Tafuta/Search This Blog

Tuesday, August 28, 2012

Papaa On Tuesday......Maisha Ya Pembe Tatu Ni Kwazo la Maendeleo Kwa Mkristo-2

 

Niwasalimu Kupitia jina la Bwana wetu Yesu Kristo.

Wakati Zoezi La Sensa Limeanza nilibahatika kuhesabiwa siku ya Jumapili na kwa dakika zisizozidi 10 nilishaongea mengi na aliyekuwa Karani Wa Sensa Kwenye Nyumba yetu. Kati Ya Mambo tuliyoongea kidogo ni Mfumo wa Maisha tuliyoamua kuishi Watanzania am Wakristo Kwa Ujumla Wao. Na Katika Mazungumzo nilikuja baini kumbe Jamaa ananifahamu na ni Msomaji Mzuri wa Blog Hii akanikumbusha Papaa On Tuesday ambayo ilimbadilisha namna ya Kuwaza ambayo ilibidi niisome tena siku ya Jumapili Usiku kuona kile ambacho kiliandikwa mwaka Juzi kilikuwa ni nini hasa.

Niwashukuru Wasomaji wa Blog na Marafiki wa Facebook waliokuja kwenye Presentation Ya Papaa On Tuesday niliyofanya Live Pale VCC Jumamosi hii ya 'Think Differently and Make a Difference". It was Awesome sana Mungu awabariki.

Kati ya Mambo unapaswa to think Differently and Make a Difference ni mfumo wa maisha ya pembe tatu tunayoishi nikiwa na maana, 1. Unapolala (Nyumbani) 2. Unapofanya shughuli zako (Kazini ama shuleni) 3. Unaposali (Kanisani ama Fellowship).Kuna watu wakiamka asubuhi wanajiandaa kwenda kazini ama darasani, wakitoka wanaenda labda kanisani ama fellowship kisha wanarudi nyumbani kulala, kesho yake wanaamka wanarudia mzunguko huo huo.

Nichangamoto kubwa sana ya kizazi hiki ambacho kila mtu anataka kuwa "mjasiriamali" wa namna moja ama nyingine ama mtu unakusudia kuongeza kipato chako cha fedha then una maisha ya pembe tatu. Mtu yeyote unayemuona either amefanikiwa kwa namna moja ama nyingine lazima huyu mtu anamizunguko zaidi ya hiyo uliyonayo. Usitafute mchawi mchawi ni wewe mwenyewe.
Siku Moja Swahiba Prosper Mwakitalima aliniambia niambia "Hakuna tusi baya kama kusema haiwezekani, then ukakuta kuna mtu amefanya". Kati ya vitu ambavyo tunavyo na hatupendi kuvitumia ni ubongo, mfumo wa makuzi na malezi tuliyokulia umetusababishia mtu mwingine awaze kwa niaba yetu sisi tuchukue mawazo yake, huwezi kuwa msomi mwenye akili za kutosha na ubunifu wa hali ya juu kwa kutegemea "madesa", notes za handout na past papers, ndio maana waliokuwa wazuri "kukariri" darasani kwenye maofisi huku ni wengine ni vituko. Mimi ni mwandishi lakini nina taaluma yangu,ninapoandika na kusababisha hii Blog iwe na mambo ya maana iwe current sio sababu ya maombi, sababu kubwa am working hard for this, nachelewa kulala sababu ya kuwaza, inanipasa kusoma sababu ya hii, inanigharimu muda ili wewe usome, inanigharimu fedha ili mtu mmoja apone, we will never be the same my dear. Chukia mizunguko mitatu kwenye maisha yako.

Unaweza pata wapi mawazo ya biashara kwa maisha ya pembe tatu, unaweza pata wapi wateja ama network ya watu kwa maisha ya pembe tatu, unaweza fanya jambo gani kwenye Jamii kwa maisha ya pembe tatu??kila utakachokuwa unaongea ni Kazini kwetu, Kanisani kwetu, kwenye TV kwenye nini sijui...Wake Up. Kwa taarifa yako kuna watu wa rika lako wanafanya mambo makubwa wewe ukiwa bado unawaza nini cha kufanya. Kuna wanafunzi kama wewe wameanza kujiongezea kipato chao, kuna wafanyakazi kama wa ngazi yako hawategemei mishahara yao..tatizo kubwa sisi tukitoka kazini haooooooo, kanisani, tukitoka kanisa haooooooo kulala, get me well kuna wengine hata maofisini mwao ama shuleni ama vyuoni mwao ama kanisani kwao hawaoni kama hao ni Opportunity kwenye maisha yao.

Kuna wengine mpaka sasa hawajaoa wala hawajaolewa si kwa sababu Bwana hajataka ila Mfumo wao wa maisha una walostisha, kuna wengine mpaka sasa hawajapata kazi si kwa sababu Bwana hajataka ila mfumo wapembe tatu unawalostisha, kuna wengine mpaka sasa biashara ni ngumu sababu ya mfumo wa pembe tatu. Ninaamini tumeumbwa tofauti, lakini through friends ndipo unaweza gundua kile ambacho Mungu ameweka kwenye Maisha yako pia. Aliyenipa wazo la kuwa na Blog is my friend Weda Ringo..she saws something in me akasema Papaa you Can do It, but wote hatukujua on "how to do" kwenye Nia pana njia, leo hii Blog imesimama, Blog imekuwa chanzo changu cha fedha, Blog imekuwa Msaada kwa Watanzania wenzangu na Ulimwengu kwa Ujumla. Blog imekuwa madhabahu ya wengine kufunguliwa. Nilipoanza Blog sikujua kama nitakuwa na "Papaa On Tuesday" lakini Mungu akawapa akaweke idea ya mimi kuwa na "Papaa On Tuesday", leo kuna wazo lingine ninalo ambalo pia litabadilisha mtazamo wa Blog hii, siangalii leo, wala mwaka huu ninatazama miaka mitano ijayo.Na kile Mungu anasema kuhusu Blog hii.This will be the most Popular Christian Blog hapa Tanzania si kwa sababu ya mapicha picha au sababu ya uandishi I came to realise this blog is not mine, last week nimepokea testmony za kutrosha mpaka nikaogopa kuwa kupitia Blog hii kuna watu wamepona kabisaaaaaa magonjwa yao, kuna watu wanainuliwa kupitia blog hii, kuna watu wanasubiri Jumanne Kusoma Papaa On Tuesday sababu anajua kuna Kitu kutoka Madhabahu hii. Nimejifunza kumsikiliza aliyeniajiri katika kazi hii na kuweka hizi idea na gifts ndani yangu anataka twende wapi kupitia blog. Is not only about writings lakini how many people wamekuwa transformed wamekuwa inspired kupitia hapa, we need to live a life with impact.

