Tafuta/Search This Blog

Saturday, September 13, 2008

UJUMBE

Wapendwa,

Ninaye rafiki yangu anaitwa A.J Kaluse. Huyu bwana huwa na mawazo ya tofauti sana na wengi wetu kuhusiana maisha. Mimi namfurahia sana kwa sababu mawazo yake huwa yananifurahisha. Amenitumia mail hii ambayo nimeona niiweke kwenye blog yetu ili niskie ninyi wapendwa wetu mtasemaje. Naamini ninyi woote ni watumiaji wa barua pepe. naomba kusikia maoni yenu.

NB: Kaka Kaluse samahani sana kwa kutumia ujumbe wako bila kukutaarifu, naamini utanielewa.

Dear All,

Let us share some of kaluse's ideas.
1. kwa nini mail nyingi tunazotumiana ni za vichekesho kuliko uelimishaji.?
2. Isitoshe idea ya kwanza ya maili tunazotumiana ni za kucopy and kupaste au forwaded?
3. Ni kweli hatuna uwezo wa kufikiri mambo na kutaarifiana yanayohusu nchi yetu au Afrika yetu mpaka twende kwenye websites za nje ya Afrika kunukuu?

NDUGU WAPENDWA, RAFIKI NA JAMAA ZANGU. SAMAHANI KWA WALE NITAKAOWAUDHI,MIMI BINAFSI SIPENDEZWI NA MAIL MOJA KUTUMIWA NA WATU MIA MBILI KWANI HII HUNIFANYA KUJIONA KAMA SISI HATUNA UWEZO WA KUFIKIRI NA KUIBUA MAWAZO MAPYA.
BASI JARIBU KUFANYA HATA EDITING TO SOME PLACES, JAMANI HATA NUKTA TUNAKUNYWA AAH MAZEE IISIYO.
KIBAYA ZAIDI MAIL ZINGINE SIO CURRENT YANI ZA CHIMBO(ZA MIAKA KIBAO ILOPITA) HALAFU BILA SONI MTU ANAKUTUMI KAMA ILIVYO BILA KUJUA YEYE NDIO KACHELEWA KUFAHAMU HUO UJUMBE.
NB;
NAOMBA NIELEWEKE SIKATAI KUPASHANA HABARI ZA NJE YA AFRIKA LA HASHAA, ILA ZIWE ZA KUENDANA NA WAKATI NA ZA AINA TOFAUTI YANI ZA KUCHEKESHA,KUELIMISHA,KUHUZUNISHA, NA KUONYA AU VINGINEVYO ZAIDI.

1 comment:

Anonymous said...

Poa tumekusikia Mtaalam wa kurekebisha tabia zilizo shindikana. Utaweza wewe?