Tafuta/Search This Blog

Tuesday, October 30, 2012

BARNABAS MINJA "BARII" NA DELPHINA SASA NI MWILI MMOJA

vijana wakijimwayamwaya...


Barii kwa aibu....!

Mr & Mrs Minja in 3D!
Hatimaye kijana wetu sasa amekuwa mkubwa na amempata mwenzake wa kuspend maisha! Arusi ilifungwa huko Moshi Tanzania na kushuhudiwa na wazazi pamoja na marafiki lakini pia kutakuwa na sherehe ya kumkaribisha "mwali" katika jiji la Mwanza siku chache zijazo.

SBP tunawatakia vijana wetu maisha mema na marefu ya ndoa.

**Picha kwa hisani ya kaka Stanley Joseph.

Saturday, October 20, 2012

Mazishi ya babu yetu mzee Daudi Lwendo, terehe 13 October 2012.

Babu yetu mzee Daudi Lwendo alifariki  usiku wa tarehe 10 oktoba 2012 nyumbani wake Igawa wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya baada ya kuugua. alifariki akiwa ameishi miaka 98! Tulimshukuru Mungu kwa maisha yake na kupata nafasi ya kusherehekea maisha yake na kumlaza kaburini siku ya jumamosi tarehe 13 Oktoba hukohuko Igawa.
Hizi ni baadhi ya picha za tukio hilo.

Kwa mara ya mwisho tunamuaga.


Mavumbini ulitoka na mavumbini utarudi.


Bibi Judith akiweka shada la maua kwenye kaburi la marehemu mume wake.

Mama yetu akiweka shada la maua kwenye kaburi la mkwe wake.

Hapa ndipo tulipoulaza mwili wa babu yetu.



Ndugu katika kaburi 

Old friends! kaka Gee na rafiki yake ambaye pia ni babu yake mzee Mazengo.
Heri wafu wafao katika Bwana.
Tunaendelea kumshukuru Mungu kwa maisha ya Babu yetu!

Thursday, October 18, 2012

Tanzania ninayoijua mimi ni nzuri!!

Mbarali karibu na makao makuu ya wilaya ya mbarali. Kwa mbali inaonekana mwanzo ya milima ya Udzungwa.

Mto Mbarali, maeneo ya Igawa.

Shamba la miti la Sao Hill maeneo ya Mafinga.
Maeneo ya mwanzo wa mlima Kitonga, Iringa.
Mimi bado ninaamini hii ni nchi nzuri sana. Je unaamini pamoja nami?? Please do.