Tafuta/Search This Blog

Saturday, December 18, 2010

Tangi J alipopata mwenza wake!

Hayawi hayawi sasa yamekuwa!! Walisema haijai sasa inamwagika!!!
Hatimaye mmoja kati ya wakurugenzi wa SBP kaka Tangi J a.ka Tangibovu amejitwalia mtoto wa kinyasa na kuhalalishiwa mbele ya mimbari takatifu ya kanisa la TAG Kigogo Mburahati Dar Es Salaam. Ilikuwa ni siku iliyofana sana na hatuna mengi maana picha zifuatazo zinajieleza...Mr&Mrs J Lwendo wakiwa na nyuso bashasha za kuanza maisha mapya
Usafiri walioutumia maarusi!


Maarusi wakiwa wamezungukwa na jopo la waheshimiwa wasimamizi na mashahidi. Wote hawa ni ndugu wa Joshua na Happiness.


Vijana wakipigwa maombi ya kuwasaidia kulitunza agano waliloliweka la ndoa takatifu.


Happiness a.k.a Chimwemwe akimvishapete mume wake.

Tangi pia akimvisha pete mkewe.



Maarusi na mashahidi wao. Mr&Mrs J Lwendo na Mr&Mrs G Lwendo.




Kama hapo juu.



Fullu kicheko.


Matumaini.

Wote kwa pamoja.
SPB inawatakia baraka za Mungu katika maisha yenu na Shemeji jiandae kwa ugeni wetu siku za karibuni tutakapokuja kukukabidhi jiko!!

2 comments:

Subi Nukta said...

Mungu awabariki sana.
Hongereni kwa kufunga arusi, mlipendeza.
Asante kwa picha!

Anonymous said...

Mlipendeza sana hongera sana kaka Tangi J...