Ajinyonga baada ya kufiwa na mtoto | Send to a friend |
MWANAMKE aliyefahamika kwa jina la Monika Mapoli[22],Mkazi wa Kijiji cha Isima kata ya Butundwe wilayani Geita, amekutwa amejinyonga juzi kwa kutumia kipande cha nguo karibu na Ofisi ya Mganga Mkuu Wilaya ya Geita. Taarifa za mashuhuda wa tukio hilo zilisema kuwa Mapoli alichukua uamuzi huo baada ya kufiwa na mtoto wake Jumanne Philimo(2) aliyekuwa amelazwa wodi namba moja katika Hospitali ya Wilaya ya Geita akipatiwa matibabu. Ilielezwa kuwa baada ya mtoto huyo kufariki dunia,mama huyo alitoweka wodini na kwenda kusikojulikana hadi alipokutwa amejining’iniza kwenye mti uliopo jirani na Ofisi ya Mganga Mkuu wa wilaya hiyo Dk Omari Dihenga. Mmoja wa mashuhuda wa tukio hilo Petro Majiasi aliyekuwa kwenye wodi hiyo alisema chanzo cha kifo cha mtoto huyo ni huduma duni za matibabu zinazotolewa hospitalini hapo ambapo tangu mtoto huyo alipolazwa hakupatiwa matibabu hadi mauti yalipomkuta. Akizungumzia tukio hilo, Mganga Mfawidhi wa Hospitali hiyo Dk.Nelson Bukuru, alithibisha kumpokea mtoto huyo saa 7 mchana juzi akisumbuliwa na homa ya mapafu lakini kutokana na uhaba wa dawa za kutibu ugonjwa huo walilazimika kumlaza wodi ya watoto ili taratibu za kupata dawa ya ugonjwa huo zikifanyika. Alisema kabla ya kupatikana kwa dawa hizo mgonjwa alifariki dunia akiwa amelazwa wodini chini ya uangalizi wa wazazi wake na katika hali ya kusikitisha kulipopambazuka walikuta mwanamke huyo akiwa amejinyonga na kuning’inia juu ya mti ulio ndani ya hospitali hiyo. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita Leonard Paul alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba jeshi la polisi linaendelea na uchunguzi ili kubaini chanzo. -Mwananchi Neno letu. Uchungu wa mwana aujuaye ni mzazi. Huyu mama inaonesha alipata uchungu mkubwa sana kwa kuona kwamba sehemu alipompeleka mwanaye ili apate msaada hakuupata na ikapelekea kifo cha mwanaye mpenzi. Inasikitisha kwamba alikata tamaa na kwakuwa mara nyingi pia kwenye hivi vituo vya afya watuhawana elimu ya ushauri nasaha hivyo aliishia kujinyonga. Hatujafurahishwa kabisa na jambo hili sisi kama watanzania na pia kama wanadamu tunaothamini sana maisha!! |
No comments:
Post a Comment