Tafuta/Search This Blog

Thursday, March 29, 2012

Siasa au matusi??



Hawa ndio wanasiasa wetu na hizi ndio kampeni zetu! Anayeongea hapo ni mwanamume mwenye mke nyumbani na ana watoto na pia chama chake kimemuamini kumtuma kuja kuongea kwenye kipaza sauti kwenye uwanja huo. Lakini jambo kubwa zaidi ni kwamba mtu huyu pia anakaa kwenye chombo kikubwa cha kutunga sheria hapa nchini, BUNGE.

Nimesikitika sana kwa sababu mwanasiasa anajitapa kwenye jukwaa kwamba yeye ana MATUSI. Kama chama kina watu wenye umri mkubwa na wameona hii naamini hawatakaa kimya, lakini kama ni kweli kwamba ni genge la wahuni then watakaa kimya na kufurahia haya ambayo kuna siku watayatolea hesabu mbele za waTanzania.

Namalizia kwa kusema, biblia inasema,"Msidanganyike, mazungumzo mabaya huharibu TABIA njema."

Tuesday, March 27, 2012

Rehema's Send off party.

Jina lake ni Rehema Rashid Mwevirah, kutoka Iringa na anaishi Arusha. Jumamosi ilikuwa ni siku ambayo wazazi wake walimuaga ili aoelewe na kijana Mwaluko Chilewa pia wa Arusha. Hizi ndio picha za matukio katika sherehe hiyo ya kumuaga binti huyo iliyofanyika katika viwanja vya kanisa la Kirumba Valley christian Center Mwanza.

Rehema na mpambe wake Beatrice.

Kijana Mwaluko Chilewa.

Mpambe wa Mwaluko kaka Jadon Kuyokwa akimweka sawa.

Shemeji mkubwa mama Gratian akiwa na vijana wake muda mfupi kabla ya kuelekea kwenye sherehe.

Baba na mama Gratian, wenyeji wa Chilewa na familia yake.


Wazazi wa Chilewa pamoja na kaka mkubwa Humphrey.


Makabidhiano ya sanduku kutoka kwa shangazi kwenda kwa shangazi.

Sanduku linapigwa ukaguzi kama linafaa.

Sanduku limefaa na familia ya Rehema kupitia kwa shangazi mama Lyabandi wamekubali kumtoa binti yao.

Mama mdogo wa Rehema, Pastor Tina akiwa na mama mzazi wa Rehema.

Kapu la wamama hilo.

Wamama wabeba kapu wakiwapongeza mama wa Rehema.

Wazazi wa Mwaluko Chilewa.

Mzee wa kanisa mama Masalakulangwa akishusha sala.

Vijana wa sherehe wakisubiri dada rehema awaone.

Hatimaye amepatikana, looking good!

Misosi time.


Familia ya Rehema.

Blanketi kwa mama.

Mwakilishi wa kanisa la Calvary Arusha akitoa neno la shukrani baada ya mambo yote.

Mapozi kidogo...

Mzee Haule kaimalizia sherehe kwa sala.

Kaka Baraka Chilewa pia alikuwepo.

Mkuu Salum na mkewe Isabela wakipose kwa picha.

Mama Gratian na dada Jane.
Rehema ndio huyoo.


Mission accomplished. Arusi itakuwa tarehe 31 March Calvary Temple Arusha. Mnakaribishwa!.

Monday, March 26, 2012

Kijana wetu Joseph Msami awa MORANI.

Hatimaye kijana wetu amekuwa Morani baada ya sherehe za kimila zilizofanika huko mkoani Manyara wilaya ya simanjiro kijiji cha Terat.

Kijana wetu Joseph Msami akiwa katika mavazi rasmi baada ya kuwa Morani.


Hapa Kijana wetu alihudhuria moja ya sherehe ya kimila ya LAION yaani vijana wadogo ambao hawajatahiriwa.

Thursday, March 22, 2012

Praise and Worship on 9th April at Kigogo TAG.



Kikundi cha WANAFUNZI (Student Club) wa kanisa la TAG Kigogo Dar es Salaam wameandaa ibada ya Kusifu na Kuabudu tar 9/4/2012 katika eneo la Kanisa ili kumsifu na kumwabudu Mungu wetu.

Tafadhali Ungana nao ili KUMWINUA MUNGU......

Monday, March 19, 2012

Vurugu za Kirumba Mwanza Jumamosi 17th March 2012





Jamani hiyo ndio hali halisi iliyotokea mitaa ya Kirumba jumamosi iliyopita!

Video ni kwa hisani ya kaka yangu Musa Nduta Dede.