Tafuta/Search This Blog

Thursday, March 29, 2012

Siasa au matusi??



Hawa ndio wanasiasa wetu na hizi ndio kampeni zetu! Anayeongea hapo ni mwanamume mwenye mke nyumbani na ana watoto na pia chama chake kimemuamini kumtuma kuja kuongea kwenye kipaza sauti kwenye uwanja huo. Lakini jambo kubwa zaidi ni kwamba mtu huyu pia anakaa kwenye chombo kikubwa cha kutunga sheria hapa nchini, BUNGE.

Nimesikitika sana kwa sababu mwanasiasa anajitapa kwenye jukwaa kwamba yeye ana MATUSI. Kama chama kina watu wenye umri mkubwa na wameona hii naamini hawatakaa kimya, lakini kama ni kweli kwamba ni genge la wahuni then watakaa kimya na kufurahia haya ambayo kuna siku watayatolea hesabu mbele za waTanzania.

Namalizia kwa kusema, biblia inasema,"Msidanganyike, mazungumzo mabaya huharibu TABIA njema."

1 comment:

Subi Nukta said...

Hayo maneno aliyoyasema yote hapo, lipo hata moja linalotekelezeka ili kumkomboa mwananchi kutokana na matatizo yake?

Pengine siasa hatuzijui sisi, lakini maneno yao yanatuathiri sana. Kama ameweza kutamka kwenye hadhara, sijui ni hali ikoje wawapo kwenye faragha.