Lakini haya yote is not all about me kuna watu wananiombea kuna watu wananipa Ideas. Let me be Honesty Mwanzo ni mgumu sana, na kuna watu wanapenda wengine wafanye wao wanavyodhani ni vizuri, nimekutana na watu wengi sana wanatamani Blog yangu ile kivileeeeeeeee, wengine wanaongea rangi mbaya, wengine wanaongea lugha ninayotumia, wengine wanaongea kuna picha nyingiiiii, the simplest thing that I always do, ninasikiliza then ninachambua kina go ahead ya ndani ama lah kama sio napiga chini wazo kama unaona unaweza anzisha Blog yako iwe inavyotaka kuwa, usikate tamaa kwenye maisha huwezi jua nini kitakutoa kwenye maisha yako.

Ukiona mwezi mzima unamaisha ya pembetatu tafakari kisha chukua hatua. Kila siku ya Mungu lazima nikutane na watu kwa ajili ya kubadilishana mawazo na kila siku ninapata mawazo mapya kupitia watu kupitia vitabu mbalimbali.

Think Differently and Make a Difference.
...//Papaa
0713 494110
samuel_sasali@yahoo.com
posted by 0718817706

Thursday, August 23, 2012

Ustaarabu kwa tafsiri yetu...

Unashindwa kabisa kuelewa!! Mtu katoka huko alikotokea akaamua kwa moyo wake wote kuweka tangazo la muziki wa Taarabu juu ya alama ya barabarani! Hivi ni kweli kwamba hii ngozi yetu ina matatizo?? Hivi ni kweli huyu mtu hakuona umuhimu wa hiyo alama kuwepo hapo?? Hivi ni kweli kwamba Taarabu ya TOT ni muhimu kuliko watumiaji wote wa barabara hii kubwa?? Anhaa hii ndio tafsiri ya usataarabu kwetu, unaangalia jambo linalokuhusu tu, mengine  unaachana nayo.
Picha hii imepigwa kwenye jucton ya Mwaloni katika barabara ya Makongoro, Jijini Mwanza.

Wednesday, August 22, 2012

STUDY IN UKRAIN WITH LOW COST BUT HIGH QUALITY EDUCATION PROVISION


Overseastudies Agency is an unique organization under Ukrdasprom with high reputation for overseas studies. Working together with Dasprom, It recruits students with qualification to study in International universities in abroad. We recruit students to undergo Bachelors, Masters, and PhDs. We have pleasure to welcome you for new programs of university studies, undergraduate & postgraduate in Ukraine. Its a tremendous opportunity that could be yours by choosing studying at the universities with low fees payments but high quality education provision. Ukrdasprom has registered in Ukraine with Reg.14801020000047850. It links as an agent for many universities.
More than 130 in different specialties like medicine, pharmaceutical science, engineering, economics, computer science, arts etc. Studies in Ukraine are in either in English or in Russian language, for those who will find their desire courses in English, will begin first course directly, but for those that their courses are not available in English will have to begin by preparatory course in Russian language for duration of six to nine months.
Study in Ukraine may re-assure you that time spent studying abroad does not have to be costly venture.
Overseastudies Agency offer you the perfect opportunity to live, study and travel in another country during a holidays.
By studying in Ukraine you can have a chance to:
·  Have a funny challenging experiences
·  Study at a leading International research university with experts in your subjects
·  Enhance your job opportunities –make your CV stand out from the rest
·  Learn more language skills improve already you have
·  Get to know new cities, countries, and take advantage of trip and travel during holidays
·  Meet variety of people and make international network of friends
·  Acquire life skills including confidence and independence
 
BACHELORS AND MASTRES DEGREES PROGRAMS
Universities provide many profession programs of bachelor degree, some of them are:
·  Medicine
·  Pharmacy
·  Stomatology / Dentistry
·  Pediatrics/Nursing
·  Biomedical/chemical Engineering
·  Automobile engineering
·  Road and Highways construction engineering
·  Computer Engineering and Information Technology
·  Aeronautical and Aviation Engineering
·  Flight, Navigation and Piloting
·  Machinery Construction Engineering
·  Mechanical and Electrical Engineering
·  Economics, Accounting and Business Administration
·  Tourism and Hotels Management
·  Journalism and Judiciary Laws
·  Ecology/Mining industry and Environmental Technology
·  Theater, Music Art
·  Agronomy
·  Oil and Gas Engineering
·  Marine and sailing etc.
 
