Tafuta/Search This Blog

Saturday, January 24, 2009

Tumshukuru Mungu...

Tuna kila sababu ya kwenda mbele za Mungu kwa shukrani kila siku maana yeye anajishughulisha sana na mambo yetu.

Ninasema maneno haya maana kila siku mimi ninapita katika daraja la Nduruma ambalo karibu kila mwaka kunatokea ajali mbaya zinazochukua maisha ya waTanzania wengi.

Siku ya Jumanne tarehe 21 Jan 2009 nilipita kwenye daraja hilo asubuhi na mchana ikatokea ajali mbaya sana iliyochukua maisha ya watu zaidi ya 18. Nilipopita mahali hapo jioni baada ya ajali nilihisi machozi yakinilenngalenga na nikasema Mungu ninakushukuru kwa sababu umenipa nafasi nyingine zaidi ya kuishi.

Picha hizi nimepiga asubuhi hii wakati napita tena.


Picha kutoka ndani ya basi wakati tupo juu ya daraja.
Mbele kidogo ya daraja.
Hebu jaribu kujipa nafasi hata ya dakika moja na utafakari jinsi Mungu alivyokupitisha katika hatari mbali mbali na kukupa nafasi ya kuwa hai sio kwa sababu unastahili.
Tunawapenda!!

1 comment:

Anonymous said...

Pole sana kaka Gluv