Kuna wakati huwa sielewi kwamba tatizo liko wapi. Kwa mfano kwenye hii picha hapa chini...
Hapa ni ubungo, kuna power plant kubwa na upande wa pili kuna mtambo mkubwa wa kuzalisha umeme kwa kutumia Gas. Lakini ajabu ni kwamba eneo hili liko busy na shughuli za wananchi. Kuna wanaouza mboga na matunda kuna wanaouza mitumba kuna wanaouza DVDs na vitu vingine vingi bila kusahau wanunuzi wao! Sasa mimi hadi sasa hivi sijaelewa kwamba yakitokea maafa hapa tutamlaumu nani?? Tutamlaumu Mungu, au Tanesco kwa kuweka mitambo hapo? au City Council kwa kushindwa kutukataza kufanya biashara hapo? au tutamlaumu mwananchi kwa kununua bidhaa hapo? au labda mtanilaumu mimi kwa kuandika haya??
Nimeamua kumuachia Mungu....
1 comment:
Nashangaa, wakiambiwa watasema wananyanyaswa..
Post a Comment