Tafuta/Search This Blog

Saturday, October 15, 2011

Kumbukumbu ya Mwalimu JK Nyerere


Imetimia miaka 12, Tanzania bila mwalimu! Kama angekuwepo sijui angekuwa na maoni gani kuhsu taifa hili alilolipigania! Mimi na wewe hatujui, tunabakia kumkumbuka tu.

Kutoka mkuoani Mara SBP inakuletea taswira za hivi karibuni zinazohusu maisha ya baba wa Taifa letu.

Suti aliyovaa mwalimu mara ya mwisho alipokuwa anaondoka Tanzania kuelekea uingereza kwenye matibabu na ndio hakurudi tena.


Mwalimu wa mwalimu! Mzee huyu mwenye umri kama miaka 120 alimfundisha mwalimu JK Nyerere. Moyo wake umjaa malalamiko ikiwemo kunyimwa pension yake!

Mke wa mwalimu wa mwalimu.

Mnara wa kumbukumbu katika shule ya msingi ya Mwisenge aliposoma mwalimu.


Darasa alilosoma mwalimu.


Dawati alilotumia mwalimu katika shule ya msingi Mwisenge likiwa limejengewa ili kuhifadhiwa kwa ajili ya kumbukumbu.


Sehemu ya nyumba ya Mwalimu.

Gari alilotumia Mwalimu mara ya mwisho kabisa ya uhai wake likiwa katika eneo la makumbusho kijijini Mwitongo Butiama.


Ukipata nafasi unaweza kutembelea makumbusho ya mwalimu Nyerere huko Butiama na ukapata maelezo ya mambo mengi yanayomuhusu mwalimu kama raisi na pia kama baba na mwanakijiji. Kiingilio katika makumbusho hayo ni Tshs 1500 tu!

*********************************************************************************

Note, picha zetu leo tumeziweka alama kwa kuwa kumekuwa na watu wana tumia picha zetu kwenye blogs na magazetu bila hata ya kutuomba kibali au hata kuacknowledge! Kama utaipenda picha yetu please itumie na useme kwamba umeichukua kwetu kama ambavyo sisi mara zote hufanya!

Barikiweni!

Picha zote zimepigwa na Elias Msuya.

1 comment:

shalom broz productions said...

Tunafurahi kuona historia ya mwalimu. Asante sana shalom broz. Kutumia picha unprofessionally sio vizuri kwa kweli.