Tafuta/Search This Blog

Thursday, March 16, 2017

FC BARCELONA NA GLENN CUNNINGHAM WANATHIBITISHA KUWA TANZANIA YA VIWANDA INAWEZAKANA



Nilipenda kukimbia tokea nikiwa mvulana. Ilikuwa ni kukimbia maili moja (sawa na kilomita 1.8). Glen alikuwa mvulana na hadithi yake ni ya kweli na kusisimua yenye mkasa unaotupa funzo la kuwa ukiwa na nguvu ya dhamira na kufanyia kazi kile unachoamini hakuna lisilowezekana chini ya jua.
Kwa kifupi hii ni hadithi ya Glenn Cunningham alezaliwa August 4, 1909 huko Kansas nchini Marekani.
Akiwa shule msingi na umri wa miaka 8, siku moja Glenn aliungua moto kufuatia mlipuko mkubwa darasani ulisababishwa na galoni la mafuta ya Petroli. Nyakati hizo kulikuwa baridi kali na kila siku wanafunzi walikuwa na jukumu la kuwasha jiko kwa kutumia mafuta ya taa ili kupasha chumba cha darasa joto. Siku moja, mtu asiefahamika aliweka petroli kwenye galoni badala ya mafuta ya taa. Glenn bila kujua aliwasha moto kama kawaida na kupatwa na mlipuko uliounguza mwili mzima na miguu yake kupoteza hisia kabisa kufuatia kufa kwa mifumo ya ufahamu.
Ushauri wa madaktari ni kuwa akatwe miguu kwani asingeweza kutembea kabisa maishani mwake. Mama wa Glenn aliekuwa anaitwa Rosa alikataa ushauri huo wa kumkata mwanae miguu ulitolewa na daktari. Glenn alikaa hospitali kwenye hali ya kutojitambua (in coma situation) na baada ya siku nyingi fahamu zilirudi na taratibu hisia za ufahamu zikaweza kuwa hai tena.
Baadae Glenn alipata ruhusa ya kwenda nyumban. Akiwa nyumbani alikuwa anawekwa juani na wazazi kwenye kiti cha magurudumu (wheel chair) kama mtu mwenye ulemavu. Kuifanya hadithi hii kuwa fupi kuna siku Glenn aliweza kutembea. Alipofanikiwa kutembea japo kwa kuanguka anguka, aliamini kuna siku anaweza kukimbia. Glenn alikuwa anatafakari na kukiri kitabu cha Isaya 40:31 “Lakini wote wanaomtumainia Mwenyezi-Mungu,watapata nguvu mpya.Wataruka juu kwa mabawa kama tai; watakimbia bila kuchoka;watatembea bila kuchoka."
Miaka kadhaa baadae Glenn aliweka rekodi kadhaa za dunia katika mchezo wa riadha. Ntaziweka rekodi chache hapa chini kwa ajili ya kumbukumbu.
Alimaliza mbio za riadha za Olimpiki ya majira ya joto mwaka 1932 na 1936. Akiwa njiani kurejea kutoka kwenye Olimpiki ya nchini Ujerumani, alipigiwa kura kama mtu maarufu kabisa huko Marekani na wana riadha wenzake wa Olympiki.
Mwaka 1933 Glenn alishinda medali ya Sullivan kwa mafanikio yake katika mbio za kati.
Mwaka 1932 kwenye Olimpiki alikuwa mtu wa 4 katika mbio za mita1500
Mwaka 1936 katika Olimpiki zilizofanyika huko Berlin Ujerumani, Glenn alishinda Medali ya fedha katika riadha, umbali wa mita 1500
Mwaka 1934, Glenn aliweka rekodi ya dunia kwa kukimbia maili moja kwa muda wa 4:06.8. Rekodi hii ilichukua miaka 3 kuvunjwa.
Mwaka 1936, Glenn aliweka rekodi ya dunia yam bio za mita 800.
Kwa kifupi Glenn aliweka rekidi nyingi sana. Tukumbuke, hakutarajiwa kutembea kwa vipimo vya kidaktari kutokana na hali aliyokuwa nayo kufuatia kuunguzwa vibaya na moto. Glenn alistaafu riadha mwaka 1940 akiwa na miaka 31.

Hadithi ya Glenn imenikumbusha mechi ya fainali ya mpira wa miguu kati ya Liverpool na AC Milan ya wakali wa wakati huo kama Andrey Shevchenko, Paolo Maldini, Kaka na Hernan Crespo na wengine wengi. Mpaka dakika 45 zinaisha vijana wa Anifield walikuwa nyuma kwa bao 3-0. Kipindi cha pili, Liverpool chini ya nahodha Steve Gerald walirudisha magoli 3 na kuingia katika changamoto za mikuwaju ya penati. Kwa wapenzi wa soka mnakumbuka, Liverpool chini ya kocha Raphael Benitez, walichukua kombe la klabu bingwa Ulaya 2005 kufuatia kuwashinda AC Milan kwa mikwaju ya penati.
Usiku wa jana kuamkia leo kati ya saa 4.45 usiku na kuendelea FC Barcelona ikiwa chini ya Luis Enrique imeleta historia ya kupindua goli 4-0 za mechi ya kwanza kwa kuibamiza PSG kutoka Ufarasa kwa bao 6-1. Kufuatia ushindi huo, naomba kunukuu maneno machache kutoka kwa wanakabumbu kutoka Calanonia.
Gerard Piqué alisama haya baada ya mchezo… “Tumeona matokeo mengi yakibadlishwa katika soka, ila si kama ushindi huu” akimaanisha kupidua magoli 4-0. Na kufunga mabao 6-1 ndani ya dakika 90. Pique aliendelea kusema….”Yeyote asie-amini, anatakiwa aende na aje tena”
Mtu mwingine ni nahodha wa FC Barcelona kiungo mchezeshaji, Andrés Iniesta, ambae alisema hivi…“Tumeshuhudia kitendo cha kihistoria” Iniesta alihitimisha kwa kusema “Hatukukoma kuamini – kiuhalisia ilikuwa haiwezekani isipokuwa imetendeka” (We never stopped believing — it was virtually impossible but it happened.)
Mpira wa jana kati ya FC Barcelona na PSG una mafundisho makubwa kwetu wanadamu, hususan sisi Watanzania. Tunawajibika kuamini na kutoacha kuamini kwa jambo jema tunalolipigania haijalishi uhalisia wa matokeo ya kushindwa huko nyuma ukoje.

Kwa akili tulizo nazo na tukiamua kuweka juhudi kubwa kuleta msukumo kwenye ujenzi wa Tanzania ya Viwanda hususani lenye nia njema kwa kutengeneza bidhaa zenye uhitaji katika soko. Tunaweza  kubadili maisha yetu  kiuchumi na kuwa sehemu ya kujenga daraja la kada la uchumi wa kati Tanzania
Rasilimali zipo, fursa zipo. Cha msingi tunatakiwa kuweka msukumo na jitihada kubwa ili kupata matokeo tunayotarajia.
Mkusanyiko wa jitihada (concentrated efforts) na imani ya kufanya kile unachokusudia bila kukata tamaa, kunaweza kubadili matokeo na historia ya maisha. Ni kweli Rais Magufuli ana muda wa miezi karibu 17 kati ya miezi 60 ya utawala wa awamu yake ya kwanza. Na matokeo yataonekana kwa wale watakao amua kuwa sehemu ya mchezo kubali matokeo na si kulalamika au kuwa watazamaji.
FC Barcelona wamevuka kwenda robo fainali ndani ya dakika 90. Tumbuke, goli 3 zimefungwa kuanzia dakika ya 87 ukijumlisha na muda wa ziada (extra time).
Watanzania, tuna nafasi ya kuwa sehemu ya kujenga uchumi wa viwanda ikiwemo kulima kilimo endelevu kwa kuangalia mahitaji ya soko ndani nan je ya nchi. . Kenya wametangaza, njaa kutokana na changamoto za mabadiliko ya tabia nchi. Somalia wametangaza njaa. Djibout na Sudan hali kadhalika. Wingi wa watu hawa wanahitaji chakula. Tanzania tuna fursa ya kufanya kilimo endelevu cha umwagiliaji. Tuna fursa ya kuvuna na kusindika mazao ya chakula na mazao malighafi kwa viwanda ili kukidhi mahitaji ya soko la ndani na nje.
Barcelona waliamini na kutumia jitihada zote ili kuweka historia. Nasi tuna nafasi ya kuamini na kufanya mambo ya maana. Glenn hakutarajiwa hata kutembea. Ushauri wa daktari ilikuwa ni kukatwa miguu. Miguu ya Glenn, maishani mwake iliweka rekodi kadhaa si za kukimbia kama mimi na wewe ambao tunaweza kukimbia si kwa mashindano, bali Glenn alivishwa medali katika mashindani makubwa kama Olimpiki ndani na nje ya nchi yake.

Watanzania tunawajibika kuamua. Tunaweza kuwa-prove wrong wale wasio amini na watazamaji. Nchi za Asia ya mbali miaka ya 60 zilikuwa kama sisi katika hali ya kiuchumi. Asia waliamua kwa juhudi zote na leo baadhi ya nchi hizo wanatusaidia kiutaalamu, kutuunzia vitu na mambo chungu mzima.

Ni wakati wa kuamini na kutenda kwa kupigana mpaka mambo yatokee. Barcelona hawakuwa na muda wa kumlaumu kocha Luiz Enrique. Wachezaji walicheza mpira ili kuleta matokeo. Watanzania tunawajibika kucheza mpira wa kuwa sehemu ya maendeleo ya Viwanda. Tukiweza kukuza kundi la wazalishaji bila shaka kundi la walipa kodi litakuwa na kuongeza makusanyo ya hazina.

Kwa pamoja tunaweza kujienga Tanzania.  

Fred Matuja
fmatuja@hotmail.com  
 



Tuesday, March 7, 2017

RAIS MAGUFULI ANATUTAKA TUSOME KITABU CHA DONALD TRUMP




The beginning of every government starts with the education of our youth.
(Mwanzo wa kila serikali unaanza na kuwapatia elimu vijana wetu)
—Pythagoras


Katika kitabu chake cha “Think Like a Champion” yaani fikiria kama mshindi, mwandishi Donald J. Trump ambae kwa sasa ni Rais na Amri Jeshi mkuu wa taifa tajiri na nguvu za kijeshi la Marekani, amenukuu falsafa ya Pythagoras.


Muandishi Donald Trump, amehimiza umuhimu kwa kujifunza na kuoanisha aina ya kujifunza kama mwanzo mpya kwenye kila zama ambayo mtu unaingia. Katika kitabu hicho Donald Trump ameonesha jinsi Pythagoras aliekuwa nguli wa falsafa hususani katika somo la hisabati, mara nyingi alitafsiri mambo mengi kwa kuoanisha au kuwakilisha na tarakimu au nambari.


Donald Trump yeye kama mfanya biashara nyakati ameandika na kupiga chapa kitabu kicho yaani mwaka 2009 ameonesha kuwa kuna muunganiko wa moja kwa moja kati ya elimu inayompa mtu mmoja mmoja maarifa hali kadhalika jamii nzima kupata maarifa kupitia mifumo mbalimbali ya elimu.


Mie ninaendika makala hii kwa uzoefu na ujuzi niliopata wakati nasoma chuo cha ualimu na baadae kupata mafunzo ya taaluma nyingine, naweza kurejea jambo ambao nimewahi kuandika huko nyuma kuwa sisi wanadamu, tuna namna ya kujifunza shule au vyuoni (formal education), kuna namna ya tunajifunza kwa malengo maalum ili kupata ujuzi tunaoutaka (non-formal education). Vilevile tunaweza kujifunza kwa kupitia vitabu, majarida, mitandao ya kijamii, program za radio, televiseni n.k na hii inaitwa (informal education). Vyovyote vile, maarifa tunayoyapata yanatakiwa kutubadilisha namna ya kufikiri na kuzalisha mabadiliko ya kitabia.


Trump, alijikita katika kusisitiza kila mtu anapoanza jambo jipya, kuna umuhimu wa kujifunza au kujiongezea maarifa mapya kuhusiana na mambo mapya anayotaka kuyafanya. Mwandishi ambae ni Rais wa awamu ya 45 kwa sasa ya Marekani amejielezea kwa uzuri namna ambavyo amekuwa katika kujifunza ujenzi wa nyumba na hoteli ili anapokuwa na wahandisi-wajenzi walau asiachwe nyuma na lugha za kimsingi za kiufundi hasa katika ujenzi.


Kuna nyakati alijikita katika uendelezaji wa viwanja vya gofu, ilimlamlazimu pia atafute kundi la wataalamu wa kucheza mchezo wa gofu na wajenzi wa viwanja wa gofu. Lengo lake, ilikuwa ni kukaa na wataalamu kwa lengo la kupata taarifa za msingi kutoka kwenye uzoefu wa sekta au biashara ambayo alikusudia kuifanya.


Donald Trump aliamini na anaamini sana katika hisia mpya huwa zinajengwa katika misingi ya mwanzo mpya na mwanzo mpya umeunganishwa na maarifa mapya yanayopelekea namna mpya ya kufikiri na namna mpya ya kutenda ili kupata matokeo mapya.


Haina tofauti na msemo wa kibiblia wa umuhimu wa divai mpya katika chupa mpya ili kupata matokeo tarajiwa. Tofauti na divai mpya unaweka katika chupa ya zamani. Inapelekea kupoteza divai na chupa hali kadhalika.


Natamani kununua au kuazima uzoefu wa falsafa ya Donald Trump katika muktadha wa Tanzania ya Rais John Pombe Magufuli na Watanzania walio wengi.


Kuna namna Mheshimiwa Rais ameingia darasani kama mwalimu na anatoa mafunzo kwa chaki ubaoni. Wakati Mwl. Magufuli anafundisha kwa mujibu wa mungozo mpya wa somo (new syllabus) kwa upande mwingine wanafunzi ambao ni Watanzania wanakumbuka mafunzo na malezi ya Mwl. Jakaya Mrisho Kikwete ya awamu ya 4. Na wengi wakitaka kuishi kama awamu ya 4.


Falsafa ya Mwl. Kikwete ilikuwa 1+ ( ) = 5. Wanafunzi ambao ni Watanzania tulikuwa na jukumu la kufikiri ni namba ngapi ikijumlishwa na moja tunapata 5. Kwa muongozo wa kujifunza haukuhitaji njia ya kuonesha jibu ambalo ni 4 umelipataje. Na kwa muongozo wa mafunzo yale, ukiweka 4 mwalimu atakupa vema kwa kuwa jibu ililoweka ni sahihi.


Mara hii ameingia Mwl. Magufuli ambae ana swali kama lile la mwalimu wa awamu ya nne, isipokuwa badala ya parandesi, wakati swali lina herufi X
1+X = 5.


Mwalimu Magufuli anataka utafute thamani ya X kwa njia za kihisabati za jiometri.


Sote tunakubaliana kuwa thamani ya X ni 4, isipokuwa njia ya kuifikia 4 ni tofauti na muongozo wa mafunzo ya Mwl. Kikwete.


Awamu ya 5 anatutaka ili kupata jibu, sisi Watanzania ambao ni wanafunzi darasani, tuna wajibu wa kujua kwamba tunatakiwa kuonesha njia ya kulifikia jibu ambalo ni 4.


Kwa lugha rahisi inatakiwa kuchukua swali 1+X = 5 na kutoa 1 kila upande


1+ (-1)+ X = 5 – 1


Jibu litakalopatikana litakuwa wazi kabisa kuwa


0 + X = 4


Hivyo basi kumbe thamani ya X = 4.


Huu ndiyo mfumo wa muongozo wa mafunzo anayotumia mwalimu wa awamu ya 5. Kuna uwezekano kutokana na wepesi wa masomo awamu ya 4, kuna nyakati mwalimu alihitaji tuimbe nyimbo kama sehemu ya kujifunza.


Isipokuwa muongozo wa kujifunza na kufundishia uliopo sasa watutaka tujue namna tofauti ya kutafuta thamani ya X. Muongozo wa mwalimu hautupi fursa ya kuimba kama namna ya kujifunza kama kule nyuma. Na hapa ndipo tofauti inapoanza kuonekana kwani baadhi ya wanafunzi bado wanatamani uji kumbe tupo katika zama za kula ugali na nyama ya mifupa. Tunawajibika kutumia meno yetu kutafuna kuitoa nyama katika mifupa.


Wanafunzi darasani (yaani Watanzania wengi) bado wanataka mwl. Magufuli afundishe kama mwl. Kikwete na kutumia njia za zamani kuja na jibu la thamani ya X.


Nitoe rai kwa Watanzania wenzangu ambao ni wanafunzi katika darasa la mwalimu wa awamu ya 5; chonde chonde, tuna jukumu moja kubwa la kufanywa upya namna ya kufikiri. Namna pekee ya kufikiri na kukubaliana na ukweli, mfumo mpya wa muongozo wa mafunzo ndivyo unavyotaka, na mwalimu tulie nae, muongozo wa masomo na mbinu zake za kujifunzia si kuimba (nibebe nibembeleze kama wimbo mmoja uliowahi kutamba katika nyimbo za injili).


Tukiji-position kwa kujua tupo awamu ya 5 na kuamua kujikita katika mbinu mpya za kukokotoa ili kupata majibu; tukifanya hivyo bila shaka lawama na manung’uniko yataisha. Na tutajikuta tunawajibika na kujituma kwa kutumia mbinu halali na njia halali ya kufikia jibu.


Tukigoma kujifunza, tunajiweka katika hali ya kutokua kiufahamu hususani kwenye kukabiliana na changamoto zinazotuzunguka.


Tunaweza kupata jibu la changamoto nyingi ikiwemo kutengeneza hela kihalali bila kutumia njia za mkato pale tu tunapojua, awamu hii na muhula huu, unahitaji mtanzamo mpya katika utatuzi wa matatizo yanayotuzunguka.
Na utatuzi unapofanyika, maana yake njia ya kufikia jibu inatakiwa kuwa wazi ili mtu yeyote anaekagua namna mwanafunzi alivyopata jibu, bila maswali ya ziada aone jibu lilivyopatikana.


Ili tufaulu hisabati za mwl. Magufuli hatuna budi kumpenda na kumkubali kuwa ndiye mwalimu wetu na tunawajibika kukubaliana na mbinu zake za kufundishia na kujifunza ili kupata matokeo tunayotarajia.


Wataalamu wa saikolojia wanaonesha kuwa, wanafunzi hufaulu vyema pale wanapokuwa na uhusinaano mzuri na mwalimu huhusani kwa kumpenda na kushirikiana nae hata nje ya saa za darasa kwa kwa nia njema ya kujifunza ili kutatua mafumbo kwa lengo la kupata majibu.


Chuki kwa mwalimu hupelekea kuchukia somo vilevile, na hatimaye kushindwa kukabili changamoto za masomo. Ufaulu wa masomo ni faida ya mwanafunzi kupata daraja zuri au alama nzuri. Ufaulu wa kutatua changamoto zinazotuzunguka, sisi wanafunzi (Watanzania) ni wafaidika wa kwanza.


Hii yanikumbusha siku chache zilizopita nilipata kuhudhuria mafunzo yaliyokuwa yakifanywa na maafisa wa kijeshi. Moja ya kitu nilichopata katika mafunzo yale, ni namna wapiganaji hao wanavyofikiri ili kupata majibu ya utatuzi wa maswali magumu au changamoto mbele yao.


Afisa mmoja akatoa mfano, ukikutana na mto wenye mamba wakali na unatakiwa kuvuka upande wa pili wa mto; Je utapita katikati ya maji ili mamba wakutafune au utafanya nini. Afisa yule wa kijeshi akaweka wazi kuwa, kuna namna ya kuishughulisha akili ili kupata suluhisho la kusonga mbele na kuendelea na safari ili kufika kule unakotaraji.
Moja ya suluhisho lililotolewa na mpiganaji yule ni kurusha kamba upande wa pili wa mto na kuifunga kamba nyingine kwenye kipago au mti mubwa na kisha kuvuka kwa kutambaa kwa miguu na mikono kwenye kamba huku mamba wakikukodolea macho unapopita juu yao.


Kwa mtu mwingine angeweza kurudi alikotoka, mwingine angeweza kutupa lawama ooh… kuna mamba kwenye mto, na mie siwezi kuvuka. Tofauti ya kufikiri kwenye tatizo lile lile ndilo linawafanya Wanajeshi kujiona washindi na akili zao zimejiengwa kusonga mbele hata pale mambo yanapokuwa magumu. Hivyo kurusha kamba upande wa pili na kisha, anavuka kwa kamba ni moja ya mbadala katika mbinu mpya ya kutatua tatizo la mto wenye mamba.


Katika nyakati hizi, tuna wajibu wa kufikiri kwa kiwango sawia na muongozo wa somo la awamu ya 5. Moja ya assignment (homework) aliyoitoa mwalimu Magufuli wakati mmoja akiongea na wahariri, ni waandishi kufungua kampuni ili kujenga viwanda au kuwa na shughuli ya uzalishaji mkubwa unaotoa ajira kwa vijana na kuongeza thamani ya malighafi hasa za mazao ya kilimo na mifugo. Nae Mheshimiwa Rais alitoa ahadi ya kusaidia mchakato ili kampuni hilo lipate mkopo kutoka benki ya ukekezaji. Je kuna, mtu au waandishi wameshapeleka andiko la mradi wa kampuni na mwalimu wetu wa darasa la awamu ya 5 akashidwa kutoa msaada? Au ndiyo wengi wanatumia kalamu na keyboard za social media kulalamika tu?


Kumbe tunaweza pia kungusha mti na kuulaza upande mmoja wa mto kwenda upande mwingine na kuvuka kwa kutambaa juu ya gogo la mti na kuendelea na safari ya maisha pasi kulalamika kwanini mwalimu anatuelekezea njia ngumu za kupata matokeo.


Mungu ibariki Tanzania. Tuna jukumu la kumkubali mwalimu wetu ili tufaulu mitihani katika zama za mafunzo mapya ili kupata alama nzuri na kusonga mbele katika hatua ijayo.


Fred Matuja

fmatuja@hotmail.com