana na watu wale wa kukatisha tama njiani, walikuwa wanazomea na kuongea maneno ya kukatisha tama, mbwa walibweka, na wengine walitishia njia za Washiriki na wengi wao waliishia njiani hawakuza kutwaa Lulu. Alitokea kijana mmoja ambaye alidharauriwa na watu, huyu kijana aakaanza safari alipanda mlima mwanzo mwisho alikutana na makelele, na wanyama lakini alisonga mbele alivuka vikwazo vyote mpaka akatwaa Lulu, Watu walipoenda kumuongelesha wakagundua kijana hana uwezo wa Kusikia kwa maana ni “Kiziwi”, ndipo wakagundua kumbe kelele zote zile za njiani kijana hakuwa anazisikia na kwa sababu hiyo hazikuwa na madhara kwake, unataka kupiga hatua kwenye maisha kuna nyakati lazima uamue kutia pamba masikio, ila usitie pamba iliyolegea itabaki sikioni.
Mimi mwenyewe pamoja na wengine wengi tumekuwa tukipanga mambo mengi sana kwenye maisha yetu ya kila siku lakini tumekuwa hatutimizi yale tuliyokuwa tukijipangia changamoto kubwa ikiwa ni KUAMUA, tena KUAMUA kufanya. We unadhani watu hawana mipango??wahenga wakasema Mipango sio Matumizi, tunapanga lakini sasa issue kutimizia, mambo ambayo tumekuwa hatupangi kufanya ndio yamekuwa tunayapa kipaumbele na kuyatimiza na mwisho wa siku. Mtume Paul kwenye Moja za Nyaraka zake kwa Kanisa la Rumi anasema Lile ninalotaka Kutenda Silitendi nisilotaka ndilo ninalolitenda. Bibi yangu aliwahi niambia Wanaume hawana akili mpaka wanapokuwa wameoa, ndio maana wengi wao hupata mafanikio yanayoonekana baada ya kuoa kwa sababu tu kuna utekelezaji way ale wanayokuwa wamepanga.
Nakumbuka wakati nasoma mambo ya Utawala niliwahi soma “Theory X and Theory Y” ambapo moja ya theory hizo zinaeleza wazi kuwa By nature kuna watu hawapendi kutekeleza majukumu yao hata kama wamepanga kufanya na wamejiandikia kuyafanya majukumu hayo kwenye makaratasi mpaka awepo mtu wa kuwasimamia, we hujawai ona Wafanyakazi wengi hawakosi cha kufanya hata kama cha kuzuga once mabosi zao wanapokuwepo jirani na wao. Bila kusimamiwa wengine hawawezi kufanya kitu, lakini wengine hawafanyi sababu tu kuna watu “watawaonaje” ama “wanawakatisha tama”.
Katika hadithi ya kijana aliyekuwa na ulemavu wa masikio alishinda sababu aliamua ku-focus katika safari yake ya maisha yake. Ukijiridhisha na safari uliyonayo weka pamba kwa muda kuna wengine wako kando ya njia kukatisha tama wengine.
Lazima tujifunze Kukomaa katika kile tunachoamini kuwa tuko sahihi, lazima tujifunze kuamua, au hujui kujifunza kuamua inahitaji uamuzi, kuna nyakati zinatokea kwenye maisha unaona kama ulimwengu mzima unakuzomea, au ulimwengu mzima utakutazamaje, kuna wakati sababu ya kulinda reputations zetu katika jamii tumejikuta tumejifungia ndani, jambo moja ambalo huwa nina uhakika haijalishi ukubwa wa Mlima upende wa pili wa Mlima ni Mteremko, kuna kitu Mungu ametuwekea wandamu nayo ni kusahau, kuna watu ninawajua waliwahi kuwa na issues, wengine scandals wengine fedheha, wengine mapito, lakini it’s a matter of time, nothing lasts forever.
Kama kuna mtu unamuona leo yuko Juu basi lazima ujue aliwahi kuwa chini maana kila juu ina chini yake. Katika kutimiza ndoto za kwenye maisha lazima vitendo vichukue mkondo wake, ndoto sio ile unayoiota usiku ukiwa umelala, bali ndoto ni ile inayokukosesha usingizi wakati wengine wamelala.
Kama Nuhu angesikiliza maneno ya watu asingejenga safina, Kama Mussa angeendele kukubali kuitwa binti farao asingewakomboa wana wa Israel kutoka utumwani, Kama Daudi asingeenda kwente Battle Field na kuwasikiliza kakazake asinge mpiga Goliathi, Kila kitu kinatokea kwenye maisha kwa makusudi ya kujifunza. Wengi wetu tumewahi poteza fursa zaidi ya nyingi sababu tu ya kutokujifunza kosa tulilofanya mara ya kwanza tukakosea basi tumejikuta tumekuwa tukifanya hilo hilo kosa na kutunyima fursa ya kusonga mbele, kosa lile lile lililosababisha tukapoteza biashara na kupata hasara tumejikuta tukilirudia, kosa lile lile tulilolifanya tukakosa wenzi wa maisha sahihi tumejikuta tukilifanya sababu gani?hatujifunzi kutokana na makosa.
Kupenda ni Kuchagua, Kufanya ni Kuamua, think differently and make a difference.
Papaa Ze Blogger
"Shalombroz.blogspot.com" soon of facebook
No comments:
Post a Comment