Tafuta/Search This Blog

Monday, May 23, 2011

Friday, May 20, 2011

Breaking Newzzzzz!!!!

Habari kutoka blog ya jamii yaani MICHUZI zinasema kwamba sheikh Yahya Hussein amefariki dunia leo. Sheikh Yahya alikuwa mtabiri maarufu sana na mnajimu wa mambo ya nyota.

CAMARO Boutique Tabata Bima.

Duka la vitu vya ukweli ndani ya Tabata Bima opposite Swiss Pub. Njoo ujipatie vitu vya wakati huu na kama hutavipata dukani kwetu tutakuagizia.

Jionee baadhi ya vitu vyetu hapa...





Mambo ya mitoko ya mguuni...




Contact 0712-679651 or 0712700066

We receive orders and we also provide self delivery service.

Thursday, May 12, 2011

MAKOMANDOO VHM WAICHOMA MOTO AIRPORT YA WACHAWI HANDENI TANGA!!!!

Salaam sana katika jina la Yesu Kristo.

Ama kwa hakika Mungu anatenda mambo ya ajabu sana.

Huduma ya VHM Tanzania kupitia kikosi chake cha mashambulizi wiki hii, kilitua na kupiga kambi katika wilaya ya Handeni mkoani Tanga katika moja ya vijiji sugu vilivyo jaa nguvu za giza, uchawi na mambo ya kishirikina. Ilikuwa ni wiki la mapambano makali sana katika ulimwengu wa roho na katika ulimwengu wa mwili pia.

Roho za uchawi, uasherati na uzinzi zimekandamiza sana vijiji hivi vya Handeni na kuwafanya wakazi wake kuishi kwa shida bila matumaini yeyote.

Hili lilikuwa ni wiki la kufunga na kuomba pamoja na kupambana na mkuu wa anga la vijiji hivi ili tutakapokwenda kuhubiri, watu wawe wamelainishwa mioyo yao tayari kwa kupokea injili ya Bwana wetu Yesu Kristo.



KAMBI YA WAEBRANIA VIJIJI VYA HANDENI




Hapa ndipo mahali ambapo jeshi la Bwana kikosi cha wakata “network za shetani” kilipoweka kambi katika kijiji hiki hapa handeni. Hawa ni watu wenye kazi zao na biashara zao za maana tu, lakini hawakujali kuacha nyumba zao nzuri na kuja kuishi hapa chini ya miti na kulala chini ili kufunga na kuomba kwa ajili ya kupambana na mkuu wa anga ili aweze kuwaachia huru watu wa Mungu katika vijiji hivi.

Mkuu wa anga huwa hafanyi kazi peke yake, ameweka ma agent wake ili kukamilisha kazi zake. Katika kampeni hii ya kuvunja kazi za shetani tulifanya utafiti na tukagundua maeneo mbalimbali ambayo mkuu wa anga anafanya kazi kupitia ma agent wake alio waweka kuifanya kazi yake.

Tulifanikiwa kupenya katika nyumba zote za waganga na wachawi maarufu kijijini hapo na kufanya maombi ndani ya nyumba zao bila wao kujua. Tuliingia kwa wachawi na tulijifanya kama wateja wanaotafuta kufanyiwa ramri ili tuweze kupata tiba na kuwajua wabaya wetu. Ilikuwa patashika nguo kuchanika.



HII NDIYO AIRPORT YA KUPOKEA NA KURUSHA NDEGE ZA KICHAWI



Hii inayoonekana katika picha hizi hapo juu, inajulikana kama AIRPORT ya wanga na wachawi. Katika msitu huu, hapa ndipo ndege zote za ungo zinapotua na kupaa kutoka na kwenda sehemu mbalimbali hapa nchini na hata nje ya nchi kwa kutumia ungo na vifaa vya kichawi.

