Nicholas Winton |
Nicholas alitengeneza mpango wa kuwavusha kutoka Czechsolovakia
na kuwapeleka watoto hao England; alipofika England alifanya kazi ya kutafuta
familia za Waingereza na kuzishawishi ziwachukue watoto hao kwa lengo la
kuwalea.
Katika mpango huo kabambe, Nicholaus alichukua magari 8 na kwa
umakini na usiri mkubwa alifanikisha zoezi hilo la kuwaokoa watoto hao.
Nicholaus alifanya siri ambayo hata mkewe hakuweza kujua. Miaka 50 baadae,
mkewe wakati anapekua pekua vitu, aliweza kuona kitabu kikiwa kimefichwa kwenye
dari. Kitabu hicho cha similizi kinachojulikana kama (scrapbook) kilikuwa na
majina na picha za watoto wote waliokolewa na Nicholas kwa takribani miongo 5
iliyopita. Mkewe, Greta aliamua kuichukua simulizi hiyo na kumpelekea Elisabeth
Maxwell ambae alikuwa mtafiti wa mauji ya kimbari ya Wayahudi (Holocaust) na
barua za hao watu waliokuwa watoto nyakati hizo. Kulikuwa na mwitikio kutoka kwa
watu zaidi ya 200 kati ya wale 669 katika ile orodha ya watoto kwa miongo 5
iliyopita kwa wakati huo.
Dunia iliyobakia nikiwemo mimi nawe msomaji wangu ilikuja
kuifahamu simulizi hii kupitia filamu-simulizi (documentary) iliyotengenezwa na
kituo cha habari cha BBC yenye jina That’s life (yaani haya ndiyo maisha).
Nicholaus alialikwa kama mmoja wa wahudhuriaji wa katika onesho hilo. Kile
kitabu chake cha kumbukumbu kikafunuliwa na maelezo kutolewa, na aliekuwa
mwenyeji wa hafla hiyo akauliza umma uliokuwa umehudhuria ambao walikuwa
wameokolewa kutoka na uamuzi wa Nicholas kuokoa maisha yao. Zaidi ya watu 20
walisimama wakiwa wamemzunguka Nicholas na kupigia makofi ya kumpongeza na
kumshangilia Nicholas.
Waweza kuiona video hiii kupitia tovuti ya www.youtube.com/watch?v=6_nFuJAF5F0 na kumwona mtu mkuu alieamua kugusa
maisha ya watu na vizazi vingine baadae maishani. Kwa uchache kati ya watu
aliowaokoa ambao ni maarufu katika jamii ni pamoja na Alf Dubs, Baron Dubs
(iliezaliwa mwaka 1932) na alikuwa Mbunge wa bunge la Ungereza kwa kupitia
chama cha Labour. Heini Halberstam (aliezaliwa mwaka 1926) na alikuwa bingwa wa
hisabati. Renata Laxova (aliezaliwa 1931), alikuwa daktari bingwa wa masuala ya
vinasaba vya watoto (peadiatric geneticist). Wengine ni Joe Schlesinger
(aliezaliwa 1928) alikuwa mtangazaji wa vipindi vya televisheni huko Canada na
muandishi wa vitabu. Na wa mwisho kumtaja katika makala hii katika orodha ndefu
ni Yitzchok Tuvia Weiss (aliezaliwa 1926), alikuwa Rabi Mkuu Jerusalem. Rabi ni
mwalimu wa dini ya kiyahudi.
Mpaka mwaka 2015 shirika la habari Uingereza BBC liliweza
kuwasiliana na zaidi ya watu 200 kati ya waliokuwa watoto 669 walioweza kuoka
na zahma la mauji ya kimbari.
Kutokana na maamuzi aliyoyafanya Nicholas, amefanikuwa kukusanya
tuzo za heshima chungu nzima ikiwemo kupewa cheo cha heshima na ushujaa kutoka
kwa malkia Elizabeth II wa na kuwa SIR NICHOLAS WENTON. Jamhuri ya Czech ilimpa
Sir Nicholas Wenton tuzo ya heshima ya Simba Shujaa; Kwa upende wake Rais wa
awamu ya 7 nchi Israel Ezer Weizman aliwahi kumpa tuzo ya heshima kwa niaba ya
Taifa lake.
Nimeguswa sana na watu wengie pia wameguswa na maamuzi ya Nicholas aliemua kuhatarisha maisha yake na kutumia gharama zake kwenda katika kambi kwa lengo la kuokoa watoto ili mkono wa mauaji ya kimbari wa Adolf Hitler usiwafikie. Miaka 50 baadae simulizi hiyo iliwekwa wazi na watu wengi kujua juhudi na “innitiatives” za Sir Wenton alizofanya akiwa kijana mdogo.
Napiga picha ya initiative ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam
Ndugu Paulo Makonda ya kunzisha vita dhidi ya uuzwaji wa dawa za kulevya jijini
Dar es Salaam. Kimsingi watu wengi wamepokea taarifa hii kwa mshangao kuna
kwamba “atafika wapi!”
Aidha kuna wengine wanamkejeli kama mtu anaejaribu kufunika aibu
ya wanafunzi wa kidato cha nne kufeli hususan mkoani Dar es Salaam. Wengina
wakidhani anatafuta umaarufu. Kila mmoja kwa hisia zake.
Binafsi nampongeza Paulo Makonda kwa nafasi yake na uzalendo
wake kwa nchi uamuzi wa kuchukua hatua ya kufanya uchunguzi kwa kushirikiana na
vyombo vilivyo chini ya ofisi yake na kutoa amri ya watuhumiwa wanaohusika
kukamatwa ili wahojiwe na wengine kusimamishwa kazi ili uchunguzi uendelee
pasipo wao kuathiri uchunguzi kama watakuwa kazini.
Nia ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam ni njema. Amenuia kupiga
vita vizuri dhidi ya biashara ambayo inaua hatima ya vijana wa Kitanzania.
Tukumbuke matokeo ya vijana kutumia “unga” ni kuwaharibia kesho yao na mchango
wao ambao wangeweza kuutoa katika ujenzi wa taifa hili.
Ilitakiwa Watanzania kwa nafasi zozote tulizonazo tusimame na
Paulo Makonda kwa kuwa anachokipinga ni kitu kibaya. Michelle Obama wakati
mmoja aliwahi kusema kuwa “kumpiga vita mmoja wetu ni kutupiga vita sote” Kwa
mantiki hiyo kumpiga Paulo Makonda nia yake njema ni kupinga sheria za nchi
zenye lengo la kuzuia matumizi, uuzwaji na usambazaji wa madawa ya kulevya.
Ni ukweli ulio wazi kuwa, mtu yeyote mwenye mguso maishani
alijengewa mazingira mazuri ya kumsaidia kufika ndoto zake maishani. Mihidarati
ni kitu ambacho kinaweza kuharibu tabia njema na mwenendo wa vijana na watoto
kuifikia kesho yao. Hivyo basi tunawajibika kuipingwa kwa ngivu zote.
Yawezekana si kila mtu ana nafasi ya kuwa kwenye vyombo vya dola
ili kutumia misuli kuzuia utumiaji wa mihadarati au usambazaji; kutokuwa na
nafasi kama ya Paulo Makonda au IGP Ernest Mangu, bado tuna jukumu la kupigana
kwa kupitia kuwatia moyo wapiganaji walio-mstari wa mbele kwa njia ya kuwaombea
kwa Mungu au hata kupaza sauti kupitia vyombo vya habari. Na tukiachukulia
mfano wa wapenzi wa soka anafahamu nguvu ya kumshangilia mchezaji au wachezaji
wanapofanya vizuri.
Nicholas alifanya maamuzi ya kuokoa watoto 669, miaka 50 baadae,
watu wale walikuwa watu wenye mguso akiwemo muandishi wa habari, daktrari
bingwa wa watoto, mwalimu mkuu wa dini na wengine wengi. Juhudi za Makonda zikifanikiwa
Dar es Salaam na kila mmoja akacheza nafasi yake kutimiza wajibu wake kukaba
ili wasambazaji wasiendelee kuuzaa katikati yetu, ni watu wangapi tutawaokoa?
Kama Mtanzania mzalendo, sioni kama mihadarati ina nafasi ya
kuongeza thamani katika maisha ya watoto na vijana kama wahanga wakubwa wa
mihadarati.
Rai yangu ni kuwa sisi kama wanajamii tunawajibika kwa pamoja
kuijenga nchi hii. Jirani akiharibikiwa au mtoto wa jirani akiharibikiwa
madhara yake yana uwezekano kwa upande mmoja au mwingine kugusa maisha yangu au
watoto wangu. Njia rahisi ni kuamua kupigana kuzuia madhara yasisambae kuliko
kuachilia yasambae.
Rais John Magufuli kampongeza IGP Mangu kwa kuchukua hatua ya
haraka za kinidhamu kwa watuhumiwa ndani ya Jeshi la Polisi ili kupisha uchunguzi
ufanyike.
Tukipanda mbegu njema kwa kugusa maisha ya wengine, ipo siku
tutavuna taji ya heshima kwa mrejesho wa watoto wetu na vijana wetu kuwa na
mguso chanya kwenye jamii. Ili jamii yetu iwe na uzalishiaji wenye tija
(effective production) mihadarati lazima ipigwe vita ndani ya mipaka yetu.
Paulo Makonda kaonesha mfano, kwa pamoja tumuunge mkono.
Fredrick Matuja
fmatuja@hotmail.com
fmatuja@hotmail.com
Note: Tunamshukuru sana Fred Matuja ambaye amekuwa akitutumia makala ili tushirikiane na wadau mnaopitia kwenye blog yetu.
No comments:
Post a Comment