Master Degrees in English language Includes:
·  Economics
·  Management
·  Computer systems & Networks
·  Accountancy
·  Medicine
 
CONTACT US
UKRAINE Office 82/1 Kharkov Sumskaya
Tel:
+380 935348972
+380970857571
Fax: +380577004958
Email:dsm@europe.com
info@dasprom.com.ua

TANZANIA Correspondent:
Tel:
+255718817706
+255784494906
Email:enson79@yahoo.co.uk
KENYA Correspondent
Penina N. Mwikali
Tel: +254724177585
Visit our site now
 

Friday, August 10, 2012

USIKU WA REGINA 9/8/2012 MSASANI BEACH CLUB (MAKUTI)

Siku ya Regina Kokubanza Divas ,..... matukio machache katika picha.. ilikua ni Birthday yake pia.... karibu utazame...
 Regina ktk Pozi la Saluni


 Na Uzuri unachangia


 Mrembo Reginaktk tabasamu la Send Off yake tar 9/8/2012 ambayo pia ni siku yake ya kuzaliwa.


 Pozi
 Mama wazaa hema


 Baba Mzaa chema ndani ya JUMBA


 Keki ya Send Off na Dirthday ya Regina Kokubanza Divas


 Mzee wa Heshima


 Dr. Pracseda.... mgeni aliyependeza kupita wote ( Tathmini ilifanywa na Blog hii)


 Baba mzaa chema akizirudi mbele ya ukumbi huku akisaidiwa na wapambe wake.. mahalah ilikua nzuri


 Bi Regina na Mpambe wake ktk POZIIIII


 Bwana Arusi mtarajiwa na Bi Regina Mr&Mrs to be.. (kama watakavyopendeza katika Arusi yao)


 Tulikula nini?


 Shalom Broz Production (Mitambo)


 Wamependezaje!


 Wosia wa Baba


 Burudani kabambe.. song (Sasa nimehamia Mtaa wa Saba...)


 Kwaito ikisakatwa.... Ilikua raha kupitiliza
Mambo ya Kwaito...
JJ Mwijage, Msuya the Blogger na Sister Hafsa Big Boss...

WAFANYAKAZI A HOSPTALI YA TAIFA MUHIMBILI.
kutoka kulia ni Sr. Lymo, Msuya Eneza, JJ Mwijage. Wa pili Kutoka kushoto ni Sr Letisia na Zainab

Picha na Eneza Msuya wa Shalom Broz Productions
+255718817706 na +255784494906

Tuesday, August 7, 2012

Papaa On Tuesday....Wenye Akili Zao Hunyamaza

Ninakila sababu Za Kumshukuru Mungu Kwa ajili ya Siku hii Ya leo kutupa tena uzima. Ni Matumaini yangu kuwa mgogoro wa Kidiplomasia Baina ya Tanzania na Malawi Utamalizwa kwa Njia Za Kidiplomasia Zaidi Kuliko nguvu.

Mwaka 2010 tarehe 14, September niliandika Papaa On Tuesday yenye Kichwa cha 'Wenye Akili Zao Kimyaa". Nilipokuwa ninasoma Papaa On Tuesday hiyo nikapata Ufunuo Mwingine wa Wakati huu kupitia Ujumbe ule wa Mwaka 2010 uliokuwa unafanana na Mwaka huo.

Kunyamaza ni Silaha mojawapo inayotumika kwenye maisha na style hii haikuanza jana wala juzi. Ukisoma Biblia utaona wakati Yesu amezongwa na Wayahudi wakitaka kumsulubisha na wakimbeza na kumzomea na kuuliza kama kweli ni Mfalme wa Wayahudi, Yesu alikuwa hawajibu chochote alikuwa anajinyamazia Kimyaaaaa. Hata walipomuuliza wale wakuu wa Makuhani kama yeye ni Mwana Wa Mungu...Yesu na akili zake akijianyamazia Kimya.
Si Yesu tu, tazama Rais Mstaafu Mkapa, watu walisema mengi wakasema alifanya biashara Ikulu, yeye ni Fisadi Mkubwa, tulimbeza tukamwambia aibu yake ama aibu yetu, lakini Rai Mkapa alinyamaza Kimyaaaaaaa, Leo hii Mkapa anaonekana ni mtu muhimu kuliko Kiongozi kama Makamba alikuwa anaeongea kila kitu na kila siku akiwa CCM leo yuko wapi Kimyaaaaaa, yule yule tuliyembeza jana leo amegeuka kuwa rafiki, huyu alitumia akili zake kunyamaza kimyaaaa mwingine akatumia kuropoka.
Aliyekuwa Waziri Mkuu Mhe. Lowassa, mara baada ya kupata Kashfa ya Richmond Silaha pekee aliyotumia ni kunyamaza kimyaa, pasipo kujibu chochote. Kwa kunyamaza kwake imeanza kumuonesha yeye ni mtu mwenye akili na uwezo wa namna gani katika kupambana na wale waliokuwa wakimcheka na kumdharau. Leo Watu wale wale waliokuwa wanamuambia ametutia aibu tunasema Bora Lowassa Kuliko Mtoto wa Mkulima.

Hakuna Silaha kali na pengine mbaya kuliko mtu akunyamazie tena akunyamazie ukiwa hujui kwanini Kanyamaza. Kunyamaza ni Ishara ya kudharau, ukitaka kujua unadharauliwa ama lah basi mtu akunyamazie unamuuliza kitu anakutazama tu pengine juu mpaka chini, Unaweza kujiua kabisa. Assume umeolewa, pengine kutokana na matatizo ya ndoa ama shetani kupata nafasi katika ndoa, mwanamke akasaliti ndoa yake yaani aka cheat, uzuri ama ubaya mumeo siku akakukuta live live kabisa na huyo mwingine. Then Mume anaamua kulinyamazia hilo jambo kama halijatokea. Unamuomba msamaha ye anasema its ok na yameisha, ila hakusemeshi, hakuulizi wala hakusalimu. Kama unaroho nyepesi unabeba kilichochako unaenda nyumbani. Walio wanandoa wanajua ingawa wanadai sina experiance hahahaha afadhari unayamaziwe na Mchungaji wa Kanisa lako kuliko unyamaziwe na mpenzio ama mwenzi wako wa Maisha.

Huwezi ipotezea kirahisi inauma sana kunyamaziwa bila kujua hukumu ya Kosa lako bora mtu akuchape akuseme kiishe kuliko akupotezeee.
Kunyamaza wakati mwingine kwenye maisha inakupa sababu ya kujipanga ki-hoja zaidi katika makosa, wenye akili zao huwa wanatulia mambo yanapokuwa yanaenda mrama, kuna msemo unasema watasema mchana na usiku watalala, wenye akilizao wanapokuwa na wakati mgumu hunyamaza,kunyamaza kunamfanya adui yako amalize upesi kuongea kuliko ukijibizana nae, mkijibizana nae inampa nafasi ya kusema na mambo mengine lakini mtu akiongea na akatukana we unajinyamazia mwisho asimaye huamua kunyamaza na yeye.
 

Biblia inasema Mpumbavu akinyamaza huonekana anahekima. Ni heri kuna wakati unyamaze kimyaaaa utakuwa salama zaidi kuliko ukitaka kuongea ukajikuta umeharibu reputation yako uliyoijenga miaka mingi. Kuna Wakati Mwingine tabia ya Kukimbilia Kuongea Kama Yule Baba Wa Jeshi la Polisi, Jambo Kidogo tu anaita Media anavyoongea issue akapigwa na Maswali huwa naona inamdhihirisha  kwa kumuonesha “Real Him” ambayo kwangu naona ni vema akaitunza hiyo personality kwa kunyamaza...hapo wenye akili zao hujinyamazia. 
Nimalize kwa kusema, huwezi wazuia watu kuongea juu ya wewe, wengine wataongea mambo makubwa na mabaya kuhusu wewe, kila ukitaka kujibizana nao ndo inaonesha wewe ulivyo. Kabla hujajibizana nae kumbuka wenye akili zao hutulia kwanza na kijipanga ki-hoja kabla hawajakurupuka. Ukikurupuka tu basi aibu yako inaweza kuwa kubwa zaidi, Kunyamaza ni hekima ndo maana Biblia inasema Mpumbavu akinyamaza anaonekana ana hekima. Biblia kama ilivyosema kila jambo na Wakati Wake kuna wakati Wa Kusema na Kuna wakati Wa Kunyamaza. Usinyamaze tu unapokuwa Umelala, Ila hata pale ulipopaswa wakati mwingine kusema wewe nyamaza.

Kunyamza inakufanya kuelewa wapi ujipange na watu wanakuonaje pia. Huwezi wazuia watu kuongea kuna wanaoongea kwa kuzusha na kuna wanaoongea kwa kuongeza chumvi, lakini kunyamaza inakupa nafasi ya kujipanga. Leo ukifanya makosa either ukateleza katika maisha huwezi wazuia watu kuongea watasema sana aibu yako aibu yetuuu..lakini wenye akili zao?hapo wanayamaza. Kunyamaza kunakufanya ujipange na kuelewa nani yupo nawe na nani hayupo nawe kuna kujitia nguvu pale unapo nyamaza. Ukisoma Bible kuna wakati Daudi aligeukwa na rafiki zake, askari wenzake baada ya kukuta kila kitu chao kimeteketezwa ukisoma bible pamoja na shutuma zote But David Strengthern himself in the Lord. Kwenye maisha kuna wakati wa kunyamaza. Mtu mmoja alisema “There is a voice in every Silence” ukikaa mahali kimyaaaa just alone, wengine ndo tunapataga madesa ya kuongea na watu. Kama mtu mwenye akili timamu lazima kuna wakati wa kunyamaza.
Wakati mwingine kwenye maisha ni vema ukajinyamazia kuliko ukaongea, utakuwa na akili zaidi ukatunza personality kuliko ukasema neno moja likaharibu. Ukitaka kutunza heshima yako sio kila saa na kila kitu lazima uongee, jinyamazie kimyaaaaaa. Kwenye ndoa na mahusiano kumekuwa na kuto kuelewana sababu tu kila mtu hataki kuonewa, huyu akiongea na huyu anaongea, tujifunze kunywa maji na kutoyameza mtu anapokuweka kiti moto. Kukubali kosa ama makosa si kuonesha mapungufu kuliko ukiendelea kuongea ndo kuonesha hayo mapungufu uliyonayo kwa wenye akili zao huwa wanakunyamazia tu then wanaongea pembeni. Wanaume tumekuwa na ubabe wa kubeba maamuzi, wengine kutokana na vipaji vyetu vya kuongea kila Kosa tunataka Kujustfy kuwa ni a,b,c kwanini tusijifunze kunyamaza kama wenye akili?

Kuna Watu wanaongea sana, Wanaongea Kwa Maandishi Wanaongea na Maneno, sembuse siku hizi kuna facebook na Tweeter na zingine basi jambo lolote la kwake mtajua, akipata hela mtajua, akipata mchumba mtajua, akiachwa mtajua, akilala njaa mtajua, yaani chochote Cha Kwake Mtajua sababu ya Kuongea sana.

...//Papaa
0713 494110

Saturday, August 4, 2012

Hii imetusikitisha sana....

Ajinyonga baada ya kufiwa na mtoto Send to a friend

Salum Maige,Geita

MWANAMKE aliyefahamika kwa jina la Monika Mapoli[22],Mkazi wa Kijiji cha Isima kata ya Butundwe wilayani Geita, amekutwa amejinyonga juzi kwa kutumia kipande cha nguo karibu na Ofisi ya Mganga Mkuu Wilaya ya  Geita.

Taarifa za mashuhuda wa tukio hilo zilisema kuwa Mapoli alichukua uamuzi huo baada ya kufiwa na mtoto wake Jumanne Philimo(2) aliyekuwa amelazwa wodi namba moja  katika Hospitali ya Wilaya ya Geita akipatiwa matibabu.

Ilielezwa kuwa baada ya mtoto  huyo kufariki dunia,mama huyo  alitoweka wodini na kwenda kusikojulikana hadi alipokutwa amejining’iniza kwenye mti uliopo jirani na Ofisi ya Mganga Mkuu wa wilaya hiyo Dk Omari Dihenga.

Mmoja wa mashuhuda wa tukio hilo Petro Majiasi aliyekuwa kwenye wodi hiyo alisema chanzo cha kifo cha  mtoto huyo  ni huduma duni za matibabu zinazotolewa hospitalini hapo ambapo tangu mtoto huyo   alipolazwa hakupatiwa matibabu hadi mauti yalipomkuta.

Akizungumzia tukio hilo, Mganga Mfawidhi wa Hospitali hiyo Dk.Nelson Bukuru, alithibisha kumpokea mtoto huyo saa 7 mchana juzi akisumbuliwa na homa ya mapafu lakini kutokana na uhaba wa dawa za kutibu ugonjwa huo walilazimika kumlaza  wodi ya watoto ili taratibu za kupata dawa ya ugonjwa huo zikifanyika.

Alisema kabla ya kupatikana kwa dawa hizo mgonjwa alifariki dunia akiwa amelazwa wodini chini ya uangalizi wa wazazi wake na katika hali ya kusikitisha kulipopambazuka walikuta mwanamke huyo akiwa amejinyonga na kuning’inia juu ya mti ulio ndani ya hospitali hiyo.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita Leonard Paul alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba jeshi la polisi  linaendelea na uchunguzi ili kubaini chanzo.

-Mwananchi


Neno letu.

Uchungu wa mwana aujuaye ni mzazi. Huyu mama inaonesha alipata uchungu mkubwa sana kwa kuona kwamba sehemu alipompeleka mwanaye ili apate msaada hakuupata na ikapelekea kifo cha mwanaye mpenzi. Inasikitisha kwamba alikata tamaa na kwakuwa mara nyingi pia kwenye hivi vituo vya afya watuhawana elimu ya ushauri nasaha hivyo aliishia kujinyonga. Hatujafurahishwa kabisa na jambo hili sisi kama watanzania na pia kama wanadamu tunaothamini sana maisha!!

Thursday, August 2, 2012

HOTUBA YA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA MH. JAKAYA MRISHO KIKWETE KWA WAHARIRI WA VYOMBO VYA HABARI....

Ndugu Wananchi;
Naomba nianze kwa kuomba radhi kwa kutoa hotuba ya mwisho wa mwezi wa saba, leo tarehe 01 Agosti, 2012 badala ya jana tarehe 31 Julai, 2012. Hii ni kwa sababu ya msiba uliotukuta katika familia na mimi kwenda Lindi kushiriki maziko ya marehemu wetu. Tofauti na miezi iliyopita leo, pamoja na hotuba ya kawaida ya mwisho wa mwezi nimetoa fursa kwa Wahariri wa vyombo vya habari nchini kuniuliza maswali nami kujibu. Kwa upande wangu nina mambo matatu ambayo nitayazungumzia leo.

Ajali ya Kuzama kwa Meli ya MV SKAGIT
Ndugu Wananchi;
Jambo la kwanza ni ajali ya Meli ya MV SKAGIT iliyotokea tarehe 18 Julai, 2012. Meli hiyo ilikuwa na watu290, wakiwemo mabaharia 9, abiria watu wazima 250 na watoto 31. Juhudi za uokoaji zilianza mara baada ya taarifa ya kuzama kwa meli hiyo kupatikana. Maofisa na askari wa JWTZ, Polisi na KMKM walishiriki pamoja na meli na watu binafsi katika uokoaji. Waokoaji walifanikiwa kuwapata ndugu zetu 146 wakiwa hai na maiti 126 hadi tarehe 27 Julai, 2012. Kwa maana hiyo basi, watu 18 hawajulikani walipo na inahofiwa kuwa nao pia hawako hai. Huenda wamezama pamoja na meli au walizama baharini lakini miili yao haikuweza kupatikana.

Ndugu Wananchi;
Napenda kutumia nafasi hii kurudia kutoa mkono wa rambirambi na pole nyingi kwa wale wote waliopoteza ndugu, jamaa na marafiki katika ajali ile. Nampongeza sana Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mheshimiwa Dkt. Ali Mohamed Shein na viongozi wenzake wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) kwa kazi kubwa na nzuri waliofanya kuongoza juhudi za uokoaji pamoja na huduma walizotoa kwa waliokolewa, waliojeruhiwa na waliofariki. Kwa wale ambao walikuwa wenyeji wa Unguja na Pemba, SMZ ilitoa sanda na usafirishaji wa maiti mpaka makwao kwa mazishi. Kwa wale wasiokuwa na ndugu Serikali ilibeba jukumu la kuwazika kule Kama, Kusini Unguja.

Natoa pongezi za pekee kwa wale wote walioshiriki katika uokoaji kwani juhudi zao ziliwezesha ndugu zetu wengi kusalimika na maiti nyingi kupatikana.

Ndugu Wananchi;
Kutokea kwa ajali ile kumetonesha jeraha la huzuni, majonzi na mashaka makubwa yaliyolipata taifa letu miezi 11 iliyopita kufuatia ajali ya kuzama kwa meli ya MV Spice Islander. Katika mkutano maalum wa Baraza la Usalama wa Taifa niliouitisha tarehe 20 Julai, 2012 kuzungumzia ajali ya MV SKAGIT tulifanya mapitio ya utekelezaji wa maagizo yetu ya mkutano wa tarehe 11 Septemba, 2011 kufuatia ajali ya MV Spice Islander. Kwa ujumla tumeridhika kuwa utekelezaji umekuwa mzuri kwa upande wa mamlaka zinazohusika na usafirishaji majini yaani SUMATRA, Zanzibar Maritime Authority na mamlaka za Bandari za nchi zetu mbili. Ushirikiano baina ya mamlaka hizo sasa ni mzuri kwa mambo yote muhimu ambayo Baraza liliagiza wafanye hivyo. Pamoja na hayo Baraza limetaka ushirikiano huo uzidishwe na kuimarishwa.

