Tafuta/Search This Blog

Sunday, July 18, 2010

Moshi tena...


Nilipata nafasi ya kuutembelea mji msafi wa Moshi weekend hii. Nilipokuwa kwenye kituo chao cha basi(bus terminal) ambayo kwa kweli ni ya kisasa, nilipiga hii picha. Nikagundua kitu kimoja kwamba maaskari wa usalama barabarani ndio wanaoshughulika pia na kuyapanga mabasi hapa kituoni na kuhakikisha hakuna matatizo yeyote yanayofanywa na madereva wa mabasi. Hii niliipenda. Lakini pia nikaona jambo jingine ambalo dada yangu Subi ataniunga mkono kwamba matangazo ya biashara (mabango) yamekuwa mengi sana. Kwa upande huu niliopiga picha tu nimeyahesabu yako 9!! Inawezekana kufanyika kitu cha kuyapunguza ili miji yetu ipendeze zaidi?? Nawakilisha!!

1 comment:

Subi Nukta said...

Ni kweli, hayo mambango ni aina moja ya 'uchafu' kwa kuwa yapo 'shaghalabaghala', laiti wangeyaweka katika mpangilio maalumu kama vile kulipia kamuni itakayotengeneza 'scrolling ads' ingevutia sana na kuacha uoto wa asili ma majengo yakionekana kwa ustaarabu.