Kwa kawaida, msitu huu ambao wanakijiji wameupa jina la airport, mali na shughuli za usafiri wa kichawi, eneo hili lenye ukubwa wa zaidi ya hekali mia moja, hutumika pia kwa shughuli za matambiko ya kimizimu pamoja na shughuli za kichawi. Mti unaoonekana katika picha ya juu hutumika kuhifadhi mimba za wanawake ambao mara tu baada ya kupata ujauzito mimba zao huchukuliwa kichawi na kufungwa juu ya mti huu. Wanawake hao hubakia na matumbo makubwa lakini ndani yake hakuna kitu. Tulikutana na wanawake wajawazito ambao mimba zao zimechukua zaidi ya miaka miwili na bado hawana dalili zozote za kujifungua.

Picha hiyo ya mwisho hapo juu, ni picha ya kaburi ambalo limechimbwa kichawi. Kazi ya kaburi hilo ni kuwavuta watu kimazingara na kuwazika humo kichawi na huyo mtu aliyezikwa humo kichawi ndio atakuwa amepotea ghafla au kuanguka ghafla na kufa, lakini katika hali halisi atakuwa amehamia katika ulimwengu mwingine.

Tumekutana na mambo makubwa sana na ya ajabu ya kushangaza. Tangu tumeanza huduma hatujakutana na maruweruwe kama tuliyoyaona katika kambi hii ya maombi.



USIKU WA UVAMIZI KWENYE UWANJA WA WACHAWI



Huu ni usiku ambao huwenda sitausahau katika maisha yangu yote. Ulikuwa ni usiku wa kuwavamia wachawi na wanga wakiwa wametua katika uwanja wao huo kufanya shughuli zao kisha kuruka kuelekea katika miji tofauti walikotoka. Ilikuwa ni kama MOVIE ya kinaijeria, lakini ilikuwa ni kweli na LIVE, maana mimi mwenyewe nilikuwepo katika msafara huo.

Tulivamia airport hiyo usiku wa saa nane kabla hawajaruka kurudi walikotoka. Lengo letu ilikuwa ni kuwakamata na kuwapeleka katika kambi yetu ya maombi ili tuweze kuwashughulikia vizuri. Katika operation hii tuliteua makomandoo kama 11 kufanya uvamizi huu usiku wa manane. Tulipoingia katika msitu huo, tulikuwa tukitembea kwa kunyata mithiri ya mwizi anayetaka kuiba bila kusikika. Tulikokuwa tumekaribia uwanja huo, wachawi hao walihisi uvamizi huo na ndipo lilipotimia lile neno linalosema adui watakuja kwa njia moja na watatawanyika kwa njia saba. Hivyo ndivyo ilivyokuwa. Wachawi hao walitimua mbio na kupepea kama karatasi na kutokomea.

Kwa sababu tulikuwa tumewakurupusha, waliacha baadhi ya vifaa vyao walivyokuwa wakivitumia hapo airport yao. Hapo ndipo tulipopata wasaa kukusanya kila kitu chao kilichokuwepo hapo kwenye airport yao, usiku huo huo tulikwenda kutafuta moto na tukavipiga moto na kuvisimamia vikiteketea kwa moto mpaka vilipomalizika vyote ndipo tuliporudi kwenye kambi yetu na kuendelea na maombi. Picha ya tatu kutoka kushoto ni kaburi la kichawi ambalo hutumika kupotezea watu, kaburi hilo nalo tulilichoma moto. Katika vijiji hivyo kuna taarifa nyingi za watoto wengi na baadhi ya watu wazima kupotea katika mazingira tata na mpaka leo hawajawahi kupatikana.



KUZAMIA


Unaweza kuona na kuhisi jinsi ambavyo kikosi chetu cha mashambulizi kilivyokuwa kikiomba kwa uchungu na mzigo dhidi ya mambo ambayo shetani anayafanya katika vijiji hivyo. Ilikuwa ni wiki la kazi moja tu kuomba na kushambulika ngome na vichaka vya shetani. Tuliweza kuona jinsi shetani anavyowatesa watu na kuwadhalilisha watu. Tuliona waganga wakiwachukuwa watu wazima na kuwapeleka kwenye vidimbwi na kuwavua nguo na kuwaogesha wakiwa uchi tena hadharani mchana peupe ili kuwaondoa nuksi. Hii ndiyo sababu tulikuwa tukiomba kwa uchungu kwa ajili ya ukombozi wa watu hawa


KUFUTURU

Baada ya mfungo huo mzito wenye misukosuko mingi, huu ulikuwa wakati wa kufungulia na kupata chochote kwaajili ya tumbo maana ulikuwa ni mfungo mzito sana lakini Mungu alitutia nguvu sana. Tuliziona nguvu zisizo za kawaida ndani yetu na ndipo tulipoungana na mtume Paulo pale aliposema “sio mimi ninayeishi bali Kristo ndani yangu” Wanakijiji walikuwa wanatuhurumia sana kwani msitu huo huwa hauingiwi na watu wa kawaida na kama mtu asiyehusuka akiingia hata kama ni kwa bahati mbaya, basi atakuwa kichaa au akiingia na viatu atapata matende na wakati mwingine atauwawa kichawi kabisa. Hayo ndiyo wanakijiji waliyoyategemea kuyaona yakitokea kwetu kwani hatukuiheshimu mizimu yao. Pamoja na mambo yote hayo Mungu ametutetea hakuna aliyejikwaa wala hata mafua. TUPO NGANGALI KATIKA BWANA YESU KRISTO.

Wiki hii tunapeleka kikosi kingine kule KILWA mahali tulipokuwa tumefanya huduma wiki chache zilizopita ili kwenda kuimarisha kazi tuliyoianzisha na kuwatia moyo kondoo waliompa yesu maisha wakati wa misheni hiyo.

Tunahitaji sana uwezesho ili kazi hii iweze kusonga mbele.


If you would like to support this Ministry and Mission:

THE VOICE OF HOPE MINISTRIES

NBC VICTORIA BRANCH

A/C NO. 074103001247

M-pesa 0767 56 39 39

Tigo-Pesa 0713 18 39 39

In Christ

Peter Mitimingi.



NB: Tunamfahamu vyema kaka Peter Mitimingi ambaye ni mratibu wa hii huduma. SBP tunaipongeza sana hii huduma na wote waliojitolea kuifanya kazi ya Mungu na tutaendelea kuwapatia taarifa wananchi/wapendwa.

Tuesday, May 10, 2011

Monday, May 9, 2011

Mkapa aibuka shujaa.

BAADA ya kimya cha muda mrefu, huku akizongwa na kutuhumiwa kwa mambo kadhaa, Rais mstaafu Benjamin Mkapa ameibuka shujaa katika siku za karibuni. Hata mwenyewe amelitambua na kulithibitisha hilo.

Kuzingatia vipaumbele, kuinua uchumi na kukusanya kodi, ni baadhi ya mambo anayojivunia, na ambayo jamii inayatumia kumpima na kulinganisha utawala wake na wa Rais Jakaya Kikwete.

Mkapa ambaye mara baada ya kumaliza ngwe ya uongozi wake aliandamwa na kashfa za ufisadi, hivi sasa anatajwa kuwa kiongozi mahiri aliyemudu kudhibiti mfumuko wa bei pamoja na kukuza uchumi, tofauti na utawala wa sasa wa Rais Kikwete.

Utawala wa sasa umekuwa ukilalamikiwa kwa kufifisha uchumi, kushindwa kudhibiti mfumuko wa bei pamoja na maisha ya wananchi kuzidi kuwa magumu kadiri siku zinavyosonga mbele.

Serikali ya Awamu ya Nne ilipoingia madarakani mwaka 2005, zilifanyika jitihada za chinichini kubeza kazi za Rais Mkapa na kuibua kashfa mbalimbali zilizowahusu watendaji wake na yeye mwenyewe.

Kuna wakati wananchi walifikia mahali pa kuaminishwa kwamba Rais Mkapa aliharibu nchi, hata baadhi ya vijana wakadiriki kumzomea.

Hata hivyo, ugumu wa maisha, kinyume cha ahadi ya maisha bora ya Rais Jakaya Kikwete, umewafanya wananchi wamwone Rais Mkapa kama shujaa aliyeinua uchumi, ambao sasa hivi unadidimia na maisha yanakuwa magumu zaidi.

Kiongozi huyo ambaye mara nyingi amekuwa kimya kuzungumzia masuala mbalimbali ya utawala wake, alionyesha wazi hisia zake juzi usiku jijini Dar es Salaam baada ya kukabidhiwa tuzo ya heshima kwa mchango wake wa kuthamini michezo nchini, iliyoandaliwa na Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA).

Serikali ya Mkapa ndiyo iliyosimamia ujenzi wa Uwanja wa Taifa kwa ushirikiano na China. Ni uwanja wa kisasa wenye uwezo wa kuingiza watu 60,000 waliokaa.

Mkapa alisema wakati akiingia madarakani aliikuta nchi katika hali ngumu ya kiuchumi, jambo lililomfanya kuweka kando mambo mengi na kutoa kipaumbele katika uchumi ili wananchi waweze kupata unafuu wa maisha.

Alibainisha kuwa alijikita katika uboreshaji wa ukusanyaji wa kodi na kulipa madeni ili kuliokoa taifa na wananchi wake kwenye hatari ya kudidimia kiuchumi.

Alisema kazi ya kuimarisha uchumi haikuwa nyepesi, hivyo alilazimika mara kadhaa kuumiza kichwa na kukubaliana na washauri wake wakiwemo mawaziri katika kipaumbele cha kuimarisha uchumi wa nchi.

Mkapa alisema kutokana na mazingira aliyoyakuta wakati anaingia madarakani alilazimika kutumia kanuni za hayati Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere za kuwa kupanga ni kuchagua na kutenda ni kuamua.

“Mwalimu Nyerere alikuwa akisisitiza umuhimu wa kufanya jambo husika kulingana na wakati uliopo, nami nilipanga, nikachagua na matokeo yake yakaonekana,” alisema.

Alisema kuwa aliona ni muhimu kujenga misingi imara ya uchumi kwa kuimarisha ukusanyaji wa kodi ili kuiondoa nchi katika wimbi kubwa la madeni iliyokuwa ikidaiwa.

“Katika kipindi changu cha awamu ya kwanza nilipoingia madarakani, nilionekana kutopenda michezo kwa sababu nililazimika kuongoza kiukapa kutokana na mazingira niliyoyakuta. Hivyo, niliamua kuanza na kuimarisha uchumi kwa kujenga misingi ya kukusanya kodi.

“Pamoja na mambo mengine, kazi hiyo ilifanyika kwa umakini mkubwa na ilinifanya nishindwe kuhudhuria hata masuala ya michezo… na hiyo ikawa sifa yangu ya kuonekana sipendi michezo,” alisema.

Aliongeza kuwa mazingira ya wakati ule yalimfanya afikirie zaidi uchumi na aliiwezesha serikali yake kupata msamaha wa madeni iliyokuwa ikidaiwa na nchi wahisani na wafadhili.

Mkapa alisema baada ya awamu ya kwanza kuimarisha uchumi ilipofika awamu ya pili ya utawala wake ndipo sasa akaamua kugeukia mambo mengine, yakiwemo hayo ya michezo ambapo aliona kitu pekee ambacho anaweza kuwaachia Watanzania na kuwa kumbukumbu nzuri kwake ni kujenga uwanja wa soka wa kimataifa katika Jiji la Dar es Salaam.

Hafla hiyo ilihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa serikali wakiongozwa na Makamu wa Rais, Dk. Mohamed Gharib Bilal, Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Emmanuel Nchimbi na watu mashuhuri ambao baadhi yao wamelilitumikia taifa katika nyanja mbalimbali.

Mkapa pamoja na kupewa heshima hiyo bado alitoa wito kwa Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo nchini (TASWA) kuhakikisha wanautambua mchango wa Rais Kikwete katika medani ya michezo.

Alisema kujengwa kwa uwanja huo wa kimataifa Rais Kikwete amefanya kazi kubwa ya kujenga hoja wakati walipokwenda China kuomba msaada wao ili kufanikisha ujenzi huo.

Alisema kuwa baada ya serikali yake kuamua kujenga uwanja wa mpira wa miguu wa kimataifa, kazi ya kujenga hoja na kufanya mazungumzo ya namna gani uwanja utakuwa alimuachia Rais Kikwete wakati huo akiwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na hatimaye hoja zake kufanikiwa na China kukubali kuujenga.

“Hivyo Rais Kikwete anastahili heshima ya kutambulika kwa mchango wake katika michezo kwa kitendo chake cha kuwezesha kujengwa uwanja huo pamoja na aliyekuwa Waziri wa Kazi, Ajira na Vijana, Profesa Juma Kapuya, kutokana na kuhimiza mara kwa mara kuhusu mchakato wa kuanza kwa ujenzi wetu,” alisema Mkapa.

“Kapuya amefanya kazi kubwa katika kufanikisha serikali kujenga uwanja huo wa kimataifa, alikuwa akinihimiza mara kwa mara na hatimaye tukafanikisha. Hivyo TASWA mnapaswa kutambua mchango wake na ikiwezekana naye apewe tuzo ya heshima,” alisema.

Aliwaomba Watanzania kutambua haki na wajibu wa kuutunza uwanja huo ili uweze kudumu kwa muda mrefu na hatimaye kuwa kumbukumbu hata kwa kizazi kinachokuja.

Wakati akizungumza hayo, alikuwa akiwaeleza waliofika kushuhudia tukio hilo la utoaji wa tuzo kwa mwanamichezo bora wa mwaka 2010.

Katika hafla hiyo, Mkapa alionekana kukonga nyoyo za waliohudhuria ambapo mara kwa mara alilazimika kusitisha kwa muda kusoma hotuba yake kutokana na kushangiliwa, ikiwa ni ishara ya kuukubali utawala wake na mambo aliyolifanyia taifa.

Akizungumza katika sherehe hizo, kabla ya kutoa tuzo ya mwanamichezo bora, mgeni rasmi Makamu wa Rais, Dk. Mohamed Gharib Bilal, alisema amefanya kazi na Rais Mkapa wakati huo yeye akiwa Katibu Mkuu Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, ambapo alisifu ujasiri aliokuwa nao Mkapa katika mambo mbalimbali.

“Rais wetu mstaafu tunakupa heshima kubwa ya kutambua kuwa nchi yetu inahitaji kufungua njia katika sekta ya michezo na kwa kufanya hivyo ulikubali kubana bajeti ya serikali ambayo ingejenga zahanati na shule lakini ukatambua afya njema na elimu bora hupatikana kama wananchi wanashiriki michezo.

“Uwanja uliotuachia ni kielelezo tosha na wala usikatishwe tamaa na vijana hawa wanaposhindwa kutupa matokeo mazuri katika mechi zao na hakika kazi yako uliyofanya itabaki katika ramani ya michezo nchini na kamwe haitasahulika,” alisema Dk. Bilal huku akisifu ujasiri wa rais ambao alithubutu na hata kuweza kujenga uwanja huo wa kimataifa.

-Tanzania Daima.

Wednesday, May 4, 2011

Monday, May 2, 2011

OSAMA BIN LADEN IS DEAD....

Wakati wa uhai wake



Tutakukumbuka kwa mengi, likiwemo la September 11, 2001. Bwana ametoa Bwana ametwaa Jina lake Libarikiwe
Akiwa ameudedi