Muhimbili yazichachafya taasisi za Serikali 84 Wiki ya Utumishi wa Umma
· Yaongoza
kwa tuzo ya Ubunifu (Kangaroo) na Banda Bora
Na. Aminiel Aligaesha (MNH)
Hospitali
ya Taifa Muhimbili (MNH) imezichachafya taasisi 84 zilizoshiriki
maonyesho ya wiki
ya Utumishi wa Umma kwa kutwaa tuzo mbili kati ya tano maalum
zikiashiria kuwa mshindi wa kwanza kwa kila tuzo. Tuzo ya kwanza ni ya
ubunifu katika kutoa huduma iliyokuwa ikitaka taasisi kuwa na ubunifu
ama wa kuiga (adoption) au asili (origin) na ambao haujawahi
kufanyika hapa nchini na ubunifu huo uwe umeleta tija katika utoaji
huduma eneo la kazi.
Katika
tuzo hii MNH imeshinda kwa kubuni njia mbadala ya kulea watoto
waliozaliwa kabla ya wakati
(njiti) kupitia njia ya KANGAROO. Ubunifu huu uliigwa kutoka nchi za
Afrika Magharibi na Afrika ya Kusini ambao walifanya utafiti kwa
kumsoma KANGAROO anavyolea watoto wake akiwa amewakumbatia na kuonyesha
mafanikio makubwa. Kwa misingi hiyo walionekana kufaulu
ambapo vifo vya watoto waliozaliwa kabla ya wakati vilipungua
ukilinganisha na wale wanaolelewa kwenye incubators. MNH ilianza mpango
huu mwaka 2002 na tayari umeonyesha mafanikio makubwa sana ambapo tayari
Hospitali ya Lutheran Hydom iliyoko Arusha nayo imefundishwa
na watalaam wetu kutumia njia hii nayo ikafanikiwa.
Tuzo
ya pili iliyonyakuliwa na MNH ni tuzo ya banda bora kuliko yote wakati
wa maonyesho ambayo
vigezo vyake pamoja na mambo vigezo vingine ni uwezo wa washiriki husika
kujua taaluma yao, uwezo wa kuelezea huduma zinazotolewa na taasisi
wanayofanyia kazi, unadhifu katika banda na huduma bora kwa wateja.
Maonyesho
ya Wiki ya Utumishi wa Umma yalijumuisha taasisi 84 zilishiriki
kushindania tuzo
nne ambazo ni (Tuzo ya Ubunifu, Tuzo ya Taasisi/Wizara Inayosimamamiwa
kwa Mjibu wa Utawala Bora, Tuzo ya Uwezeshaji Akina Mama, Tuzo ya Mpango
wa Wafanyakazi Wanaoishi na VVU Mahali pa kazi. Aidha kati ya taasisi
hizo ni taasisi 42 ambazo zilishindanishwa
kwenye Tuzo ya Tano ya Banda Bora.
Kwa
misingi hiyo, MNH imezigaraza taasisi 42 zilizojitokeza kugombea nafasi
hiyo ikiziongoza
ambapo tuzo hutolewa kwa washindi wa kwanza hadi wa tatu. Aidha MNH
imeziongoza pia 84 kwenye nafasi ya kwanza kwenye tuzo ya ubunifu. Hii
inadhihirisha MNH ipo juu taasisi hizi haziiwezi, haikamatiki. Katika
tuzo ya Taasisi/Wizara Inayosimamamiwa kwa Mjibu
wa Utawala Bora, MNH imepata nafasi ya 8 kwani kila tuzo imetoa fursa
angalu ya kutambua taasisi 10.
Fuatilia habari katika picha:
Dkt. Bashir Nyangasa, Daktari Bingwa wa Upasuaji Moyo akifurahi baada ya kukabidhiwa tuzo
ya Ubunifu
Baada
ya kupata tuzo mbili. Kutoka kushoto ni muuguzi kutoka chumba maalum
cha kujifungulia
Anna Danfold ambaye alikuwa akielezea dakika ya dhahabu ya kuokoa maisha
ya mtoto mara tu anapozaliwa. Anayefuatia ni Muuguzi Rose Silaa ambaye
ni Mkuu wa Kitengo cha Utunzaji wa Watoto kwa Njia ya Kangaroo
akionyesha mtoto anavyotunzwa kwa njia hiyo.
Wakashindwa kuzuia furaha zao hapa Washiriki wa MNH wakasakata dansi baada ya kupokea
tuzo mbili
Wakapata picha ya pamoja kabla ya kuelekea Muhimbili kukabidhi kikombe kwa Mkurugenzi
Mtendaji wao aliyewatuma
Wakawasili Muhimbili kwa mbwembwe
Juu na chini ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili akipokea vikombe
kutoka washiriki wa maonyesho. Juu ni Muuguzi Nemganga Kizegha na chini Dkt. Bashir Nyangasa
Msitari wa mbele ni baadhi ya Wakurugenzi wa MNH kwa pamoja wakiwa na nyuso za furaha
katika picha ya pamoja na baadhi ya washiriki
Mkurugenzi wa Teknohama Bw. Modou Gaye akipokea tuzo hizo na kuyaweka Ofisi ya Mkurugenzi
Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili