Tafuta/Search This Blog

Friday, February 10, 2017

Nimekutana na mama Elizabeth Bhoke!

 Katika maisha kuna wakati huwa unaweza ukapata changamoto sana na ikakufanya ujiulize na ujichunguze Imani yako kwa Mungu. Kuna watu wanampenda Mungu sana na maisha yao wamejitoa kwa Mungu kwa asilimia zote. Sasa hii changamoto ndio niliyokutana nayo.

Nimekutana na huyu mama anaitwa Elizabeth Bhoke. Mama huyu ana umri wa miaka 79 na hana mume wala mtoto lakini yeye ni mwinjilisti ambaye huzunguka akikusanya Pesa ili ajenge makanisa katika wilaya ya Serengeti. Mama huyu wa kanisa la Sabato, tayari amejenga makanisa matano huko Serengeti na anaendelea kukusanya pesa ili kujenga mengine.

Huu ni moyo wa ajabu sana sana na kwa kweli umenipa changamoto sana ya kumpenda Mungu zaidi na kujali kile ambacho Mungu amekiweka ndani yangu na kukifanya kwa bidii sana kama huyu mama.

Kama mama huyu atakufikia tafadhali nyosha mkono wako na umbariki. Yeye pia hutoa maneno ya kubariki sana na pia ni mchangamfu mwenye maneno mengi ya kutia moyo....



Im so challenged!. God Bless you mama!

No comments: