Tafuta/Search This Blog

Thursday, October 20, 2011

Hatimaye Ghaddafi AKAMATWA!!!!

Habari zilizoandikwa hivi punde na BBC zinasema kwamba kiongozi wa Zamani wa Libya Kanali M. Gaddafi amekamatwa na kikosi kinachompinga.
Inasemekana amekamatwa akiwa na majeraha na amepelekwa kwenye hospitali kwa kutumia gari la kubeba wagonjwa.

Kwa habari zaidi fuatilia kwenye link ya BBC hapa chini.

UZINDUZI WA ALBUM YA MWANAHARAKATI WA HIP HOP GOSPEL, DOUGLAS PIUS. DPC TAR 16 OCTOBER 2011

DP akipaform wimbo unaoitwa hotuba. ulikuwa wa ukweli sana

Praise and worship team ya Boko basihaya ikiwa ina mtukuza mungu
huyu si mwanajeshi bali ni mwanamuziki, hapa anaimba wimbo unaoitwa MAJESHI MAJESHI


Saturday, October 15, 2011

Kumbukumbu ya Mwalimu JK Nyerere


Imetimia miaka 12, Tanzania bila mwalimu! Kama angekuwepo sijui angekuwa na maoni gani kuhsu taifa hili alilolipigania! Mimi na wewe hatujui, tunabakia kumkumbuka tu.

Kutoka mkuoani Mara SBP inakuletea taswira za hivi karibuni zinazohusu maisha ya baba wa Taifa letu.

Suti aliyovaa mwalimu mara ya mwisho alipokuwa anaondoka Tanzania kuelekea uingereza kwenye matibabu na ndio hakurudi tena.


Mwalimu wa mwalimu! Mzee huyu mwenye umri kama miaka 120 alimfundisha mwalimu JK Nyerere. Moyo wake umjaa malalamiko ikiwemo kunyimwa pension yake!

Mke wa mwalimu wa mwalimu.

Mnara wa kumbukumbu katika shule ya msingi ya Mwisenge aliposoma mwalimu.


Darasa alilosoma mwalimu.


Dawati alilotumia mwalimu katika shule ya msingi Mwisenge likiwa limejengewa ili kuhifadhiwa kwa ajili ya kumbukumbu.


Sehemu ya nyumba ya Mwalimu.

Gari alilotumia Mwalimu mara ya mwisho kabisa ya uhai wake likiwa katika eneo la makumbusho kijijini Mwitongo Butiama.


Ukipata nafasi unaweza kutembelea makumbusho ya mwalimu Nyerere huko Butiama na ukapata maelezo ya mambo mengi yanayomuhusu mwalimu kama raisi na pia kama baba na mwanakijiji. Kiingilio katika makumbusho hayo ni Tshs 1500 tu!

*********************************************************************************

Note, picha zetu leo tumeziweka alama kwa kuwa kumekuwa na watu wana tumia picha zetu kwenye blogs na magazetu bila hata ya kutuomba kibali au hata kuacknowledge! Kama utaipenda picha yetu please itumie na useme kwamba umeichukua kwetu kama ambavyo sisi mara zote hufanya!

Barikiweni!

Picha zote zimepigwa na Elias Msuya.

Wednesday, October 12, 2011

video - New life Band Live in Mwanza.

NEW LIFE BAND LIVE IN MWANZA


Jumapili ya tarehe 9October New Life Band walikuwa katika viwanja vya Furahisha jijini Mwanza kwa ajili ya tamasha la kusifu na kuabudu. Mambo yalikuwa mazuri sana na hizi ni baadhi ya picha!!
Eliud, Goodluck na Jimmy Kimutuo wakisebenesha!!
Kaka Abednego doing his things!

Jimmy, Abednego na mzee Gideon.
Pastor Isaya na Askofu Batenzi wakitoa neno la ufunguzi.


wananchi wakiserebuka - ayee Mungu wa milele wa mapendo Mungu wa milele!!