Tafuta/Search This Blog

Friday, November 28, 2008

TABIBU??????


Nimekutana na hili tangazo ambalo lilipatikana huko Iringa kumhusu huyu tabibu anayedai kuwa anaweza kutibu mambo lukuki ya kimaisha hadi UTORO wa shule!!


Inasikitisha kwamba watu wengi wameingia kwenye hii mitego na kujikuta wakipeleka mali zao zote kwa "matabibu" wa namna hii!!


Jamani wapendwa, kuna tabibu mmoja tu anayeweza kuweka sawa mwili wako na Roho yako pia, ni YESU KRISTO!!


Habari ndio hiyo!!

Thursday, November 27, 2008

Dom kwa Vipita shoto.

kipita shoto pale.
Kingine.


Hata maeneo ya makazi ya watu utazikuta,..

Humu ndani pia vipo vipita shoto



Kaka Enson ambaye aliwakilisha Shalom Broz Prod huko Dodoma.





Shalom Broz Tulizuru Dodoma, Mh Vumbi Tupu


KWA KUKUHAKIKISHIA CHEKI MJENGO HUO. NILIPITA PALE NJE, DU NIPAZURI USIPIME.CCM BWANA WAMEJIJENGA SANA HAPA NCHINI, KAMA UNAVYOWEZA KUONA HAPA. WALA HAPA SIO MAKAO MAKUU. NILIKUA NAHUDHURIA SEMINA HII. NILIKUA BUSY SANA KAMA UNAVYOWEZA KUONA.


MAPUMZIKO HAYA. TULIKUA TANZANIA ASSEMBLIES OF GOD BIBLE COLLAGE

HAPA GETINI. HAWA NI WADAU WA SEMINA. DANIEL NA MWENZAKE.









Saturday, November 22, 2008

Kutoka ARUSHA na KIA

ARUSHA
Kikwangua anga kipya cha Arusha kama kinavyoonekana kutoka katika uwanja wa michezo wa Sheikh Amri Abeid Karume.


Mnara wa kumbukumbu ya azimio la Arusha

KIA

Kaka Gee mbele ya Boeing 737-700(BBJ) iliyotutembelea hivi karibuni.


Engeneer Conrad Andrew.








Friday, November 14, 2008

Hayawi hayawi sasa yamekuwa!!!!!!!!!!

sweet moment
At last!!
vilaji

vinywaji hai tebo!!




tabasamu la Sanga.


Baada ya kusubiri huu ubwabwa kwa muda mrefu hatimaye Bwana alifungua njia na Ubwabwa wa kaka Noel Sanga ukaliwa tarehe 8Nov. Sanga amemuoa binti na mtumishi wa Mungu anyeitwa Mercy.

Kama kawa sisi SBP tunawatakia maisha yenye furaha tele na inshaalah tunasubiri "wajomba"


Thursday, November 13, 2008

Sisi kwa kumodifai!!

Yaani sisi wa TZ kutengeneza vitu vipya inaweza ikawa ngumu sana, lakini kwa kurekebisha walivyotengeneza wajapani.... sisi nooooma!! Hebu ona hii, nimeikuta kwenye blogu ya SUMO.

picture by http://mpoki.blogspot.com/

Msiba Kibosho

Mpendwa wetu na kaka yetu Erasmus Joseph Mmasi amefiwa na mama yake mzazi na mazishi yameanyika leo mchana huko Kibosho.

Kwa niaba ya wamiliki woote wa SBP tunapenda kutoa salamu zetu za pole kwa kaka Erasmus pamoja na familia yote ya Mmasi kwa msiba huu mkubwa uliowapata.

Mungu wa amani awakumbatie.

Tuesday, November 11, 2008

Nionvyo mimi.

Huyu hapa Obama, wengine wanasema Mtanzania, wengine eti mchaga kabisa (Obamaeli) ila mimi naona anafanana na Kikwete. Angalia vizuri wakicheka.

Huyu ni Kikwete, naona pia ukimtazama haraka haraka ni kama Obama vile. Hebu toa maoni hapo, wewe unawafananishaje?

Sunday, November 9, 2008

Weekend iliyopita

Naamini wadau woote kabisa mko fit na mnaendelea vyema na shughuli zenu za kila siku.
Weekend iliyopita nilikwenda kumsalimu babu yetu huko katika milima ya ugweno. Nilipiga picha kidogo ambazo naona itakuwa vyema na ninyi mkaziona.

Mlima Kilimanjaro unavoonekana ukiwa maeneo ya Bomang'ombe.


Huyo kijana wa katikati ndio mjanja wa kijijini, anaitwa Eliamani au Godlove G. Temba ni mtoto wa Uncle wetu anayeitwa Goodluck.


Nilipenda sana hili pozi la hawa marafiki wawili niliowakuta nyumbani kwa babu yangu. Yani huyo Mbwa hana noma kabisa akiwa na huyu Paka kiasi kwamba kuna wakati utakuta wanapiga stori zao na hakuna tatizo kabisa. Hapa walikuwa wameshiba na wanaanza kupata kausingizi ka mchana!!

Nice time wadau...