Tafuta/Search This Blog

Thursday, June 16, 2011

Siku ya Mtoto wa AFRIKA. (African Child Day)

Yaaaaaaaap! Emmanuel: Mtoto kamili wa Africa.




Kutoka kushoto ni Lukundo, Eliza Mwl Eneza, na Rachel


Watoto tunatani sana Kuoneshwa kuwa wenzetu na wazazi wanatujali sana.... Jali na kupenda watoto kila siku


Wanahitaji kupendwa na KUWAJALI



Hawa ni wa DAR lakini wanawakilisha wale wa Africa


hili ni Taifa la kesho na Keshokutwa.


Thursday, June 2, 2011

IBADA YA SHUKURANI kwa familia ya MSUYA SOLOMON.David huko Muheza Tanga.

Wami hapo. tukiwa safarini kwenda Muheza. Kuanzia kulia ni Enson(Bonge), Paulina (mamaa kitinda mimba), Fadhili (BabaGlory), David(Mwana mpotevu), na Elias (Zee la kusi, au Baba Mchina)


Baada ya kuwasili kwa Mama Muheza Tanga kijiji cha Mdote.




Mama mzaa chema akimshukuru Mungu kwa Mwanae David aliyepotelea UGHAIBUNI kwa takriban miaka 16. mama alibubujikwa na machozi ya furaha siku hiyo





Mwana Mpotevu akitoa nasaha. alisoma zab 117 katika neno lake la Kumshukuru Mungu.


Enson/Eneza akitoa nasaha za Shukurani mbele ya waumini wa TAG Muheza



Familia yote

Kuanzia Kushoto ni Mama, david,Erica, Elifadhili, Elias,Eneza/Enson, na Paulina



Naukwea msandarusi..... Solomon akifundishwa ukwezi na Baba yake mzazi. Historia ya familia yetu inaonesha Babu wetu alikua Mkwezi.....




Tunabadili pozi


Watoto wote wa familia ya Mzee Solomon Msuya. hatujawahi kukutana hivi yapata miaka 20 iliyopita. Angekuepo marehemu Baba yetu tungekutana wooooooooooote.

Asante yesu kwakuwa umwema.
Mwaka 1995 Kaka yetu mpendwa David alisafiri kwenda masomoni Ukraine ktk nchi za Kirusi. alifanya masomo yake ya kompyuta na baadae kulowea huko. alioa huko na anaishi na mtoto wa kirusi Shem Hellen. tulimwomba Mungu sana amrudishe bila mafanikio. Kumbe alikua anajipanga kutia timu home. Juzi tar 19 May 2011 alitusaprizi kwani alipiga simu akisema nipo kipawa. haikua rahisi sana Kuaminimwacho. ila kweli alikua amerudi. imepita miaka 16 toka aondoke. lakini tumepata nafasi ya kumshukuru kwa pamoja....

......jina la Bwana libarikiwe...