Tafuta/Search This Blog

Tuesday, March 26, 2013

Ni kweli huwa simba anazaa wakati huu??

Mvua kubwa ya jioni wakati jua bado linawaka sana.

Hapa ni KVCC Mwanza.

Tangu nikiwa mdogo, nimekuwa nikisikia kwamba ukiona mvua inanyesha na jua linawaka ujue Simba anazaa.Juzi nikakutana na hili tukio tena lakini hii ya juzi mvua ilikuwa kubwa sana wakati jua linawaka. Kuna mtu anajua ukweli wowote??
Ila cha msingi ni kwamba msimu wa mvua umeanza!

Wednesday, March 20, 2013

Salma Cone Mwanza hapa...

Kijiwe maarufu sana jijini Mwanza kwa mambo ya Ice Cream, Kuku wekundu, Mishkaki, chipsi na mazagazaga yote ya tumboni. Jioni huwa panakuwa busy sana. Makao makuu ya klabu ya mpira wa miguu ya Toto Africans yapo karibu sana na hapa.

Sunday, March 17, 2013

Please Vote for our very own doctor Naiz!


Dear Friends and colleagues,
Please vote for me, I applied for grants in grand challenge Canada with an Idea of setting up a local RHD control program in lake zone/Mwanza, kindly follow the link below which will direct you to vote.Thank you very much for your assistance on this.Please help me by telling others too.

Naiz
Pediatric Cardiology Fellow
Wolfson-Israel




Saturday, March 16, 2013

Mdogo wetu Maria Mtili ametunukiwa Diploma ya Teknolojia ya Mawasiliano (IT)

Mwaka umeanza na shangwe pia zimeshaanza. Mdogo wetu hatimaye amefanikiwa kumaliza masomo yake na kutunikiwa diploma katika taasisi ya IIT hapo Dar Es Salaam. Hizi ndio picha za tukio.


Pozi la kisomi.


Mdada.

Mama na binti yake.


Mfanano, kama mtu na dada yake.


Fullu tabasamu...



Hongera dada.



...Na hasa kama una akili...


Zaidi ya diploma binti huyu pia alipata tuzo kadhaa kwa kuwa mkali sana darasani.





Tunakupongeza sana mdogo wetu na tunakuombea heri ili uende mbele na mbali zaidi.
Hongera nyingi kutoka kwa kaka mkubwa Godlove.

Wednesday, March 13, 2013

Sikujua kuhusu hii plate number...


Gari analotumia mheshimiwa Freeman Mbowe ambaye ni Kiongozi wa Upinzani Bungeni. Hapa alikuwa katika mkutano huko Musoma.

KUB - Kiongozi wa Upinzani Bungeni.

Picha hii ni mali ya website ya Wavuti.