Tafuta/Search This Blog

Wednesday, February 20, 2013

SBP ndani ya Kisiwa cha UKEREWE.

Hapa taratiibu chombo kikiondoka Mwanza na mandhari ya Mwanza kutokea kwenye ziwa Victoria. 
The really meaning of Rock City as seen from Lake victoria.


Ndani ya chombo (Nyehunge). Hii nisehemu ya mizigo na magari. Chombo hiki kinaweza kubeba malori kama mawili na mizigo na abiria pia.


Kaka Gee chomboni, hapa ni kwa nje.

Ndani ya chombo sehemu ya kukaa abiria.
Visiwa vidogo njiani.

Kisiwa cha Ukerewe kinavyoonekana kutoka kwenye maji.

Hiyo ni meli ya serikali inayofanya safari za Mwanza - Ukerewe - Mwanza. Inaitwa CLARIUS. 

Ndani ya kisiwa cha ukerewe, hapa ni Nansio. Barabara hazina magari mengi ila pikipiki na baiskeli ni nyingi.

Usafiri wa Bodaboda chap chap.

Jengo la Halmashauri ya wilaya ya Ukerewe. Ni zuri kwa kweli na safi pia.


Kanisa Katoliki la Nansio.

Hapa ni mtaani. Huku mitaa imepangwa vyema, bado hawajaanza kujenga kwa vurugu.

Bukongo.

Bandari ya Ukerewe hiyo.

Nansio hapa
Haya tunarudi Mwanza na hapa ni Mwanza International Fish Market Mwaloni.

Hayo ndio yaliyojiri huko kisiwani.

Haya ndio mambo ambayo unahitaji kuyafahamu kuhusu Ukerewe.
  •  Kisiwa cha ukerewe kina ukubwa wa kilomita za mraba 530.
  • Ukerewe kama wilaya inaundwa pia na visiwa vidogo vidogo 38.
  • Kutoka Mwanza hadi ukerewe ni umbali wa kama kilometa 45 ila vyombo vilivyopo vinatumia takribani masaa manne kusafiri umbali huo.
  • Inasemekana kisiwa hiki kimezalisha wasomi wengi sana hapa Tanzania. Kwa taarifa ambazo nimepewa na mtu (sio lazima uamini na mimi sina jinsi ya kuzidhibitisha) kisiwa hiki kimetoa maprofesa 70.
  • Hiki ndio kisiwa kikubwa zaidi kilichopo ndani ya bara Africa. (inland island)
  • Kuna Matatizo mengi sana ya ardhi kwenye kisiwa hiki hadi inaonekana kama watu ni wengi kuliko ukubwa wa kisiwa.
  • Kama kuna lingine unalifahamu unaweza ukalituma ili tulifahamu.

Plan to visit Ukerewe, you wont regret.



No comments: