Tafuta/Search This Blog

Wednesday, June 30, 2010

Tuesday, June 29, 2010

WANYAMA WANAPATA TAABU NCHI KUGEUKA JANGWA

TUTUNZE MITI ILI ITUTUNZE...
Kuna foleni kama hizi katika ATM, LUKU, Maji, nk.... sasa wanyama wameanza.
Kukojoa kwa zamu.

Thursday, June 24, 2010

(Uwiiiiiii! Ungejua...) Haya angalia kwa makini


1

2

3

4

Wakati mwingi tunafanya mambo bila kujua upande wa pili wa jambo lenyewe. Tunakua kama huyo ndege asiyejua kusoma wala kuandika... lakini huyu aliyeandika habari za Global Warming haku-foresee. 

Jenga Tabia ya kuona mbali, Ila hata kama utaweza kuona mbali huwezi kuzuia mambo kama ya picha 1

Monday, June 21, 2010

Familia yaongezeka...

Hatimaye katika familia ya Mr & Mrs Mwakajila (Jojo Jose na Matilda Mlay) amezaliwa mtoto wa kike wiki iliyopita. Mama pamoja na mtoto wote wako salama na wenye afya njema.

SBP tunapenda kumshukuru Mungu pamoja nanyi kwa baraka hii kubwa katika familia yenu. Na kama ilivyo ada tutakuja kuleta uvumba na manemane na kunywa mtori japo kidogo katika kumsindikiza Matilda.

**Mr & Mrs Mwakajila ni watumishi wa Mungu katika uimbaji na ni wadau wa karibu wa hili baraza.

Saturday, June 19, 2010

Pastor and mrs Elisa Kabora.

The newly wed couple have been seen in the city of Arusha enjoying their honey moon!

SBP wishes Pastor and Mrs Kabora all the love and happiness in their new life!!

Ujumbe kwenye t-shirt!


Unajifanya huelewi??

Tangi J atangaza nia!!


Hatimaye kijana wetu Joshua Lwendo almaaruf Tangi J(in the box) leo ametangaza nia nyumbani kwa mchungaji Nathaniel Sasali kwamba analo kusudio la kumuoa binti yake aitwaye Happy!

Akiwa amesindikizwa na mshenga maarufu mzee Kalinga pamoja na washangiliaji lukuki waliobeba mavuvuzela yao kijana aliutangazia umma kwamba amekua.

Haya sasa tunasubiria mpunga! Hongera Tangi J!!

Friday, June 18, 2010

Mwananyamala...

Mambo ya mwananyamala...



Hii nyumba ipo maeneo flani ya mwananyamala. Inaonekana ni ya miaka mingi iliyopita na imechoka na bahati mbaya zaidi imekaa kwenye mkondo wa maji. Ninaamini baada ya miaka michache nitakuta nyumba nyingine kwenye eneo hili kali sana.
Ila nimependa sana ujumbe niliokuta kwenye mlango wa mbele wa nyumba hiyo!!

Mapenzi popote

Hawa niliwakuta ubungo maziwa. Wamekaa kwa amani wakiongea...kweli mapenzi hayaogopi hata magari!!





Safi sana!

Thursday, June 17, 2010

Janga la kitaifa!!

Rafiki yangu mmoja aliwahi kuniambia kwamba lugha ya Kiingereza ni janga la kitaifa maana kwa kweli inatupeleka vibaya sana. Tunapenda sana kuitumia lakini tunatumia kile kinachoitwa "kiingereza cha ugoko!!"

Hii nimekutana nayo siku za karibuni...



Kwa mbele...



Nadhani alimaanisha YESU NI NGUVU au KWA NGUVU ZA YESU, nimeshindwa kuelewa!!



Kwa nyuma...



Nadhani alimaanisha NI MAOMBI PEKEE!




Hivi hakuna washauri kabla ya kuandika????

Tuesday, June 15, 2010

Elifadhili atoa MBUTA!!

Kuna kila dalili njema kwamba kaka yetu aliyeonekana kama anasuasua kwenye suala la kumtafuta mwenzi wake wa maisha sasa amempata na mwaka huu hautakwisha kabla hajatuletea mkwe! Jumamosi ilopita kaka yetu Elifadhili Solomon Msuya alikwenda rasmi kwa familia na kujieleza kwamba amekuwa na amepata mchumba na sasa anaomba baraka za wazee ili aendelee na process za kuoa. Kama kawaida kamera yetu ya SBP ilijimuvuzisha kwenye tukio hili muhimu kwa mdau huyu... Tukio hili kwa kigweno linaitwa kutoa MBUTA!

Hapa anatoa maelezo kwamba upweke umemshinda na ameona atafute mwenzake!


Kutoa maelezo kama haya ni kazi kidogo inayoweza kumtoa mtu mzima jasho. Kikao hiki kinahudhuriwa na watu wenye ndoa tuuu!! Waseja hawaruhusiwi hata kukaa karibu na nyumba inayofanyikia kikao!
Kaka Kibabu akimsikiliza kijana akimwaga sera.

Dada Krista.

Kaka Gee



Kaka Stanley Msami.




kaka mkubwa David Yonaeli Msuya.

Kaka Godson Y. Msuya.


Kaka Max.



Kabla ya uamuzi wa kuikubali Mbuta ni lazima mawasiliano yafanyike kwa ndugu walio mbali ili wapewe taarifa kwamba kijana amekuwa anataka kuoa.



Baada ya kueleweka, sasa Mbuta inaweza kusogezwa ili ikabidhiwe kwa wakubwa.




Mama mkubwa akionja kama Mbuta imeiva au la. mama alikubali kwamba imeiva na kumpa kijana baraka za kuendelea.



Sasa mambo ni Bien, twaweza kunywa na kumpongeza kijana.




Sasa mwali anatambulishwa na kukaribishwa kwenye familia.


Mwisho kabisa ni sala ya kumalizia yote.
SBP inakutakia kaka Solo maandalizi mema ili tuje kubandika picha za arusi soon.

Wednesday, June 2, 2010

LEO HEDARU KESHO...?

Najua sababu zinazofanya Wananchi ambao tumezoea kuwapa jina la WENYE HASIRA kuvamia vituo au kuwaua watuhumiwa wa uhalifu... Sababu hizi hata Said Mwema anazijua. Sasa tutafika wapi katika haya? Nini kifanyike?