Tafuta/Search This Blog

Monday, December 14, 2009

Usalama kwanza...


Kumekuwa na ongezeko kubwa sana la matumizi ya pikipiki kama chombo cha usafiri hapa Tanzania. Ni kweli kwamba kimerahisisha sana usafiri lakini kwa kweli suala la usalama kwa watumiaji wa chombo hiki limekuwa haliwekewi mkazo.
Nilikutana na bwana huyu kwenye barabara ya Moshi Arusha alikuwa hajavaa helmet na alikuwa anapeta tu na tulikuwa tumepishana na askari wa usalama barabarani aliyekuwa busy kuyasimamisha malori na mabasi ya abiria nadhani pia ni kwa sababu huko kuna rushwa.
Kuna kila sababu ya watumiaji wa vyombo hivi vya usafiri kuwa makini na kujali usalama wao kabla maafa hayajawakuta.
Nimewasilisha!!

1 comment:

Anonymous said...

Wengi huwa wanawaita hawa, 'organ dornors' maana wakipiga hiyo kichwa hapo chini kinachobakia ni kutumbua viungo vya ndani vizima kama figo hivi na kuwasaidia wagonjwa mahospitali maana hawa wanaoendesha pikipiki walishaamua kujiachia.

Usalama wako mwenyewe unataka ushikiwe fimbo? Kama ni kutokujua na ujinga sawa, askari awafunze, kama ni umasikini nalo jingine (sijui atanunuaje pikipiki ashindwe kuwa na helmet na kama ni ya kazini sidhani kama watakupa pikipiki udai helmet washindwe kukupa, hata wakishindwa, nunua yako) lakini kama ndiyo wale vichwa ngumu na wabishi, basi acha apate kitakachobishana naye (kifo au ajali) na tuone kama atakibishia.