Kwa mfano, Baraza limefurahishwa na kupongeza kitendo cha mamlaka hizo kutumia Dar es Salaam Maritime Institute kwa ushauri kuhusu ubora wa meli na huduma za usafirishaji majini. Baraza limeagiza vyombo hivyo viwe na hadidu za rejea zinazofanana kwa vigezo vya ubora ili nchi yetu iwe na viwango vinavyofanana vya ubora wa meli na huduma za usafirishaji baharini kwa pande zetu mbili za Muungano. Bahari ni moja na vyombo vinahudumia watu wale wale, kuwa na vigezo tofauti vya ubora wa meli na viwango vya huduma ni jambo lisilostahili kuwepo tena, ni la hatari. Baraza pia limeagiza pawepo na ukomo wa umri wa meli zilizokwishatumika zinazoruhusiwa kutumika hapa nchini.

Aidha, Baraza limerudia kuagiza pawepo na usimamizi makini zaidi kuhusu upakiaji wa mizigo na abiria. Mamlaka husika, yaani SUMATRA, ZMA na maofisa wa bandari wahakikishe kuwa uwezo wa meli uliohakikiwa na kutambuliwa unaheshimiwa ipasavyo. Pia, meli zikaguliwe mara kwa mara na vigezo vifanane.

Ndugu Wananchi;
Pamoja na hayo, Baraza la Usalama wa Taifa limeona kuwa wakati umefika kwa Serikali yetu kuwa na Coast Guards, yaani kikosi maalum cha uokoaji na usalama majini. Aidha, Baraza limetaka hatua za makusudi zichukuliwe kuimarisha KMKM na Police Marines. Mwisho, Baraza lilipongeza uamuzi wa SMZ wa kuunda Tume ya kuchunguza ajali ile kama ilivyofanya wakati wa ajali ya MV Spice Islander.

Utafutaji na Uchimbaji Gesi Nchini
Ndugu Wananchi,
Jambo la pili ninalopenda kulizungumzia leo ni kuhusu maendeleo ya sekta ya gesi asili nchini. Juhudi za kutafuta mafuta nchini zilianza mwaka 1952 na mwaka 1954 wakati kampuni ya BP ilichimba kisima cha kwanza kule Mafia. Bahati mbaya kisima hicho hakikuzaa matunda yaliyotarajiwa na juhudi za utafutaji mafuta zikafifia kabisa mwanzoni mwa miaka ya 1960. Miaka kumi baadae, juhudi hizo zilianza upya na kuendelea kwa kiwango na kasi za namna mbalimbali hadi sasa. Katika miaka ya hivi karibuni juhudi zimekuwa kubwa na kuhusisha makampuni kadhaa ya kimataifa yakiwemo makubwa na madogo.

Ndugu Wananchi;
Tangu mwaka 1954, mpaka sasa visima 61vimechimbwa, kati ya hivyo, gesi asili imegunduliwa katika visima 22, visima 14 vya nchi kavu na maeneo ya maji mafupi na visima 8 vya bahari ya kina kirefu. Hatujabahatika kupata mafuta lakini tumefanikiwa kupata gesi asili katika maeneo kadhaa baharini na nchi kavu katika mikoa ya Mtwara, Lindi na Pwani.

Kwa mujibu wa taarifa zilizopo kutokana na visima vilivyochimbwa mpaka sasa, akiba ya gesi asili iliyopo nchini inakadiriwa kuwa kati ya futi za ujazo trilioni 25.4 – 28.9. Yapo matumaini makubwa ya gesi nyingi zaidi kugundulika katika miaka michache ijayo. Hii ni kutokana na ukweli kwamba shughuli za utafutaji mafuta na hasa gesi baharini zilizoanza mwaka 2004 kukiwa na kampuni moja sasa zipo 18. Baada ya ugunduzi wa kwanza wa gesi mwaka 2010, shughuli za utafutaji sasa zimepamba moto na zimekuwa na mafanikio. Naamini gesi nyingi zaidi itaendelea kupatikana.

Fursa za Maendeleo
Ndugu Wananchi;
Kwa kiasi cha gesi asili kilichokwishagunduliwa na kwa matumaini yaliyopo ya gesi zaidi kupatikana kunaifanya Tanzania kuwa moja ya nchi za kutumainiwa duniani kwa upatikanaji wa gesi asili miaka michache ijayo. Hali hiyo inaipa nchi yetu fursa kubwa ya kuweza kujiletea maendeleo makubwa ya kiuchumi na kijamii muda si mrefu kutoka sasa.

Gesi asili ni rasilimali inayoweza kutumika kuzalisha mbolea na hivyo kusaidia katika kuendeleza kilimo nchini kwa kurahisisha upatikanaji wake na kuwa ya bei nafuu. Gesi asili inaweza kutumika kuzalisha umeme na hivyo kuiwezesha nchi kupata umeme wa kutosha na kuwepo ziada ya kuuza nje. Hivi sasa, katika gridi ya taifa megawati 350 za umeme zinatokana na gesi asili na hata lengo letu la kuzalisha megawati 3,500 ifikapo maka 2015 tunategemea zaidi gesi asili kuwezesha hilo kutimia. Ujenzi wa bomba la gesi kutoka Mtwara kuja Dar es Salaam una shabaha hiyo.

