Tafuta/Search This Blog

Wednesday, November 16, 2011

Tunapenda sana KUDHAMINIWA!

Nilipokuwa naperuzi kwenye blogu ya blogger mkongwe wa hapa nchini kwetu leo nimekutana na habari ya ajabu sana kwamba kampuni ya bia Tanzania (TBL) kupitia kwenye kinywaji chake cha Grand Malt IMEDHAMINI graduu ya Mkwawa university Iringa!!! What a news!!

Hii ni ajabu sana kwa kweli! Kwani Mkwawa inamilikiwa na nani?? Na hivi inaingia akilini kwa mtu kwamba chuo kimeshindwa kufanya graduu hadi kipate udhamini?? na je kwani uongozi wa chuo ulikuwa unajua kwamba kuna siku wanafunzi watahitimu??? Nimejiuliza mengi sana na kwa kweli nimeudhika!!!

Tunapenda udhamini sana waTanzania,
Tunadhaminiwa net za kujikinga na Malaria
Tunadhaminiwa matangazo ya kufunga seat belt kwa ajili ya usalama wetu wenyewe...
Tunadhaminiwa matangazo kuhusu mahusiano kwenye ndoa zetu...
Tunadhaminiwa...
Tunadhaminiwa...

Sitashangaa siku hotuba ya rais ikidhaminiwa na USAID au siku kesi ya mahakama ya mwanzo itadhaminiwa na VODACOM!!!

Habari hii inapatikana hapa

No comments: