Tafuta/Search This Blog

Monday, November 21, 2011

Kumbikumbi!

Msimu wa mvua huwa na neema hizi pia. Jirani yangu aliwakamata hawa chakula wengi akaniletea na mimi. Nilisahau kuwapiga picha hadi walipokuwa mekaribia kabisa kuisha nikaona tufaidi pamoja na wewe mdau. Haya karibu japo mmoja wa kuonja hata kwa macho tu...

Wednesday, November 16, 2011

Tunapenda sana KUDHAMINIWA!

Nilipokuwa naperuzi kwenye blogu ya blogger mkongwe wa hapa nchini kwetu leo nimekutana na habari ya ajabu sana kwamba kampuni ya bia Tanzania (TBL) kupitia kwenye kinywaji chake cha Grand Malt IMEDHAMINI graduu ya Mkwawa university Iringa!!! What a news!!

Hii ni ajabu sana kwa kweli! Kwani Mkwawa inamilikiwa na nani?? Na hivi inaingia akilini kwa mtu kwamba chuo kimeshindwa kufanya graduu hadi kipate udhamini?? na je kwani uongozi wa chuo ulikuwa unajua kwamba kuna siku wanafunzi watahitimu??? Nimejiuliza mengi sana na kwa kweli nimeudhika!!!

Tunapenda udhamini sana waTanzania,
Tunadhaminiwa net za kujikinga na Malaria
Tunadhaminiwa matangazo ya kufunga seat belt kwa ajili ya usalama wetu wenyewe...
Tunadhaminiwa matangazo kuhusu mahusiano kwenye ndoa zetu...
Tunadhaminiwa...
Tunadhaminiwa...

Sitashangaa siku hotuba ya rais ikidhaminiwa na USAID au siku kesi ya mahakama ya mwanzo itadhaminiwa na VODACOM!!!

Habari hii inapatikana hapa

Tuesday, November 15, 2011

Tanzania is still so beautiful!!

As i was travelling from Dar es salaam to Mwanza through Morogoro,Dodoma,Singida and Shinyanga i just felt like thanking God for this beautiful country. It is beautiful for sure, we are blessed...
God's arranged rocks near Mwanza.



Sukuma's traditional house. The land is so fertile.

Giant rock at Singida region.


Manyoni - Singida road.

Usimwambie mtu...

Hili kitu bado lipo barabarani. Nililikuta Singida last week.

Friday, November 11, 2011

Hatimaye Enson....


Enson akiombewa baraka na wachungaji.



Enson na mkewe Rest.





Enson yupo karibu sana na watoto na hapa walikuja kumpongeza.


Uncle Temba akifuatilia kwa makini ibada ya ndoa iliyoongozwa na mchungaji Martin Pyuza kutoka TAG Muheza.






Mambo ya kekizz. Rest akimlisha mumewe huku kaka mkubwa Simon Mmbaga akishuhudia.




Mkurugenzi akipeleka keki kwa wakwe zake.



Familia ya mzee Solomon Msuya kwa pamoja wakiongozwa na mtoto mkubwa kaka David.







Wanandoa.


Mr&Mrs Mmbaga


Mr&Mrs Mwakisambwe.
Mr&Mrs Lwendo






Mkurugenzi hatimaye ameoa. Amemuoa Rest Kileo. Wote walisoma sekondari ya kilimo ya Ifakara, huko ndiko walipokutana. Arusi yao ilifungwa katika kanisa la TAG Kigogo Mburahati na sherehe kufanyika kwenye ukumbi wa Mwika, Sinza.