Ndugu Wananchi;
Vile vile, gesi asili inaweza kutumika kutoa nishati viwandani badala ya kutumia mafuta na hivyo kupunguza gharama za uzalishaji. Watu majumbani wanaweza kutumia gesi asili kupikia hivyo kupunguza matumizi ya umeme, mafuta, mkaa na kuni. Inapunguza gharama za maisha na kusaidia kuhifadhi mazingira kwa kupunguza ukataji wa miti. Ni kutokana na kutambua ukweli huo ndiyo maana TPDC inatekeleza mradi wa kutengeneza gridi ya mabomba ya kusambaza gesi majumbani katika jiji la Dar es Salaam.

Jambo lingine muhimu kuhusu rasilimali hii ni kwamba tukiuza nje gesi nchi yetu itapata mapato mengi tena ya fedha za kigeni. Kwa vile gesi ni nyingi mapato ya Serikali yataongezeka sana, hivyo kuijengea uwezo wa kutimiza majukumu yake vizuri zaidi. Kama matumizi yatakuwa mazuri, gesi asili itakuwa kichocheo kikubwa cha kukuza uchumi wa nchi. Maendeleo ya haraka yatapatikana na hivyo kusaidia kuwaondoa wananchi wengi kutoka katika lindi la umaskini tulionao sasa.

Changamoto Muhimu
Ndugu Wananchi;
Pamoja na ukweli kwamba kuwa na gesi asili nyingi kunaipa nchi yetu fursa kubwa ya kujiletea maendeleo, zipo pia changamoto zake. Hatuna budi kuzitambua na kuzitafutia ufumbuzi ili gesi iweze kunufaisha ipasavyo nchi yetu na watu wake. Changamoto zipo nyingi lakini kubwa zipo za namna tatu.

Changamoto ya kwanza ni ile ya kujenga uwezo wetu wenyewe wa kudhibiti shughuli zinazofanywa na makampuni ya mafuta ili tuhakikishe kuwa tunapata malipo yanayostahili. Inatulazimu tuwe na wataalamu wetu wazalendo wa fani za taaluma zihusuzo gesi kama vile uhandisi, kemia, jiofizikia, uhasibu, ukaguzi na sheria. Tusipojenga uwezo wetu wenyewe kwenye maeneo hayo kuna hatari ya kudhulumiwa na kupata hasara. Pengine ipo haja ya kuwa na chombo maalum kwa ajili hiyo kama tulivyofanya kwa mafanikio kwa upande wa dhahabu.

Changamoto ya pili ni ile ya kupata Watanzania wengi wenye ujuzi na taaluma zinazohitajika na soko la ajira la sekta ya gesi. Tusipofanya hivyo makampuni yataajiri watu hao kutoka nje na hivyo kufanya Watanzania kutokunufaika na fursa za ajira zilizopo.

Ndugu Wananchi,
Kwa changamoto hizi mbili, jawabu lipo kwenye elimu na mafunzo tunayotoa kwa vijana wetu katika shule, vyuo vya ufundi na vyuo vya elimu ya juu. Kwanza kabisa lazima tuboreshe elimu ya sayansi na hisabati katika shule zetu za msingi na sekondari. Katika vyuo vya ufundi tutoe mafundi mchundo wa taaluma zinazohitajika na tasnia ya gesi na mafuta. Hivyo hivyo kwa upande wa vyuo vikuu nako wafundishe wataalamu wa fani zinazohitajika kama vile utafutaji wa gesi na mafuta, uendelezaji wa mafuta na gesi, uchumi na biashara ya mafuta na gesi, uhasibu na ukaguzi wa mafuta na gesi pamoja na sheria za mafuta na gesi na mikataba ya utafutaji na uendelezaji wa mafuta na gesi.

Ndugu Wananchi;
Napenda kuwahakikishia kuwa tayari tumejipanga kutafuta ufumbuzi wa changamoto hizo. Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kinajiandaa kuanza kutoa mafunzo yaChemical and Environmental Lab for Oil and Gas na fani yaExploration and Production Software Technology katika mwaka huu wa masomo. Chuo cha Madini Dodoma kitaanza kutoa mafunzo ya diploma ya Petroleum Geoscience kuanzia Septemba mwaka huu. Chuo Kikuu cha Dodoma, Chuo cha Sayansi na Teknolojia cha Nelson Mandela Arusha, na Chuo cha Teknolojia cha Mbeya na kile cha Dar es Salaam pia wameanza kufundisha mitaala hiyo. Aidha, VETA Makao Makuu na VETA Mtwara nao wanafundisha masomo yahusuyo gesi. Wizara ya Nishati na Madini itawadhaminiwanafunzi 50 kutoka Mkoa wa Mtwara kwenda kupata mafunzo hayo ya gesi asili katika chuo cha VETA Mtwara.

Ndugu Wananchi;
Wizara ya Nishati na Madini pia inatekeleza mpango mkakati wa kuwapata wataalamu wa sekta hiyo kati ya 40-50 kati ya sasa na mwaka 2016. Taaluma zinazotiliwa mkazo ni Petroleum Geoscience, Petroleum Geophysics, Petroleum Geochemistry, Petroleum Engineering, Petroleum Modeling, Oil and Gas economics, Oil and Gas Accounting and Auditing na Oil and gas Legal Regimes and Contract Negotiations. Kwa upande wake, Serikali itatoa upendeleo maalum kwa kulipia gharama zote za mafunzo ili tuweze kuwapata wataalamu hawa mapema iwezekanavyo. Nawaomba vijana wetu wachangamkie fursa hizi za masomo na watakapohitimu mafunzo wawe tayari kuitumikia nchi yetu kwa bidii.

