Tafuta/Search This Blog

Tuesday, June 15, 2010

Elifadhili atoa MBUTA!!

Kuna kila dalili njema kwamba kaka yetu aliyeonekana kama anasuasua kwenye suala la kumtafuta mwenzi wake wa maisha sasa amempata na mwaka huu hautakwisha kabla hajatuletea mkwe! Jumamosi ilopita kaka yetu Elifadhili Solomon Msuya alikwenda rasmi kwa familia na kujieleza kwamba amekuwa na amepata mchumba na sasa anaomba baraka za wazee ili aendelee na process za kuoa. Kama kawaida kamera yetu ya SBP ilijimuvuzisha kwenye tukio hili muhimu kwa mdau huyu... Tukio hili kwa kigweno linaitwa kutoa MBUTA!

Hapa anatoa maelezo kwamba upweke umemshinda na ameona atafute mwenzake!


Kutoa maelezo kama haya ni kazi kidogo inayoweza kumtoa mtu mzima jasho. Kikao hiki kinahudhuriwa na watu wenye ndoa tuuu!! Waseja hawaruhusiwi hata kukaa karibu na nyumba inayofanyikia kikao!
Kaka Kibabu akimsikiliza kijana akimwaga sera.

Dada Krista.

Kaka Gee



Kaka Stanley Msami.




kaka mkubwa David Yonaeli Msuya.

Kaka Godson Y. Msuya.


Kaka Max.



Kabla ya uamuzi wa kuikubali Mbuta ni lazima mawasiliano yafanyike kwa ndugu walio mbali ili wapewe taarifa kwamba kijana amekuwa anataka kuoa.



Baada ya kueleweka, sasa Mbuta inaweza kusogezwa ili ikabidhiwe kwa wakubwa.




Mama mkubwa akionja kama Mbuta imeiva au la. mama alikubali kwamba imeiva na kumpa kijana baraka za kuendelea.



Sasa mambo ni Bien, twaweza kunywa na kumpongeza kijana.




Sasa mwali anatambulishwa na kukaribishwa kwenye familia.


Mwisho kabisa ni sala ya kumalizia yote.
SBP inakutakia kaka Solo maandalizi mema ili tuje kubandika picha za arusi soon.

1 comment:

fstaki said...

Hongera sana mkubwa kwa kutangaza nia.
Nina mpango wa kukata rufaa maana sijagawiwa MBUTA.
All the best.