Tafuta/Search This Blog

Monday, January 19, 2009

SIKIA HI TULIPOKUA TUNATOKA TANGA KTK HAFLA YA Arusi ya BWN Thomas

Mkwakwani hapa maeneo ya Tanga Kunani. katika pitapita pita zangu niliona nikuchukulie kaeneo haka
Haya tena safari ya kuja Dar ilianza na Basi hili mali ya Tashrif Coach, namba za usajili za gari hilo ni hizi T286 AAF Mara ya kwanza maeneo ya Lisanga gari ikaharibika. Kufika Wami likaharibika tena. na hapo kagiza kalikua kanaanza kwa mbaliiiiii. Unajua nini? System ya Upepo ndio ilikua inasumbua. Mara likategeshwa tegeshwa tukaondoka.


Kumaliza wami tu likaharibika tena. safari hii giza lilikua totoro, hakuna uhakika wa kuondoka pale. Gari hili ndo yale yanayoongoza kwa ajali hapa Tanzania na hasa Tanga line.




Safari iliishia hapa Chalinze kama unavyoweza kuona katika picha ya hapo chini. Hawa jamaa walikua wakiitwa YARABISALAMA. (kama kumbukumbu zangu hazijapotea), wakapata ajali mbaya za mfululizo, wakabadili na kujiita No Challange na baadae Real No Challange. wakapata maajali ya kupitiliza, na kumalizia ile ya pale Muheza ktk Mto msangazi, makabadili jina na kujiita TAASHIRIF hata leo. Sasa inawezekana kabisa wakabadilisha tena. Mbona magari mengine hayapati ajali kama hizo?




Asubuhi yake hapa ndo tukaondoka hapa.


1 comment:

Anonymous said...

Maskini poleni sana wapenzi, Namshukuru baba wa mbinguni kwa kuwalinda anyway, otherwise ilikua si salama...Take care wakati mwingine mchukue mabasi ya bei mbaya jamani...
Mbarikiwe