Kujenga Uwezo Wetu wa Kutumia Mapato ya Gesi
Ndugu Wananchi,
Changamoto nyingine kubwa sana ni ile ya kuhakikisha kuwa mapato yatokanayo na gesi yanatumika vizuri na kwa manufaa ya taifa na watu wake. Lazima tuanze sasa kufikiria na kujipanga kwa ajili hiyo. Si vyema tukangojea mpaka hapo mapato yatakapoanza kupatikana ndiyo tufikirie na kutengeneza mfumo mzuri wa kusimamia na kutumia mapato yatokanayo na gesi. Tutakuwa tumechelewa, watu laghai na waovu watakuwa wameanza kunufaika hivyo watakuwa wagumu kutengeneza mfumo utakaowanyima fursa ya kuliibia taifa.

Jambo hili ni muhimu sana kufanya kwani ipo mifano hai ya nchi zenye rasilimali nyingi za mafuta na gesi lakini nchi na wananchi wake hawanufaiki sawia. Mauzo yanafanyika na fedha nyingi kupatikana lakini manufaa kwa nchi na watu wake ni madogo au hayapo kabisa. Wanaonufaika ni viongozi na baadhi ya maofisa wa umma wanaohusika na usimamizi wa shughuli zihusuzo rasilimali hizo. Na, hata sisi tunaweza kujikuta katika hali hiyo kama tusipojipanga vizuri sasa ambayo badala ya rasilimali kuwa baraka zinageuka kuwa balaa au hata laana.

Ndugu Wananchi;
Zipo nchi duniani ambazo zina usimamizi mzuri wa mapato ya rasilimali za mafuta na gesi na kuleta baraka na neema kwa taifa na watu wake. Nchi hizo zimeweza kuhifadhi na kutumia vizuri mapato yake kukuza uchumi wa nchi kwa jumla na kuboresha upatikanaji wa huduma za kiuchumi na kijamii kwa watu. Matokeo yake ni watu wa nchi hizo kuishi maisha yaliyo bora kuliko walivyokuwa kabla ya kupatikana kwa rasilimali hizo. Lakini, hii imewezekana kutokana na usimamizi mzuri na matumizi mazuri ya mapato yatokanayo na mafuta na gesi.

Tumeamua kujifunza kutoka nchi za wenzetu waliofanikiwa ili na sisi tunufaike. Na sisi tunajiandaa kutengemeza Sera ya Gesi Asili na kurekebisha Sheria ya Utafutaji na Uzalishaji wa Mafuta na Sheria ya Menejimenti ya Mapato ya Serikali yatokanayo na gesi zitakazotoa majibu hayo na kuliwezesha taifa kuwa na mfumo mzuri wa usimamizi wa utafutaji na uchimbaji wa gesi asili pamoja na usimamizi na matumizi mazuri ya mapato yatokanayo na gesi hiyo. Wapo wenzetu kwa mfano, wanacho kitu kinachoitwa Sovereign Funds ambapo mapato yote huhifadhiwa na baadae hutolewa kwa utaratibu maalum. Tunataka tujifunze kutoka kwao ili na sisi tutengeneze chombo chetu cha namna hiyo ili tunufaike.

Ndugu Wananchi;
Mambo hayo tumeshaanza kuyafanyia kazi. Katika mazungumzo yangu na baadhi ya wakuu wa nchi rafiki na mashirika ya maendeleo ya kimataifa, nimewasilisha maombi ya kusaidiwa na kushirikiana kwa mambo mawili. Kwanza kwa kuwawezesha Watanzania kupata mafunzo ya haraka kwa wataalamu watakaosaidia kusimamia shughuli za utafutaji, uendelezaji na biashara ya gesi asili nchini. Pili, watusaidie kupata watu wenye ujuzi na uzoefu ili watushauri kuhusu namna ya kutengeneza mifumo bora ya kusimamia na kutumia mapato ya gesi kwa mujibu wa mifano ya wenzetu waliofanikiwa. Nafurahi kwamba maombi yetu yamepokelewa vizuri na nchi zote na mashirika yote ya kimataifa tuliozungumza nao. Baada ya muda si mrefu kazi itaanza.

Mgomo wa Walimu
Ndugu Wananchi;
Jambo la tatu na la mwisho ni mgomo wa walimu. Pengine ni mapema kusema kwa vile kesho Mahakama itaamua kuhusu shauri hilo. Lakini napenda kuwahakikishia walimu kuwa tunawajali, tunawathamini na kutambua mchango wao muhimu kwa taifa letu. Wakati wote tumekuwa tunashughulikia madai ya haki zao na malimbikizo mbalimbali. Madai ya safari hii ni makubwa mno, yametuzidi kimo. Athari za kuyatimiza yalivyo yataifanya bajeti ya Serikali kutumia asilimia 75 kwa ajili ya mishahara ya watumishi wa Serikali na kubakiza asilimia 25kwa kuendeshea Serikali na kutimiza majukumu ya maendeleo kwa wananchi. Haitakuwa sawa. Ndiyo maana tumeshindwa kuelewana walipokataa rai hiyo na wao kusisitiza kugoma.

Wakati tunaendelea kusubiri uamuzi wa Mahakama, nina maombi mawili kwa walimu: Moja, wasiwalazimishe walimu wasiotaka kugoma wafanye hivyo, wawaache waendelee na kazi. Pili, wasitumie watoto isivyostahili kujenga hoja zao. Nawasihi warudi kwenye meza ya mazungumzo.

Ndugu Wananchi;
Kabla ya kumaliza hotuba yangu naomba nitumie fursa hii kuwatakia Waislamu wote nchini kheri na baraka tele kwa swaumu ya mwezi mtukufu wa Ramadhan. Wakati wote, mjiombee wenyewe kwa Mwenyezi Mungu awajaalie toba na malipo mema katika mfungo huu. Mkumbuke pia kuiombea nchi yetu amani, upendo na mafanikio mema.



Baada ya maneno hayo, naomba sasa niishie hapo. Nawashukuru sana kwa kunisikiliza. Sasa nipo tayari kujibu maswali ya Wahariri kama yapo. Ndugu Wahariri mliopo hapa, karibuni.