Tafuta/Search This Blog

Tuesday, December 21, 2010

UKIPENDA BOGA UPENDE NA UA LAKE.


Nadhani wote tumesikia kuhusu mgomo wa wanachuo wa chuo kikuu cha Dodoma juzi na jana. Mimi kwa upande wangu sikutegemea chuo ambacho kipo kwenye mjengo wa chama Tawala kuna siku watagoma na kuona mabaya ya chama "chao".
Nimeshangaa sana kwamba hawa wanaharakati ambao wiki chache zilizopita waliishangilia serikali mpya na waliunda kwaya wakati wa kampeni kumsapoti mkuu, na pia waliitisha press conference kwa ajili ya kuwasema vibaya wanaharakati wa CHADEMA walipotoka nje ya bunge kwa ajili ya kudai haki za msingi za wa Tanzania, leo na wao wamezinduka! Hahahaa mmechelewa sana wadogo zangu. Itisheni tena basi ile press conference labda watawasikiliza tena wakati huu mnapokuwa kinyume nao!!
Mlidhani mtavuna nini baada ya kupanda bangi?? Haya tunawasikiliza kwa furaha sasa.
Namalizia na haya maoni yaliyotolewa na wadau wa website ya Global Publishers kuhusu habari hii nikayapenda sana;


"Teeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeh! tuliwaonya UDOM yakowapi sasa. Siyo nyie mlio kuwa mstari wa mbele kuchangia pesa kwa ajili ya kuchukulia fomu mheshimiwa, na siyo nyie mlioandika barua ndefu mkilaani yaliyotendwa na CHADEMA. mlidhani mtapewa kipaumbele kikubwa au kuwa mambo yatabadilika, hapo mtasoma plate number. Mkumbuke kuna deni la dowans na madeni ya pesa za kampeni, zote zinatakiwa zirudishwe. Hilo ni trela bado miaka 4 na miezi kadhaa, itawagharimu sana. Hiyo ndo raha ya kurupuka bila kupima na kuropoka. vumilieni ndo serikali mlioitaka. Tchaoooooooooooooo ndo maana yake."

****************************************************************************
"sasa ndo mnafanya nini? Mbona na nyie mmemgomea Rais? Au hamjui suala la kuhakikisha ubora wa elimu ni moja kati ya ahadi zake na kama hicho ndo alichowaahidi so mnagomea nini? Nyie U DOM ni waajabu sana tulitegemea wasomi kama nyie ndo mgekuwa mstari wa mbele kutazama maovu ya nchi na kusapoti wanaharakati kama wabunge wa CHADEMA ila ushamba wenu uliwafanya kukurupuka tu, Kweli kunakitu hamkipati kama wanavyuo wenzenu hasa hizo field ndo maana mnajua kuwa hapo chuoni ndo mmemaliza kila kitu. Ondoeni tongotongo kunekucha eh!!!!!!!!"
.

No comments: